Wastaafu - Kuongeza ubora wa maisha

Wastaafu - Kuongeza ubora wa maisha

pmwasyoke

Platinum Member
Joined
May 27, 2010
Posts
4,982
Reaction score
3,787
Naomba wastaafu na wastaafu watarajiwa tuutumie uzi huu kushauriana mambo kadhaa yahusuyo masilahi ya wazee kama:

(a) Jinsi ya kupitisha muda - maana masaa 24 kwa siku ni mengi. Tatizo hili ni hasa kwa wale ambao shughuli walizojiandalia kujikimu zinajiendesha bila kuhitaji muda wao mwingi;
(b) kwa wastaafu ambao kujikimu ni shida kutokana na maandalizi hafifu au kipato kidogo wakati wa ajira - mawazo kuhusu shughuli za kujipatia/kujiongezea kipato japo kidogo - kwa waajiriwa wajue kwamba kwa walio wengi mifuko ya hifadhi ya jamii hutoa kipato duni mno;
(c) Matibabu, bima za afya zihudumiazo wazee;
(d) Mbinu mbalimbali za kuongeza ubora wa maisha ya uzeeni;
(e) Kwa wasioifikia hatua hiyo, mbinu za kujiandaa ili kuongeza ubora wa maisha uzeeni;
(f) n.k.

Hili linatuhusu wote kwani hata ukiwa na umri wa miaka 30 au pungufu utafika huko.

Karibuni.
 
Nashauri tuanzishe chama cha wastaafu ndicho kitakuwa chombo cha kutetea maslahi yetu na kishairi wasyaafu watatajiwa. Natamani tujiorodheshe humu na tuliwa idadi nzuri tupange tikutane tichague uongozi wa muda.
 
Back
Top Bottom