Kutosha kwa gesi kunaendana na matumizi yako binafsi hakuna anayeweza kukuhakikishia. Kama unaishi karibu na machinjio au mfugaji utaishi kwa raha, pipa imara la plastiki linafaa na ukubwa ulingane na matumizi yako.Mie nilikuwa nataka kujua kutengeneza huo mtambo kwa kutumia pipa la plastic mfano hilo hapo juu, unaweza pata gas ya kutosha?
Nina Ng'ombe 5 na familia ya watu 8, kama kawaida kunapikwa mara 3 kwa siku. unafikiri pipa la lita 300 linatosha? nimeangalia kwny youtube nimeona pia wengine wanaweka maji kwenye pipa la pili kisha gas inayozalishwa kutoka pila la kwanza inaingizwa humo kwenye pipa la 2, nini faida yake kiufundi?Kutosha kwa gesi kunaendana na matumizi yako binafsi hakuna anayeweza kukuhakikishia. Kama unaishi karibu na machinjio au mfugaji utaishi kwa raha, pipa imara la plastiki linafaa na ukubwa ulingane na matumizi yako.
0753991378 huyu amenitengenezea yangu, hivi sasa anatengeneza dar zoo, yuko vizuriNi link nao mkuu
Bro uko sahihi sana,kasoro hapo kwenye kinyesi cha mtu:Jibu ni kuwa kinyesi cha mtu kinapitia action ya enzymes nyingi sana kuanzia mdomon hadi kwenye colon hivyo kina assimilation i.e uptaken ya nutrients kuinhia kwenye damu ni kubwa au iko effective sana kiasi kwamba kinyesi kinakua hakina kabisa nutrients,zaidi ya residualsMbolea fresh inafaa zaidi kuliko iliyokauka au iliyokaa muda mrefu lakini sio lazima.
Kwa hiyo kwa wale wanaotumia mifugo yao wenyewe wanakuwa na advantage ya kupata mbolea ambayo iko fresh, tofauti na wale ambao wananunua maana inakuwa imekaa kwa muda na baadhi ya gesi zinakuwa "zimeyeyukia hewani".
Kinyesi cha mwanadamu ni kizuri sana, tatizo linakuja kwenye sheria za nchi maana kitaalamu kinyesi cha mwanadamu kinabeba maradhi mengi sana yanayomuathiri mwanadamu.
Sidhani kama watu wa afya na mazingira wanaweza kukuruhusu kukitumia, maana unaweza kusababisha milipuko mizito sana ya magonjwa kwa watu na ikawa tatizo kwa wengine, labda kama una mitambo ya kuhakikisha kuwa unaua vimelea vyote vya magonjwa kabla ya kuitumia.
All in all sio lazima kutumia kinyesi tu ili kuzalisha umeme kwa njia hio, kwa teknolojia ya sasa unaweza kutumia pia matakataa ya jikoni au kifupi anything organic ambacho kinaweza kuoza haraka.
Fuatilia humu JF kuna nyuzi zinazungumzia sana hili.