Wasomi wanapokandamizana huku wakimkomoa MZAZI wa ki-Tz

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66
Inatia hofu kweli kwa habari zilizotolewa na vyombo vya habari juma hili toka ktk taasisi ya elimu ya chini na elimu ya juu hapa Tz.

1. Elimu ya chini; Kuna vituo vilivyofungiwa kufanya mitihani ya darasa la saba kwa miaka 3 kwa kosa la kuiba mitihani. swali, je,
wanaoadhibiwa ni wezi au ni wanafunzi watakaofuatia? je, kwanini wazazi na wanafunzi watakaofuata wabebe
makosa yasiyowahusu wakati wahusika wakuu- ambao ni walimu wasichukuliwe hatua? Iweje mtu kuadhibiwa
kwa kosa asilolifanya au lijua?

2. Elimu ya juu; Vivyo hivyo wamesema wanachuo waliofukuzwa wasikubalike ktk vyuo vingine hapa Tz. Je, wao ni akina nani?
Je, wanajua kuwa mgogoro wa vyuo vyetu unajulikana duniani kwa kuwa vyuo havina uongozi mzuri?
Je, ni kwa nini mabuum yanaongezwa kama si kwa wanavyuo kupiga kelele? Walimu wao mara ngapi wamekuwa
wakigoma? Je, unamkomoa nani hapa si mzazi wa Tz? Mkandara leo unayafanya haya lakini jua kuwa
YATAKURUDI TU.

Mimi si mwanafunzi hata sina ndugu ktk hao watoto lakini mi nikiwa m-Tz na mzazi pia naona kuwa waliotoa maamuzi hayo mawili hawana upendo na nchi yetu. Nimekua na kuwaona watu wakifukuzwa shule hapo Tz. Na wengine kuandikiwa ripoti mbaya sana za tabia, lakini leo wao ndio ma-CEO ktk makampuni makubwa ya kidunia baada ya wao kuhama nchi na kwenda kusoma nje, Matokeo yake wale waliowahujumu wakikutana nao au nduguzo huona haya.
 
Back
Top Bottom