Wassira yuko sahihi kabisa

Wassira yuko sahihi kabisa

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,571
Kauli ya STEVEN wasira kuwa Rais Jakaya Kikwete kukutana na Vyama vya upinzani wwkiwemo UKAWA hakutabadili msimamo wa Wabhnge wa CCM wa serikali 2 iko sahihi kabisa kwa sababu kuu moja nayo ni:

Wapinzani wameitwa na rais, lakini, hata kama angewaita kama Mwenyekiti wa CCM, bado wabunge wake wana haki ya kutokubaliana naye kwa kile atakachoafikiana na wapinzani. Labda hapa niwaulize swali wale wanaobeza kauli ya Mzee Wasira na hasa UKAWA. Muungano wa UKAWA ni Muungano wa MBATIA, MBOWE na LIPUMBA au ni muungano wa vyama vya NCCR, CHADEMA na CUF? Kama jibu ni muungano wa vyama na siyo watu, basi msimamo wa UKAWA kutorudi bungeni ni msimamo wa wabunge wote wa vyama vinavyounda UKAWA. Vivyo hivyo msimamo wa serikali 2 ni msimamo wa Wabunge wote wa CCM na siyo wa JK.
 
Hana usahihi wowote ccm wanafuata upepo,akisema leo jk ni tatu kesho wote watashabikia tatu hadi utashangaa.
 
Ndiyo faraja mnayokwenda nayo ikuku? Naona kumbe mmependa kumshika mkono rais wenu, nendeni
 
Mbona mnjishitukia mapema subirini JK akapigwe hoja za msingi ndio mtajua UKAWA ni nani.!
 
CCm yenyewe ukitaka kufahamu misimamo yao,waruhusu "kura ya siri".Wasira na wenzake wachache akina Lukuvi ndio wana maslahi na serikali mbili,wanajua kiama chao ni serikali Tatu.
 
Wakishakutana , usije ukapotea ndugu yangu idawa, uje urudie haya maneno yako, naona mnamuona Jk kama mtu wa wasiwasi sana, mjeshi yule
 
Kama walivyo akina arfi, leticia na Shibuda?
 
Ndiyo faraja mnayokwenda nayo ikuku? Naona kumbe mmependa kumshika mkono rais wenu, nendeni
JK kawageuka ........ila ni kawaida yake kuwa na ndimi mbili .....ugua kimya kimya .......
 
Wakishakutana , usije ukapotea ndugu yangu idawa, uje urudie haya maneno yako, naona mnamuona Jk kama mtu wa wasiwasi sana, mjeshi yule
Kumbuka hii si mara ya kwanza UKAWA kutaka kukutana na JK na JK alionyesha dalili za kuwasikiliza, lakini CCM walizuia unajua kwa nini.

CCM wanahofu wanajua JK akikutana na UKAWA lazima kuna kitu kitabadilika kwa mchakato mzima.

Kwa nini Wasira aseme CCM watabaki na msimamo wao wa serikali Mbili, anajua ni kitu kitaenda kujadiliwa au ni hofu isiyo na msingi.
 
wewe ni mburura wa kutosha, kama CCM wanaweza kuwa na uwezo wa kumzuia JK asikutane na UKAWA , wanashindwa nini kukataa kile walichoafikiana na UKAWA?
 
Waacheni UKAWA wakapige ile kitu pale mezani warudi
juiceikulu.jpg
 
JK kawageuka ........ila ni kawaida yake kuwa na ndimi mbili .....ugua kimya kimya .......

Sasa hivi mnamuona wa maana, sasa muwe wavumilivu pale UKAWA wenu watakapotoka Ikulu wameinamisha vichwa chini
 
Mkuu thatha mie sina tabu na wewe wala Mzee wa pori, a.k.a Sokwe, a.k.a Wasira!
Hayo ni maoni yenu ya kikatiba na haki yenu kuwa na misimamo.
Mambo yote wacha tukutane kwa wananchi wakati wa kupiga kampeni za kukubari au kukataa hiyo katiba pendekezwa.
Hapo ndo maala maalum pa kumwaga sera mpaka kuwashawishi wananchi kuikubari au kuikataa.
Shida yangu ni kwamba pesa za wavuja jasho zinaliwa bure kwani katiba haiwezi pita kwa wananchi bila kukubalika kwanza kwa UKAWA.

Kauli ya STEVEN wasira kuwa Rais Jakaya Kikwete kukutana na Vyama vya upinzani wwkiwemo UKAWA hakutabadili msimamo wa Wabhnge wa CCM wa serikali 2 iko sahihi kabisa kwa sababu kuu moja nayo ni:

Wapinzani wameitwa na rais, lakini, hata kama angewaita kama Mwenyekiti wa CCM, bado wabunge wake wana haki ya kutokubaliana naye kwa kile atakachoafikiana na wapinzani. Labda hapa niwaulize swali wale wanaobeza kauli ya Mzee Wasira na hasa UKAWA. Muungano wa UKAWA ni Muungano wa MBATIA, MBOWE na LIPUMBA au ni muungano wa vyama vya NCCR, CHADEMA na CUF? Kama jibu ni muungano wa vyama na siyo watu, basi msimamo wa UKAWA kutorudi bungeni ni msimamo wa wabunge wote wa vyama vinavyounda UKAWA. Vivyo hivyo msimamo wa serikali 2 ni msimamo wa Wabunge wote wa CCM na siyo wa JK.
 
Sasa hivi mnamuona wa maana, sasa muwe wavumilivu pale UKAWA wenu watakapotoka Ikulu wameinamisha vichwa chini
najua mnakatabia ka kumuita kumsuta rais Wa hovyo kabisa kutokea Tanzania.... kamati kuu itaitishwa na kutwisha zigo mwizi Wa pembe za ndovu....... azunguke nchi nzima soon
 
Back
Top Bottom