Wasomi wengi kukimbilia CCM

kamtesh

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,395
512
Naona pans tatizo kubwa. Na ndo hao wasomi wanapitisha Kanuni na Sheria za hovyo bungeni. Msomi mzima anajua maana ya Uhuru na Haki, anatia sahihi na kupitisha mambo us hovyo.

Inatuonyesha kwamba tunawasomi wenye njaa sana, hawajali maisha ya watu bali matumbo na familia zao tuu. Hawana uchungu na basic needs za wananchi. Naye anaunga mkono muradi isio na tija kwa wananchi.

Msomi ana nadi flyover za Dar es salaam, wakati jimboni kwake hakuna maji, wala Barbara zinazotumika. Msomi mzima Dr (PhD) holder ana nadi ndege, wakati kwao kuko hovyo. Ndo maana wakipata ubunge, wanaishia mjini Dar es Salaam. Yaani kura apigiwe Sumbawanga au Kasulu makazi Dar es Salaam.

Wasomi wamekua wasaliti wakubwa, wengi wamepewa ukurugenzi kwenye Taasisi za umma, lakini mchango wao ni bure kwa taiga, lakini wapo kichama zaidi. Wapo kwa kufurshisha CCM.

Wasomi wengi VIJANA, wameona AJIRA ni Udiwani, Ubunge wa CCM. Kwa sababu CCM inawalipa vizuri wanasiasa kuliko ukiwa mtumishi Profesa pale Mzumbe, Mlimani au SUA. Its a shame to our nation.
 
Unawaonaje kabudi, bashiru na polepole? Hao ni aina moja ya wasomi wachumia tumbo wa nchi hii, maslahi yao kwanza ya taifa baadaye. Wako tayari kuzitupa elimu zao kule ili wamtumikie mkoloni mweusi.

Lakini mtu kama Lissu ndiye msomi mzalendo wa kweli, yuko tayari kuhatarisha uhai wake na kuhatarisha future ya familia yake kwa ajili ya kupigania anachokiamini.

Anayo kura yangu!
 
Saa nyingine huwa naona Taifa letu ni kama Taifa lililolaaniwa kwa kupata the so called viongozi wahuni, mafisadi, majizi, waongo, waliokosa uzalendo na wasio na uwezo wowote wa kuongoza chochote kile achilia mbali kuongoza Nchi.

Inatuonyesha kwamba tunawasomi wenye njaa sana, hawajali maisha ya watu bali matumbo na familia zao tuu. Hawana uchungu na basic needs za wananchi. Naye anaunga mkono muradi isio na tija kwa wananchi...
 
Hao wasomi wapo CCM kimwili lakini kiakili wapo vyma vya upinzani vinavyo jitambu,kumbuka mtaji wa CCM ni watu masikini sana na wajinga,na wanufaika na mfumo wa MaCCM, mfano Polepole, Bashiru, Kigwangala, NAPE pamoja na vitegemezi vyao.
 
Unawaonaje kabudi, bashiru na polepole? Hao ni aina moja ya wasomi wachumia tumbo wa nchi hii, maslahi yao kwanza ya taifa baadaye. Wako tayari kuzitupa elimu zao kule ili wamtumikie mkoloni mweusi.

Lakini mtu kama Lissu ndiye msomi mzalendo wa kweli, yuko tayari kuhatarisha uhai wake na kuhatarisha future ya familia yake kwa ajili ya kupigania anachokiamini.

Anayo kura yangu!
Hao wasomi wapo CCM kimwili lakini kiakili wapo vyma vya upinzani vinavyo jitambu,kumbuka mtaji wa CCM ni watu masikini sana na wajinga,na wanufaika na mfumo wa MaCCM, mfano Polepole, Bashiru, Kigwangala, NAPE pamoja na vitegemezi vyao.
Mkuuw upo sahihi kabisa
 
Katika mradi ambao siuelewagi ni lile daraja linalopita baharini pale maeneo ya salender, sielewi kwanini tunapoteza pesa kwenye ule mradi wakati tuna vipaumbele muhimu vingi tu
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom