Wasomi wetu acheni Siasa, saidieni Taifa!

Wimana

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Posts
2,449
Reaction score
718
Jana, Profesa Ted Maliyamkono na wasomi wenzake walimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samia Sululu kitabu kinachochambua hoja kuhusu mjadala unaoendela kutokana na Rawsimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Warioba Bungeni.

Nimesikia kuwa Wasomi hao, wanapendekeza ati tubaki na Serikali mbili ikiwa ni njia ya mpito kuelekea serikali moja! Moja ya madai waliyotoa kupinga pendekezo la Serikali tatu ni yale yale 'gharama kubwa' na ati ikiwa tutakuwa na Serikali tatu, Zanziba italemewa kwa kuchangia Serikali ya Muungano maana ina uchumi mdogo! Nimeshangazwa sana, na nimefurahishwa sana na hoja za Mbunge Kafulila ambazo kwa namna zilikwa zinawapa majibu mujarabu hawa wasomi wetu.

Nilitegemea kuwa, kwa mapendekezo ya Rasimu ya pili ya Katiba, Wasomi wetu hawa wangekuja na uchambuzi yakinifu kutusaidia kuhihili gharama za kuwa na Serikali tatu (kulingana na Rasimu) badala ya kusema Zanzibar haitaweza. Wasomi wetu wanasahau kuwa Zanzibar ilikuwa nchi kamili kabla ya Tanganyika kuwepo, na ilikuwa inajitegemea kisiasa na kiuchumi bila msaada kutoka Tanganyika! Usomi gani huo?

Wito wangu ni kuwa, wasomi wetu waache kujiingiza kwenye masuala ya Kiaisasa ambayo kiukweli hatusaidii bali yanaongeza mparanganyiko usio kuwa na faida yoyote kwa Taifa na Watanzania bali kwa kundi la Wananasiasa na kundi la wale wanaofaidika na misimamo hiyo ya wanasiasa.

Wasomi wetu wajikite kuleta mapendekezo ya namna ya kulikwamua Taifa letu katui uchumi tegemezi na umasikini. Ni vema Wasome wetu wajue kuwa mchango wao umekua duni sana kwa nchi hii na wajikite kutupatia majibu ya namna ya kusonga mbele kama walibyosonga mbele wenzetu wa MAshariki ya Mbali- Indonesia, Thailand,Malaysia nk ambao wakati tunapata Uhuru mika ya 1960, uchumi wao (Nchi za Mashariki ya Mbali) ulikuwa sawa na wetu, lakini sasa wamepiga hatua kubwa sana mbele na kutuacha mbali wakati ambapo miaka hiyo tulikuwa sawa bin sawia.
 
hivi Tanzania kuna wasomi? na walianza lini kutumia usomi huo kwa faida njema ya watanzania?
usomi wao mi najua ni kuwadidimiza watafuta kazi,wanachuo na kujikomba kwa washikilia hatamu SISIEM!
 
-Wanachuo serikali 2
-Prof Shivji serikali 2
-Jopo la maprofesa serikali 2
-Kadinari Pengo serikali 2
-Mabaraza ya katiba serikali 2
Sasa kimebaki nini tena? tukubali yaishe.

Ni wasomi wa Tanganyik a hao ndugu yangu, wanasema muungano wa serikali mbili ni wa mpito, hata hawafikiri huu muungano una umri gani mpaka wanadiriki kusema ni mpito. Ndio hawa wamejaa bungeni, serikalini, kwenye maofisi ya umma, jeshini, hawana jipya la kuweza kuikomboa nchi yetu kwenye huu umasikini na utegemezi wa aibu, wao ni kupiga siasa tena zisizo na tija kwa wanyonge wa Taifa hili. Tunapo kwenda...., tutakuja ongozwa na mtu ambaye hata kidato cha kwanza hakijui(somo kwa Uganda na Idd Amin) ili aje kuyaburuta haya masomi uchwara.
 
