WaTanganyika kaeni chonjo, kikulacho...

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Hii ni mara nyingine tena nikihusisha vurugu za Zanzibar na uwepo wa utawala wa CCM .Napendelea sana kusema ktk purukushani za Zanzibar mkono wa CCM upo au haukosi, kwani uwepo wa Muungano ni uhai wa CCM ,Muungano ukifa leo basi CCM ndio imeenda arijojo.

Kivipi CCM itayaona mauti ? Kufa kwa Muungano ni kubatilika kwa serikali ya Muungano ,ni kubatilika kwa Bunge na kubatilika au kufikia mwisho kwa vyombo vingine vyote vihusikavyo na Muungano. Inamaana Tanganyika itabidi iitishe uchaguzi mpya ndani ya kipindi kifupi pengine kisicho zidi miezi sita.

Mtihani mkubwa kwa wanaCCM kuweza kushinda tena au kurudi madarakani utakuwa mgumu na asilimia kubwa watafeli,uwepo wa Muungano au nguvu zinazotumika kulinda Muungano huu usivunjike ni kuhakikisha serikali ya Muungano inabakia madarakani na mradi wa kudhibiti vyombo vyote vya dola upo chini yao.

Hivi leo hii tukiamka tunasikia Muungano umevunjika ,Zanzibar wanaserikali hawatatetereka ,je huku Tanganyika unadhani kutatokea nini ,je CCM watakubalika kuendelea na uongozi au utawala ???
 
Kwa nini watu wa bara mnaungangania muungano?

Kwa nini wanasiasa wenu toka vyama vyenu vikuu (CCM na CHADEMA ) wanaupenda sana huu muungano?

Inafika mahala mtu kama Zitto Kabwe kuthubutu kusema kuwa Muungano ni "scared" hii inaashiria nini?

Muungano haukuwepo

Ukawepo

kwa nini kama hauna maslahi kwa watu na watu hawautaki kwa nini wansiasa wanaulazimisha kwa wananchi?
 
Acha utoto, hivi unakumbuka baada ya kauri ya Mh Pinda kuwa Zanzibar si nchi, JK alipohutubia bunge si aliwauliza wazanzibar na viongozi wake kuwa kelel za nini kama kuna lingine limejificha si mseme? sasa kama hamtaki muungano mbona hatukusikia hata wabunge wa Zanzibar wanatoka bungeni?

Mh Lisu hakuwakandya kwenye muungano, lakini kuna mbunge au mwakilishi alisema haji bara? na bado wabunge wa Zanzibar kimia wanadai tu wanachukiwa, acheni unafiki nyinyi
 
Kwa nini watu wa bara mnaungangania muungano?

Kwa nini wanasiasa wenu toka vyama vyenu vikuu (CCM na CHADEMA ) wanaupenda sana huu muungano?

Inafika mahala mtu kama Zitto Kabwe kuthubutu kusema kuwa Muungano ni "scared" hii inaashiria nini?

Muungano haukuwepo

Ukawepo

kwa nini kama hauna maslahi kwa watu na watu hawautaki kwa nini wansiasa wanaulazimisha kwa wananchi?

zanzibar huru
Umepigwa bana ukaanzisha na threaid nyingine! we kweli kiboko aisee

umepigwa ban ukaanzisha id nyingine! we kweli kiboko!

Chadema wameshasema wakinyakua nchi basi wanahakikisha Tanganyika inarudi na kuwepo serikali ndogo ya Muungano ,ni juzi tu nilisikia pale Jangwani. Au hamkuwasikia ?? Zitto yumo humu.Slaa yumo wanaweza kukataa kama hawakutamka naamini ni tamko la Chama.

Tatizo lipo wapi ??? Unafikiria CCM watawacha kuulinda Muungano ?? Chadema inaunga moja kwa moja uwepo wa serikali tatu ,hivyo wanaunga mkono harakati za WaZanzibari kiana ,nashindwa kuelewa ni kwa nini wanashindwa kuidai Tanganyika kwa sauti zenye nguvu na kueleweka zaidi kuliko kuegemea hali ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom