Asante sana mkuu kwa kunielewesha ila bado na maswali kwakua nataka kufahamu..
Nahitaji niunde amplifier kwa kutumia ic mbili za tda 2030 na 2050
yani moja itoe bass au woofer na ic nyingine ya pili itoe sauti ya kawaida kama tuita.
Je? niiunde vipi ic moja itoe bass au woofer maana ndicho kinacho nisumbua mkuu nisaidie
Inawezekana, kama mkuu
Hazchem plate alivyosema. Inabidi uwe na pre amp inayoweza kiprocess signal itakayoenda kwenye IC (Amp ya kwanza) kama Trebble, na pia signal ya pili itakayoenda kwenye Amp ya pili ikiwa kama Bass.
Kifupi hapo kinachofanyika na hiyo pre-amp ni ku-Equalize signal kama trebble au bass.
Njia ya kienyeji ya kufanya hiyo bila kutumia pre-amp, ni kufunga ceramic capacitor in series kati ya input ya amplifier na source signal , hapo utapata trebble.
Na unapofunga ceramic/ electrolytic (polarity) capacitor in parallel kwenye input ya amplifier basi utapata bass.
Hizo capacitors inabidi uwe nazo zenye value tofauti tofauti ili ufanye majaribio ya bass au trebble unayotaka.
Kumbuka kama unaunda amp mbili (yaani input/output zaidi ya moja), basi pale kwenye input ni lazima kila line ya input inatakiwa iwe na volume controll yake (variable resistor) , kwa idadi sawasawa na idadi ya input/output. Hii itakusaidia pia baadae utaweza kubalance speaker LEFT na RIGHT.
Power supply pia ni vyema ikawa ina output zinazojitegemea kwa kila amplifier na current ya kutosha.
Sent from my Nokia 2.1 using Tapatalk