-Wanachuo serikali 2
-Prof Shivji serikali 2
-Jopo la maprofesa serikali 2
-Kadinari Pengo serikali 2
-Mabaraza ya katiba serikali 2
Sasa kimebaki nini tena? tukubali yaishe.

Tunaomba tuelimishe dhamira ya muungano na faida zake kwa Tanganyika pia na kwa Zanzibar kwa sisi tusio kubaliana na mfumo serikali mbili ndugu yangu wewe!
 
-Wanachuo serikali 2
-Prof Shivji serikali 2
-Jopo la maprofesa serikali 2
-Kadinari Pengo serikali 2
-Mabaraza ya katiba serikali 2
Sasa kimebaki nini tena? tukubali yaishe.

Hujazungumzia mada, umefanya yale yale ya wasomi wetu!

Nakujibu hivyo hivyo. Hao unaowataja walipaswa na bila shaka walienda kutoa maoni yao wakati Tume ya Warioba inakusanya maoni.

Hata hivyo, ktk watu laki 3 waliotoa maoni kuhusu Katiba mpya ni watu elfu 17 tu ndio waliozungumzia muundo wa Muungano, na wengi wao walitaka Muungano wa Serikali Tatu. Hiyo maana yake nini? N
1. Kati ya waliotoa maoni, idadi kubwa ya Watanzania, suala la kuwa na Muungano au kutokuwa na Muungano sio muhimu kwao; Muungano unaweza kuendelea jinsi ulivyo, unaweza kurekebishwa, au hata usipokuwepo!
2. Kati ya watoa maoni elfu 17 waliozungumzia Muungano, asilimia zaidi ya 50 wanataka muundo wa Serikali tatu. Hapo ile hoja kuwa wanaotaka Serikali tatu ni chache inatokea wapi? Ushahidi wa Takwimu uko wapi? Ni vema ieleweke kuwa Warioba aliweka takwimu za wanaotaka Serikali tatu, hao unaowataja wanapata uhalali wapi wa kudai kuwa wanaotaka Serikali tatu ni wachache? Hao unaowataja, Kadinali Pengo, Prof Shivji na wengineo wanaotaka serikali mbili wao ni nani kutusemea Watanzania? Busara ya kawaida kabisa, ikiwa tuna nia ya dhati kuondokana na mivutano ya Muungano, ni kuitisha kura ya maoni pande zote za Muungano kuhusu Muungano-Serikali mbili au moja? Na tuwe tayari kukubaliana na matokeo ya kura ya maoni yaheshimiwe na Watanzania wote.
 
Jana, Profesa Ted Maliyamkono na wasomi wenzake walimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samia Sululu kitabu kinachochambua hoja kuhusu mjadala unaoendela kutokana na Rawsimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Warioba Bungeni.

Nimesikia kuwa Wasomi hao, wanapendekeza ati tubaki na Serikali mbili ikiwa ni njia ya mpito kuelekea serikali moja! Moja ya madai waliyotoa kupinga pendekezo la Serikali tatu ni yale yale 'gharama kubwa' na ati ikiwa tutakuwa na Serikali tatu, Zanziba italemewa kwa kuchangia Serikali ya Muungano maana ina uchumi mdogo! Nimeshangazwa sana, na nimefurahishwa sana na hoja za Mbunge Kafulila ambazo kwa namna zilikwa zinawapa majibu mujarabu hawa wasomi wetu.

Nilitegemea kuwa, kwa mapendekezo ya Rasimu ya pili ya Katiba, Wasomi wetu hawa wangekuja na uchambuzi yakinifu kutusaidia kuhihili gharama za kuwa na Serikali tatu (kulingana na Rasimu) badala ya kusema Zanzibar haitaweza. Wasomi wetu wanasahau kuwa Zanzibar ilikuwa nchi kamili kabla ya Tanganyika kuwepo, na ilikuwa inajitegemea kisiasa na kiuchumi bila msaada kutoka Tanganyika! Usomi gani huo?

Wito wangu ni kuwa, wasomi wetu waache kujiingiza kwenye masuala ya Kiaisasa ambayo kiukweli hatusaidii bali yanaongeza mparanganyiko usio kuwa na faida yoyote kwa Taifa na Watanzania bali kwa kundi la Wananasiasa na kundi la wale wanaofaidika na misimamo hiyo ya wanasiasa.

Wasomi wetu wajikite kuleta mapendekezo ya namna ya kulikwamua Taifa letu katui uchumi tegemezi na umasikini. Ni vema Wasome wetu wajue kuwa mchango wao umekua duni sana kwa nchi hii na wajikite kutupatia majibu ya namna ya kusonga mbele kama walibyosonga mbele wenzetu wa MAshariki ya Mbali- Indonesia, Thailand,Malaysia nk ambao wakati tunapata Uhuru mika ya 1960, uchumi wao (Nchi za Mashariki ya Mbali) ulikuwa sawa na wetu, lakini sasa wamepiga hatua kubwa sana mbele na kutuacha mbali wakati ambapo miaka hiyo tulikuwa sawa bin sawia.

Wasomi wa tanzania wote ni wachumia tumbo, wanategemea wanasiasa hata kwa mambo ya kitaaluma, ivi inakuwaje mtu afanye research halafu mwisho wa siku awasilishe kwa mwanasiasa ili apewe fedha? hauoni ripoti italenga maslahi ya mwanasiasa huyo? tunaweza kusema wasomi pekee ni wajumbe wa kamati ya mabadiriko ya katiba wamejaribu kutumia elimu zao kwa maslahi ya taifa, pongezi kwa jaji warioba na wajumbe wenzake, wasomi wapumbavu wote wanatumia jina la baba wa taifa kiupotoshaji, mfano ni huyu makamu mwenyekiti wa kamati no.10, ni chenga tupu kama usomi ndio huo bora mimi ambae sijasoma kabisa.
 
hao si wasomi bali wasomaji ndo maana wanajikombakomba,ni vitabu vingapi wameandika vya kitaaluma? tafiti ngapi wamefanya? kujaza manila kadi bili kuzifanyia kazi ya kusaidia jamii huo ni ufilisi tu!
 
hivi Tanzania kuna wasomi? na walianza lini kutumia usomi huo kwa faida njema ya watanzania?
usomi wao mi najua ni kuwadidimiza watafuta kazi,wanachuo na kujikomba kwa washikilia hatamu SISIEM!

Inatisha zaidi na, of course, kusikitisha unapoona Profesa kamili anaanza kuwa mbeba mikoba ya akina Bernard Membe! Mimi nimekata tamaa. Tusipobadilisha mitazamo ya kusubiri 'wasomi' ndio watukomboe, basi tusubiri hadi Bwana au Mtume atakaporejea tena.
 
Sikuwa nawaelewa baadhi ya wasomi wenzangu ambao walisusia kabisa kupanda cheo na kuitwa maprofesa licha ya kuwa na machapisho mengi tu ya kuwatosha. Siwezi kuwataja majina kwa ajili ya sera tuliyoijengea hapa jukwani. Lakini kama wewe ni Profesa wa Chuo Kikuu ufananishwe na hawa wanaotumiwa kama karatasi ya msalani- hapana! Kweli hapana. Tena bila aibu kabisa sababu wanazoibua kuhusiana na haja ya kubaki na serikali mbili zinatokana sio na uzuri wa serikali mbili bali kile wanachokiona ubaya wa serikali tatu! Je kuna kisichokuwa na hasi na chanya? Tena bila kusita wanatumia hoja ya JK ya wanajeshi kuchukia na hivyo kuchukua serikali.

Afadhali nibaki mwalimu tu kuliko kuwekwa kapu moja na hawa wajiitao wasomi maprofesa! Shame be upon them!
 
walikua wapi tangu mwanzo,lakini pia wasomi hao hajui kuna nchi ndogo inaitwa commoro?je wana elewana nini?mbona tanganyika ni kubwa lakini ipo hoi kiuchumi madeni kibao
 
Wao kila wakati wanafikiri wanazungumza na wakulima wa Kantalamba tu. Katika hiyo orodha ya Comoro tunaweza kuongeza Sao Tome & Principe, Cape Verde, Seychelles, Mauritius, nk. Haya ni mataifa na dola huru na hawatembezi bakuli kama Tanganyika!!
 
