Watahiniwa 646,148 kufanya mtihani Kidato cha Pili leo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Watahiniwa 646,148 wamesajiliwa kufanya mtihani wa upimaji wa kidato cha pili unaotarajiwa kuanza Jumatatu Novemba 9 hadi Novemba 20, 2020.

Kati ya watahiniwa hao wavulana ni 301,831 sawa na asilimia 46.71 na wasichana ni 344,317 sawa na asilimia 53.29.

Akizungumza Jumapili Novemba 8, 2020 Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk Charles Msonde amesema idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 5.7 ikilinganishwa na watahiniwa waliofanya mtihani huo mwaka 2019.

Amesema kati ya watahiniwa hao wapo wenye mahitaji maalum 731 wakiwemo 406 wenye uoni hafifu, 55 wasioona, 267 wenye ulemavu wa viungo na watatu wenye ulemavu wa kusikia.

Sanjari na kidato cha pili, katibu mtendaji huyo ameeleza kuhusu upimaji wa darasa la nne unaotarajiwa kufanyika Novemba 25 na 26, 2020.

Amesema wanafunzi 1,825,679 wamesajiliwa kufanya mtihani huo wa upimaji wakiwemo wavulana 909,068 na wasichana 916,611.
 
Siku hizi mtihani wa kidato cha pili sio wa kuchuja wanafunzi wanaoingia kidatu cha tatu bali ni assessment tu. Inamaana wote watakaofanya mitihani yao hatimaye wataruhusiwa kuendelea na kidatu cha tatu bila kujali ufaulu wao!
 
Hao watoto wengi wana ndoto za kuwa waajiriwa.
Then miaka 6 mbele uje kuwaambia ajira hakuna nendeni mkajiajiri.
Na wametumia miaka mingi kukariri karibu robo ya uhai wao wote.

Serikali hamjachelewa badilisheni mfumo wa elimu ili utengeneze vijana wabunifu wagunduzi waona fursa na watengeneza ajira hapo utatengeneza vijana wanaojitambua na kujielewa na sio kutengeneza wasomi wengi ambao wanaenda kuomba ajira.

Ina maana walichosoma na miaka yote waliyotumia ni worthless.
 
Back
Top Bottom