Wassira aipa CHADEMA Ushindi wa 100% Bunda

Wassira aipa CHADEMA Ushindi wa 100% Bunda

Manu.

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2014
Posts
689
Reaction score
180
Akizungumzia mambo mbali mbali katika Ofisi za Gazeti la Mwananchi. Wasira amesema anaweza kumwachia Ester Bulaya kugombea Bunda lakini hatashinda...Kuhusu jimbo lake kuwaniwa na Mbunge wa Viti Maalumu wa CCM, Esther Bulaya,

Wasira alisema, ¡°Sina hofu juu ya mbunge huyo, kwanza siyo saizi yangu. Hata nisipogombea (Esther) hatashinda, namruhusu agombee nina uhakika hawezi kushinda.¡±
Wachambuzi wa siasa wametafsiri kauli hiyo na kuioanisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010, wakati ambapo yeye alishinda.
Mtakeo ambayo bado yanazua maswali mengi.

===================================
Wasira ajipigia mstari mbio za urais
Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira amesema kama chama chake, CCM, kitampa fursa ya kuwania wadhifa wa urais, atasimama kwenye mstari wa uadilifu na ufanisi ili kulinda heshima ya cheo hicho.

Akizungumza na Mwananchi baada ya kupokea tani 7,492 za mbolea kutoka kwa watu wa Japan jana Dar es Salaam, Wasira alisema pamoja na kwamba CCM bado haijapuliza kipenga cha kuwania nafasi hiyo, lakini kikimteua basi ana uhakika wa kuwashinda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). "Nina nguvu kwenye chama changu...mimi ni mwadilifu, sina makundi yoyote. Nina hakika nitakuwa rais bora," alisema.

Wasira, ambaye ni Mbunge wa Bunda alisema wadhifa wa urais hauangalii umri, sura au fedha bali uwezo wa kuongoza na uadilifu.

Alisema umri mkubwa siyo kigezo cha kuwa rais bora, kwani hata rais wa sasa wa Nigeria ana miaka 72. Akifafanua, alisema kama angekuwa na afya dhaifu au kukosa akili timamu, basi hicho kingeweza kuwa kigezo cha kuukosa urais. "Mimi siyo mbunge dhaifu na simhofii yeyote kisiasa. Nina hakika na usafi wangu kiakili, kimwili na uwezo wa kuongoza," alisema.

Katika kujiweka kwenye mstari wa kukubalika, mbunge huyo aliukosoa uchambuzi wa mchambuzi Julius Mtatiro katika gazeti hili uliomtaja kama mmoja wa viongozi wenye kauli za ‘kidikteta'.

Alisema, "Inapotokea nikasema ukweli, basi nisituhumiwe kuwa ni dikteta. Penye ukweli unatajwa ukweli, penye uongo, ukweli huwekwa bayana.

"Mtatiro anadai mimi nimewahi kutoa kauli za vitisho, hilo siyo kweli bali mimi ni msema kweli na huo ndiyo utawala bora."

Kuhusu jimbo lake kuwaniwa na Mbunge wa Viti Maalumu wa CCM, Esther Bulaya, Wasira alisema, "Sina hofu juu ya mbunge huyo, kwanza siyo saizi yangu. Hata nisipogombea (Esther) hatashinda, namruhusu agombee nina uhakika hawezi kushinda."

Chanzo:Mwananchi
 
Mbona hilo lipo wazi hata angegombea yeye, na hii sio Bunda tu majimbo mengi ya CCM mwaka huu wanajua kabisa wanayaachia, tena kiulaini bila hata purukushani.
 
Hawa WEZI WANAMANENO KWELI, hukishinda kiujanja janja lazma umeonye mwenzako kuwa kushinda sio kwa haalali ni mpaka ujanja ujanja ambao inawezekana nyara anajua ulaya hana huo ujanja
 
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Uhusiano na Utaratibu) Steven Wassira na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono (kulia) wakinywa dawa kwa mchungaji Ambilikile​
.
 
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Uhusiano na Utaratibu) Steven Wassira na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono (kulia) wakinywa dawa kwa mchungaji Ambilikile​
.

Hahaha kwani walikuwa wanaumwa?
 
hata agombee yeye ,hatashinda..sokwe hawezi kushinda.....full stop
 
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Uhusiano na Utaratibu) Steven Wassira na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono (kulia) wakinywa dawa kwa mchungaji Ambilikile​
.

Hahaaah!! Sasa Wassira atuambie Loliondo alikwenda kutibu nini kama yeye sio mgonjwa?
Kikombe cha Babu kilikuwa mahususi kwa watu wenye Ukimwi, then Kisukari, Presha na kansa.
 
waziri wa nchi ofisi ya rais (uhusiano na utaratibu) steven wassira na mbunge wa musoma vijijini nimrod mkono (kulia) wakinywa dawa kwa mchungaji ambilikile
.
ngoja nikusaidie
View attachment 250477View attachment 250478 images.jpg images (1).jpg Maige.JPG
 
Wasira anajua kuwa hata 2010 Bunda hakushinda bali udikteta na uchakachuaji ukapelekea kupora ushindi wa CHADEMA.

Kwa mwaka huu Wasira hawezi kufurukuta kwenye kura za maoni mbele ya Ester Bulaya, lakini hata iweje CCM hawatamsimamisha Ester Bulaya maana wasipofanya hivyo watakuwa wamelitoa Jimbo la Bunda bure kwa CHADEMA.
 
Huwezi ukaishi ndani ya shimo la choo ukakosa kuwa na harufu ya kinyesi.
 
Mbali na kuangalia uadilifu,wasira hafai kua rais wa nchi hii maana huo mwonekano wake tu ni balaaa.
 
kuhusu wizi wa Escrow wasira alisema nini?maana hicho ndicho kipimo cha msema ukweli
 
Wasira anajua kuwa hata 2010 Bunda hakushinda bali udikteta na uchakachuaji ukapelekea kupora ushindi wa CHADEMA.

Kwa mwaka huu Wasira hawezi kufurukuta kwenye kura za maoni mbele ya Ester Bulaya, lakini hata iweje CCM hawatamsimamisha Ester Bulaya maana wasipofanya hivyo watakuwa wamelitoa Jimbo la Bunda bure kwa CHADEMA.

Muwacheni rais wetu mpendwa
 
Mpaka leo nashindwa kuamini hawa viongozi walikwenda kwa babu Loliondo.Wanasayansi mulikuwa wapi...Dr. Malecela wa NIMRI..Dr Mshinda wa Ifakara toweni tamko.Kama viongozi wanaamini hiyo kikombe huoni kwamba inawafanya wengine waende mbali zaidi mpaka kwa wenye ALBINISIM. Ewe Mwenyezimungu tuepushe na balaa hilo....AAMIN
 
Wasira ana uadilifu gani? Huyu si ndiye makama kuu ilimtia hatiani kwa kutoa rushwa wakati wa uchaguzi?
Huyu ni mchafu hafai kuwa kiongozi.
 
Back
Top Bottom