Wakuu hili ni haswaa,wachina wapo tata sana,elimu yao imekaa kimtegomtego,nina maana ukiivagaa tu umeumia,Ni kweli kuna wachina wengi hujazana nje,na hii ni kwa sababu kuu mbili,
Moja,nchi huwa inawapeleka watu nje kwenda kuiba ujuzi then kurudi nao nyumbani,na wengi wanaopelekwa na serikali ni watu wa Phd au Masters,huwezi kusikia undergraduate kapelekwa nje na serikali kwani wenyewe wanaamini kuwa kumjua adui yako ni moja ya ushindi.
Pili.Kwa china ili uingie vyuo vilivyo kwenye kumi bora,kama hichi ninachosoma na upate kozi murua,kusema kweli ni kazi ya ziada,ndio maana ukiwaona wachina hapa wa zile kozi tamu kama Computer ,telecom,MIS,...huwa kama mibwege hii kutokana na mzigo unaowakabili na ushindani.sasa wale watoto wa wenye hela wanaona isiwe tabu ni bora nimpeleke mwanangu nje.
La mwisho, wachina ni wasanii,kama haupo makini unaweza ukajikuta unapelekwa chuo sicho au wakikupeleka chuo kizuri basi unapewa kozi za ajabu,la msingi ni kujua haya kabla hujaja ndio maana nikawaalert watu mapema.
Kama utaweza kukabiliana na haya yote,mimi naona kwa fani za science,unaweza kuja China kwani jambo zuri ni kuwa kama unajua kichina vizuri,basi wao material yapo wazi sana kwa watu wao,centers zipo kibwena,nina hakika 100% utatoka ukiwa fiti tena ukizingatia kwa mwendo tunaoenda ni kuwa zaidi ya 50% ya technology yetu tunawategemea wachina,hivyo lazima wapatikane watu ambao wanawaelewa wachina vzuri.
Ila usisahau,kusoma china kimtindo kunahitaji kujizira ili uweze kufikia lengo kwani wazugaji ni wengi na wanakatisha tamaa saaaaaaaaaaaana.penye nia pana njia wakuu.