Wastara: Kuvunjika kwa ndoa kumenipa amani, nikipata mtu niko tayari kuolewa tena

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Wastara-Juma.jpg

Msanii wa filamu Wastara Juma amefunguka na kuzungumzia kuvunjika kwa ndoa yake na Mbunge wa Donge kupitia CCM Sadifa Khamis Juma ambayo imeduku kwa kakribani miezi 3.

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Wastara amesema mahusiano ya mapenzi ni kama mtu anavyoishi na rafiki yake, mkizinguana maachana.

“Binafsi kwa sababu ni muda mchache naumia kuwakarahisha mashabiki wangu kwa sababu hawamchukulii Wastara katika stori hizo au katika muonekano huo,” alisema Wastara. Lakini kwa upande wangu naona ni bora zaidi nilivyotoka mapema kwa sababu pengine ingeniathiri nikashindwa kufanya kazi zangu na kulea wanangu,”

Wastara alisema hawezi kuzungumzia chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake kwa kuwa yale ni maisha yake ya ndani.

Pia Wastara amesema bado umri wake unamruhusu kuingia tena kwenye mahusiano, ukifika wakati amempata mtu sahihi ataolewa tena.
 
It's all about diginity! Huwezi kuolewa au kama roho yako inasita acha!
Sio ndoa mnazifanya kama mchezo wa kombolela, mfyuuuuuu japo mi bado shabiki yako.
 
asigwa...! Huyu mdada Ni muongo sana, last week nimekutana Na mshenga wa hiyo harusi yake Na muheshimiwa, ameniambia ukweli Na chanzo cha ndoa kuvunjika....!
Sababu moja dada anampenda sana kuonekana kwenye habari all the time....!
Na mengine mengi....!
Ila Kwa ufupi kajiachisha mwenyewe....!
 
acheni aolewe .kwani inawahusu nini? mbona hao waoaji wa kila siku hamuwasemi.
wanaume hawastahili huruma yoyote ukiwapata unawapiga tu unasepa
 
Kwani lazima kuolewa? Kwann asiji pange tu afanye mambo yake? Kwani yeye mgeni wa ndoa? Anakimbilia nn?? Atulia mpaka badae sana anaweza tokea mwanaume wa kumpenda kwa shida na raha
 
acheni aolewe .kwani inawahusu nini? mbona hao waoaji wa kila siku hamuwasemi.
wanaume hawastahili huruma yoyote ukiwapata unawapiga tu unasepa
Aisee! unawapiga unasepa?! Wakati lengo lake la kukusigina limetimia, sina shaka na wewe ni wa mwambao.
 
asigwa...! Huyu mdada Ni muongo sana, last week nimekutana Na mshenga wa hiyo harusi yake Na muheshimiwa, ameniambia ukweli Na chanzo cha ndoa kuvunjika....!
Sababu moja dada anampenda sana kuonekana kwenye habari all the time....!
Na mengine mengi....!
Ila Kwa ufupi kajiachisha mwenyewe....!
Dah, kwa hiyo hizi mbwembwe za kulalamika kwenye media kila siku ni kutafuta sympathy au nini??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom