Wataalamu wa Wizara ya Mifugo tusaidieni; Kuchunga mbuzi na ng`ombe pamoja kunapunguza magonjwa?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,653
2,000
Nimeona huu utafiti hapa je una ukweli wowote .Wataalamu wa mifugo tusaidieni

00127.jpg

SOURCE:The Uganda journal
 
Laface77

JF-Expert Member
Jul 9, 2008
2,116
2,000
Ni kweli kabisa ila ukimchanganya Daudi Albert Bashite na Faru Yohana unapata chuki, visasi na vinyongo katika taifa!
 
srinavas

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
3,481
2,000
ookey. nishajua. kumbe mleta mada ni mdau mkubwa wa bashite na genge lake. ...
 
Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
1,849
2,000
Nimeona huu utafiti hapa je una ukweli wowote .Wataalamu wa mifugo tusaidieni

00127.jpg

SOURCE:The Uganda journal

Japokua swali lako umelielekeza moja kwa moja kwa "wataalam wa wizara", naomba tu nikujibu kama mtaalam (si wa wizara).

Kwenye huo waraka wa tafiti uliouambatanisha imeelezwa ni namna gani kuchunga ng'ombe na mbuzi kwa pamoja kunaweza kupunguza " ugonjwa" wa ndigana kali yaani East Coast Fever kwa ng'ombe.

Imeelezwa kwamba baadhi ya wale kupe wanaobeba vijidudu vya ndigana wanaoitwa Rhiphicephalus appendiculatus watawashambulia mbuzi na hivyo kupunguza uwepo wao kwa ng'ombe. Kuwashambulia mbuzi kunawafanya kupe hao kutoeneza ugonjwa maana ndigana ni ugonjwa wa ng'ombe tu. Kwa kifupi ujumbe uliopo kwenye kiambatanisho chako ndio huo. Kwa muktadha huo, jibu langu ni "NDIYO, kuchunga ng'ombe na mbuzi pamoja kunapunguza UGONJWA wa ndigana Kali".

Nikijikita kwenye swali lako haswa kama lilivyo (je kuchunga ng'ombe na mbuzi kwa pamoja kunapunguza MAGONJWA ?)
As long as magonjwa is concerned, jibu langu ni HAPANA. Kitendo hicho cha kuchanganya ng'ombe na mbuzi kinaongeza uwezekano wa maambukizi kutoka kwa ng'ombe kwenda kwa mbuzi na kinyume chake hasa kwa yale magonjwa ambayo wanaathiri makundi yote ya wanyama waliotajwa.
Magonjwa hayo yanaweza kuenezwa kwa njia ya mgusano, njia ya hewa au wadudu kama kupe, ndorobo, n.k (vectors). Magonjwa hayo ni kama vile TB, Anaplasmosis (ndigana baridi), Heart water, homa ya miguu na midomo, na mengineyo.

Nini kifanyike:
Changanya ng'ombe na mbuzi kwa kadri unavyoweza ila lengo lisiwe kupunguza magonjwa, fuata njia muafaka za kuzuia magonjwa kwenye makundi yako ya mifugo kama vile chanjo, kuogesha Mara kwa Mara kuzuia makupe, kuwapa dawa za minyoo kwa wakati, usafi, lishe bora, na kuwapatia matibabu stahiki pale wanapougua.

Ninakutakia ufugaji mwema, kama una swali karibu.
 
asante mtaalamu kwa jibu zuri.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom