Watakaojaribu kudumaza Safari ya Rais Samia kuanzia 2021 kuelekea 2030 ni wasaliti, yafaa washughulikiwe mapema

Zanzibar nayo ni nchi! Arudi akagombee huko. Hussein Mwinyi ni mtu muungwana na muelewa sana. Atakubali tu kumuachia.

Ila kwa huku Tanganyika, namuomba atuachie nchi yetu. Maana kuna Watanganyika wengi tu wenye sifa kuliko yeye raia wa Visiwani.
Tunataka atawale mpaka 2030. Ikibidi hsya katiba ibadilishwe tumpe mwanya. Mama Samia ni hazina ya taifa.
 
Hazina ya Taifa lipi? La Zanzibar au Tanganyika! Kama ni Zanzibar sina tatizo. Ila kama ni hili Taifa letu la Tanganyika (Tanzania) hapa ndipo shida ilipo.
 
Watanzania wenzangu,

Aliyoyafanya kwa muda mfupi aliokaa madarakani ni makubwa na ameishangaza dunia

Kwa kutambua hilo sisi Watanzania tumeamua kwenda nae hadi 2030 na huo ndiyo utamaduni wetu

Juhudi zozote za kufifisha mpango huo mwema ni usaliti mkubwa unaotakiwa kushughulikiwa mapema kadri inavyowezekana

Tunataka Dunia nzima Itambue Kuwa Sisi Watanzania Kwa Umoja Wetu Tumeamua kuwa Mama ataendelea kutuongoza hadi 2030

Mama Samia Anao:

(1)Uwezo Wa Kutuletea Maendeleo Anao
(2)Nia Ya Kutuletea Maendeleo Anayo
(3)Sababu Za Kutuletea Maendeleo Anazo

KaziIendelee

Paza Sauti Yako Ewe Mtanzania - 2021-2030 ni zamu ya Rais Samia Suluhu Hassani
Comments reserved
 
Hazina ya Taifa lipi? La Zanzibar au Tanganyika! Kama ni Zanzibar sina tatizo. Ila kama ni hili Taifa letu la Tanganyika (Tanzania) hapa ndipo shida ilipo.
Hilo kundi lenu sasa linatumia propaganda ya Uzanzibar kupandikiza chuki kwa Watanzania bara ili wamchukie mama. Kila mtu anajua hizi nchi zimeungana na rais anaweza kutokea sehemu yeyote ya muungano.
 
Unazungumzia tumbo lako na sio Mama Samia kuwa kiongozi.
Hata wakati wa Jiwe mlisema hakuna mtu Tz anafaa ila mmeishasahau.
Sema wazi kwamba hapo unamaanisha matumbo yenu.
 
Hilo kundi lenu sasa linatumia propaganda ya Uzanzibar kupandikiza chuki kwa Watanzania bara ili wamchukie mama. Kila mtu anajua hizi nchi zimeungana na rais anaweza kutokea sehemu yeyote ya muungano.
Mimi ni Mtanganyika halisi kutoka Tanga. Na kwa taarifa yako sijaanza leo kulitetea Taifa langu dhidi ya Muungano wa kinafiki na wenye manufaa kwa upande mmoja tu.

Hivyo utakuwa umekosea kunihusisha na kundi lolote lile! Ukweli ubakie kuwa ukweli. Hakuna sababu kama nchi kutawaliwa na raia wa nchi nyingine.
 
Mliobahatika kupata nafasi ndani ya huu utawala mna haki ya kuongea hivi kama kasuku,lakini tuliofanyiwa kila aina ya figisu na udhalimu kwa serikali hii,tunaona mama hatoshi..muda utaongea

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Nchi siyo club ya kandanda. Yaani watanganyika milion 60 tumekoswa mtu wa kuongoza mpaka tukodi mtu kutoka kwenye kanchi ka watu elifu 500
Watanzania tunamtaka SSH aongoze mpaka 2030. Mama yetu mpendwa anatosha! Kazi iendelee!!! 💪🏾💪🏾💪🏾
 
Mimi ni Mtanganyika halisi kutoka Tanga. Na kwa taarifa yako sijaanza leo kulitetea Taifa langu dhidi ya Muungano wa kinafiki na wenye manufaa kwa upande mmoja tu.

Hivyo utakuwa umekosea kunihusisha na kundi lolote lile! Ukweli ubakie kuwa ukweli. Hakuna sababu kama nchi kutawaliwa na raia wa nchi nyingine.
Wewe ni mnafiki tu, huna uzalendo wowote. Ungekuwa mzalendo wa kweli usingekuwa unaongopa kuwa rais wetu mpendwa ni raia wa nchi nyingine. Unajua unachokifanya, unapiga propaganda za kumfanya mama achukiwe na Watanzania bara kwa kuamsha hisia zao eti wanatawaliwa na raia wa nchi nyingine. Yaani nashangaa USALAMA WA TAIFA uko wapi mpaka sasa kwa kuwaacha watu kama nyie kuendelea kusambaza propaganda za uongo.
 
