Watafsiri wa Lugha za alama TBC

Watafsiri wa Lugha za alama TBC

IKWETE

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
4,057
Reaction score
696
Hivi karibuni kulitokea mvutano Bungeni kati ya Tundu Lissu na Spika wa Bunge.Baada ya mvutano ule Tundu Lissu alianza kuchangia hoja ya Mbatia kuhusu Prof. Lipumba.

Siku hiyo nilikuwa nyumbani nilipata wageni mmoja wa wageni hao alikuwa mlemavu wa kutoongea anayeweza kuandika na kutafsiri lugha za alama.

Wakanikuta natazama TBC1 bunge. Tundu Lissu alipomaliza kumwaga point nilimwandikia kikaratasi yule mlemavu kumuuliza msemaji alikuwa amezungumza nini( lengo lilikuwa kutest kama wale wakalimani wa lugha za alama hawapotoshi.

Ukweli ni kuwa wanadanganya sana. Yule mkalimani wa TBC alikuwa anawadanganya watu wa Lugha za alama kuwa Tundu Lissu ameipongeza serikali kwa maendeleo ya Watanzania.

Kwakuwa hawa walemavu nao ni wapiga kura, wanadanganywa sana wakiaminishwa CCM ndio kila kitu na wakati wa kupiga kura wanaipigia CCM.

UKAWA anzisheni TV Zenu.
 
ah hahaha haha aaa haha ahahaaaaa hahaaaaaaaa hahaaaaaaaaaaaaaaaaa hahahahaaaaaaaaaaaa hahahaaaaaaaaaaaaaa hahaaaaaaaaaaaa hahaaaaaaaaaaaaaaaaaa hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa haaaaaaaaa............mkuu kama ni kweli you have made my day, Bongo ni zaidi ya uijuavyo
 
Una hakika huyo mkalimani wako anaijua vizuri lugha ya alama?,isije kuwa huyo wa kwako ndo mchemkaji...
 
Hivi karibuni kulitokea mvutano Bungeni kati ya Tundu Lissu na Spika wa Bunge.Baada ya mvutano ule Tundu Lissu alianza kuchangia hoja ya Mbatia kuhusu Prof. Lipumba.

Siku hiyo nilikuwa nyumbani nilipata wageni mmoja wa wageni hao alikuwa mlemavu wa kutoongea anayeweza kuandika na kutafsiri lugha za alama.

Wakanikuta natazama TBC1 bunge. Tundu Lissu alipomaliza kumwaga point nilimwandikia kikaratasi yule mlemavu kumuuliza msemaji alikuwa amezungumza nini( lengo lilikuwa kutest kama wale wakalimani wa lugha za alama hawapotoshi.

Ukweli ni kuwa wanadanganya sana. Yule mkalimani wa TBC alikuwa anawadanganya watu wa Lugha za alama kuwa Tundu Lissu ameipongeza serikali kwa maendeleo ya Watanzania.

Kwakuwa hawa walemavu nao ni wapiga kura, wanadanganywa sana wakiaminishwa CCM ndio kila kitu na wakati wa kupiga kura wanaipigia CCM.

UKAWA anzisheni TV Zenu.

Hahahaha umenikumbusha yule wa Mandela...hahaha
 
ah jamani acheni dhami na tuwe wakweli. Tusizungumze jambo ambalo hatuna uhakika nalo kisa tu tumesikia.
Lazima muelewe kuwa sio kila kiziwi anajua lugha ya alama, ni lazima huyo kiziwi awe ameenda shule au amejichanganya sana kwenye makundi ya viziwi ndo atajua hiyo lugha.
Binafsi naijua hiyo lugha vyema sana nimeisomea degree katika elim maalum naijua kuliko na kuna muda huwa nafanya hiyo kazi ya kutafsiri pia.
Mimi mara nyingine huwa nawapima uwezo wao hakika ni mzuri tu na huwa wanatafsiri kinachozungumzwa niamini mimi.
Mara nyingine huwa najaribu kutoa sauti kwenye tv ili kuona kama naweza elewa na ujumbe naupata vyema.
Mkuu huyo kiziwi wako kakupoteza na ukitaka kujua angalia cv yake lazma atakua hajasoma tu.
Lugha wanayotumia pale ni lugha ya alama ya taifa we kiziwi wako atakua anajua ya mtaani hivyo akiangalia pale inakua ni kama wewe unavyoangalia chanel ya kichina
 
Back
Top Bottom