Wastahafu ambao hawajasafirishwa kwenda makwao serikali itawasafirisha lini?

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Lipo jambo la kushangaza ambalo jamii, vyombo vya kisheria na asasi za kiraia zimelifumbia macho.

Wapo wazee waliostahafu mpaka hata miaka mitatu iliyopita lakini mpaka leo hawajasafirishwa,kwa maana kwamba hawajalipwa nauli ya mizigo na likizo ya mwisho.

Upo mpango wa kuipeleka serikali mahakamani kwa kukiuka sheria iliyojitungia yenyewe.Mimi ndio maana ni mmoja wa wale wanaoamini kwamba kuhangaika kutunga katiba mpya is a waste of energy,time and tax payers' money.

Kama wapo wanasheria JF tunaomba ushauri wa awali.Moderator naomba usiondoe thread hii tafadhali,maana mnaona kila thread against the government ni ya kufuta.

Please be impartial.
 
Mkuu ni wazo zuri sana. Mimi mwenyewe nimestaafu july mwaka huu. Shida ilikuja kwenye malipo ya nauli na mizigo kama ulivyosema. Kwa miezi miwili, (Agosti na Septemba) nimekuwa nazungushwa eti OC hajafika na ilipofika ilieleiezwa kwenye malipo mengine! Nilichokifanya ni kuandika madai ya posho ya kujikimu kwa siku zote ambazo wamenikalisha hapa mjini badala ya kunirudisha nyumbani kulingana na Mkataba wangu na Muajiri baada ya kustaafu. Baada ya kumlima muajiri wangu barua hiyo, amefunguka na amenilipa fedha
ya nauli na mizigo yote! Fedha hizo amezilipa toka Development! Nilimtahadharisha kuwa ikibidi malipo yangu atayalipia Mahakamani. Mtumishi wanakujali kiasi ukiwa kazini lakini ukistaafu basi inakula kwako( rejea wazee wa jumuiya ya EA).
 
Back
Top Bottom