Wewe utakua ni mjinga wa kiwango cha juu sana! Mimi kama raia wa Tanganyika nina haki ya kulipigania Taifa langu kwa nguvu zote. Hakuna Mtanganyika mwenye akili timamu, asiye tambua fika udhaifu wa Muungano tulio nao.

Sasa hizo chuki namjaza nani, na wakati ukweli uko wazi! Halafu eti unakimbilia kwa usalama wa Taifa kunishughulikia!! 😁😁 Stupid!! Usalama wa Taifa upi? Ule wa uvccm ya akina Lengai Ole Sabaya, au ule halisi ambao hata mimi kama raia mwema wa nchi hii nautumikia?
 
Wewe sio raia mwema. Raia mwema haongopi kuhusu uraia wa mtu. Raia mwema hachochei hisia za watu kwa kutaka kuwagawa kwa kutumia sehemu walizotoka.

Wewe ni mtu hatari sana kwa nchi hii na inafaa uangaliwe vizuri.
 
Tunataka atawale mpaka 2030. Ikibidi hsya katiba ibadilishwe tumpe mwanya. Mama Samia ni hazina ya taifa.
Kukosekana kwa umoja wa kitaifa hudumaza uchumi wa nchi .Tanzania uchaguzi tulioshuhudia 2020 hauhitaji kufikiria kupiga kura tena ndiyo maana wadau wamekuja na kauli mbiu ya katiba mpya maana ulikuwa ni uchafuzi
 
Watanzania wenzangu,

Aliyoyafanya kwa muda mfupi aliokaa madarakani ni makubwa na ameishangaza dunia

Kwa kutambua hilo sisi Watanzania tumeamua kwenda nae hadi 2030 na huo ndiyo utamaduni wetu

Juhudi zozote za kufifisha mpango huo mwema ni usaliti mkubwa unaotakiwa kushughulikiwa mapema kadri inavyowezekana

Tunataka Dunia nzima Itambue Kuwa Sisi Watanzania Kwa Umoja Wetu Tumeamua kuwa Mama ataendelea kutuongoza hadi 2030

Mama Samia Anao:

(1)Uwezo Wa Kutuletea Maendeleo Anao
(2)Nia Ya Kutuletea Maendeleo Anayo
(3)Sababu Za Kutuletea Maendeleo Anazo

KaziIendelee

Paza Sauti Yako Ewe Mtanzania - 2021-2030 ni zamu ya Rais Samia Suluhu Hassani
Rais jana alimuenzi Bibi Titi kwa ni pamoja na ujasiri wake kukosoa bila hofu hoja ya yeyote anapoona ina mapungufu.

Vipi unapingana na rais wako?
 
Mama hauziki.achukue chake mapema.Nani hadi sasa ajajenga airport kijijini kwake,bahati haiji mara mbili.
 
Kukosekana kwa umoja wa kitaifa hudumaza uchumi wa nchi .Tanzania uchaguzi tulioshuhudia 2020 hauhitaji kufikiria kupiga kura tena ndiyo maana wadau wamekuja na kauli mbiu ya katiba mpya maana ulikuwa ni uchafuzi
Shetani keshafungwa minyororo kwanini tusipige kura
 
Wewe sio raia mwema. Raia mwema haongopi kuhusu uraia wa mtu. Raia mwema hachochei hisia za watu kwa kutaka kuwagawa kwa kutumia sehemu walizotoka.

Wewe ni mtu hatari sana kwa nchi hii na inafaa uangaliwe vizuri.
Nchi hii inahitaji raia wema, wazalendo na wasema kweli kama mimi. Muungano wetu ndiyo chanzo cha huu mgawanyiko! Haiwezekani Wazanzibar wajitambulishe kwa Uzanzibar wao, halafu Watanganyika ndiyo tuonekane ni Watanzania.

Kama vipi kila nchi ijitawale! Au turudi kwenye Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba, inayo unga mkono uanzishwaji wa Serikali tatu. Serikali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Serikali ya Tanganyika, na ile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar!

Na hivyo Serikali ya Tanganyika iongozwe na Watanganyika wenyewe, ile ya Zanzibar iendelee kuongozwa na Wazanzibar wenyewe! Na Serikali ya Muungano iongozwe kwa kupokezana. Rais akiwa Mzanzibar, Makamu awe Mtanganyika. Na Baada ya mihula miwili kupita, Tanganyika nayo inashika madaraka.
 
Back
Top Bottom