Wakati huu kuna mkutano wa maendeleo ya miundo mbinu ktk jiji la dar kati ya mkuu wa mkoa, madiwani, wenyeviti wa mitaa na mainjinia wa jiji.
Vituko vimeanza mara baada ya mkuu wa mkoa kuruhusu mainjinia na wasomi na wasimamizi wa miradi mbali mbali ya jiji, wasomi Hawa wamegeuka wachekeshaji wakubwa kwa kushindwa kwao kujielezea ata kidogo kuhusu kile wanachokifahamu toka ktk miradi wanayoisimamia.
Mkurugenzi mzima wa Tanroads wilaya anasema tatizo la kuaribika kwa barabara ya Mwananyamala hospitali kua pale kuna tatizo sana la mvua, mvua inaharibu ile barabara, injinia mzima anaitwa ajieleze aseme kwanini barabara hazitengenezwi na pesa zinatolewa, anasema eti yeye ni mgeni pale halimashauri, anaulizwa ana muda gani tangia ahamie pale halmashauri anadai ana miaka miwili tu bado mgeni sana.
Sasa boss mzima msomi kabisa na anaongoza dawasco anasema tatizo la wananchi hawafikishi malalamiko yao dawasco kwa njia ya dawasco app. ' tena hatoi ata ufafanuzi app ni kitu gani na je kila mwananchi hapa nchini ana smartphone? Anaulizwa zaidi anasema yes ofcoz ilo tatizo wananchi wanawapigia wrong managers.
Kwa kweli wasomi hawa wako zaidi ya 30 hapa na wanajibu kwa aina moja ya ujibuji wao, na hata hawa tusiwalaumu njoo mitaa na makazini hali ni hii hii.
Tuishie hapa tu, tusije tukatukanwa mengi matusi.