Wasomi mpaka wamefikia kutoa ushauri wa serikali mbili, basi ujue kuwa serikali tatu haiwezekani na ina hasara nyingi kuliko hiyo mbili inayo pendekezwa.

Tuache ubishi kwa kusikiliza mawazo ya vilaza ya kudai serikali tatu bila ya wao kuja na mawazo ya namna ya kuendesha serikali tatu.

Serikali mbili ndio hitaji la Watanzania wengi.
 
Hivi mlikuwa mnadhani kuwa CCM itapenyezaje rasimu yake ya Katiba? Ndiyo hiyo!
 
Inatisha zaidi na, of course, kusikitisha unapoona Profesa kamili anaanza kuwa mbeba mikoba ya akina Bernard Membe! Mimi nimekata tamaa. Tusipobadilisha mitazamo ya kusubiri 'wasomi' ndio watukomboe, basi tusubiri hadi Bwana au Mtume atakaporejea tena.

Ni kweli mkuu mimi sikutegemea mtu kama shivji kuongea pumba kwa maslahi ya chama fulani,

Ila mkuu pale chini nikurekebishe kidogo Bwana Yesu ndiye atakayerejea tena ila mtume sijasoma sehem yoyote kuwa atakujarejea tena @naomba kuwakilisha
 
CCM Bwana yaani wanashindwa kabisa kwenda na wakati. Hivi ni Mtanzania gani anayeweza ku BUY huo UJI.NGA kwamba sera ya CCM ni serikali 2 kuelekea SERIKALI 1? Hata baada ya miaka 50 ya MUUNGANO hakuna hata mwana CCM mmoja anayeongelea serikali 1? You can take a man out of the bush, but you can not take the bush out of him. Hao Professors Pamoja na usomi wao wana fit well kwenye hiyo quotation!
 
waafrica ttuiliowengi elimu haijatukomboa bali imetuletea mgawanyiko tu, hawa wanaitwa wasomi wengine wananchi wa kawaida.
Hii imepelekea hilo kundi la kwanza kujiona miungu watu na kutaka kuliburuza hilo kundi la pili hata katika mambo ambayo hayauhusiano na usomi.
 
-Wanachuo serikali 2
-Prof Shivji serikali 2
-Jopo la maprofesa serikali 2
-Kadinari Pengo serikali 2
-Mabaraza ya katiba serikali 2
Sasa kimebaki nini tena? tukubali yaishe.

Tanzania tuna Wasomi ama Wachumia Tumbo?...Tungekuwa na Wasomi Wangekubali TANESCO ihujumiwe kiasi hiki? Wasomi haweze kukubali eti Rasilimali za Nchi ziwanufaishe WAGENI na kuwatesa wenyeji kiasi cha wengi kupoteza maisha... Hatuna Wasomi Tanzania! Kama yupo Mmoja na Ajitokeze Tumchambue hapa...Wote Wachumia Tumbo tu...
 
Nchi hii ya Tanzania hawa wanaojiita maprofesa ni janga la Taifa.Mwalimu Nyerere,Joseph Warioba kuwataja kwa uchache ni vichwa kweli kweli.Hao wanaoitwa maprofesa wengi ni makuwadi wa sisiemu hawana jipya.Nenda hata kwenye vyuo vikuu wanavyofundisha utajionea vituko vyao wao kazi yao ni kuwasulubu wanachuo wenye mitazamo ya kiuanarakati.Nenda Udom ukajionee mwenyewe hata hapo Udsm.Wapi profesa chachage?wapi profesa Haroub Othman?njooni walau dakika moja tu muwaone maprofesa ambao ni makuwadi wa sisiemu.Msomi yeyote yule wa ukweli,anayechambua mambo kwa uyakinifu hawezi kuwa mtetezi wa sisiemu ambayo inawadhulumu watanzania masikini.
 
Back
Top Bottom