Mbona Makondakta wa siku hizi wapole sana na ni wastaarabu, wale wa zamani walikuwa wana style za kuburuza miguu chini huku kaning'inia hatari, na kushuka kwake hushuka gari ikiwa bado kwenye mwendo na hiyo humpa utamu flani wa kuipenda kazi, inamchangamsha kwa kufanya hivyo, achilia mbali kupigwa kwa gari, ilikuwa inaitwa kupigadebe, yaani gari inapigwa hadi panalemaa na uhitaji wa kunyooshwa ufanyike, lakini siku hizi unakuta konda anadandia kiustaarabu kabisa.
Kukimbilia gari kwao ni sehemu ya kufurahishwa kwao ili kujichangamsha kikazi zaidi.