WASOMI WA VYUO VIKUU.

WASOMI WA VYUO VIKUU.

Arthurtz

Senior Member
Joined
Feb 10, 2017
Posts
151
Reaction score
121
Tanzania tumejaaliwa na vijana wengi sana ambao ndio chachu ya mendeleo na mabadiliko chanya kwa Taifa letu. Bila kusahau tuna Vyuo Vikuu na Taasisi 64 zinazotoa elimu juu (Kuanzia Certificate, Degree na hadi Masters). Dar es salaam tu kuna Vyuo Vikuu na Taasisi 22 za elimu ya juu hivyo tuna maelfu ya Vijana wenye ujuzi na taaluma za kutatua changamoto za jamii zetu kama wakiwa na ushirikiano na wakipewa nafasi.

Leo hii ningependa tujadili na kuchangua swala moja. Wewe kama Mwana JF, Mwananchi mzalendo, Mpenda maendeleo na Mlipa Kodi wa Taifa, Unadhani ni jambo gani vijana wetu wasomi wa Vyuo Vikuu kwa umoja wao wanatakiwa kuungana na kulifanya ili kuleta Mabadiliko chanya na Maendeleo kwa jamii yetu.
Tafadhali tunaomba uchangia fursa, idea, kero au wazo lolote ambalo ungependa wasomi wetu walifanyie kwa pamoja kwa manufaa ya jamii.

Angalizo, Tungependa lisihusishe Dini au Siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imarisha demokrasia kwanza ili uhuru wa kutoa maoni uheshimike, wapo wasomi wenye weledi mkubwa tu katika kupambanua mambo ila midomo yao imejaa maji, matokeo yake wanakuwa wanafiki kujishikamanisha na Serikali huku mioyo yao inauma, hii ni hatari sana aisee!
 
uber tax founder travis kallanick wakati yupo chuo kikuu mwaka wa kwanza pale university of callifornia hakupoteza muda kukusanya wanachuo kibao.. baada ya kupata idea ya uber tax.... alimshtua mshkaji wake tu mmoja tu.. akaacha chuo akaenda anzisha kampuni..

mark zuckerberg pia alipoanzisha facebook wakati yupo chuo havard akupoteza muda wala hakukusanya wanachuo wengi.. mi yeye tu na rafiki yake mmoja tu.. wakaacha chuo wakaenda ipush facebook yao..

hata google pia surgey brin alimshtua rafiki yake mmoja tu.. wakaenda anzisha google yao.

wewe kama una idea ifanye au mshtue mshkaji wako tu mmoja au wawili mkaifanye...

mambo ya kukusanya wanachuo wote au wahitimu utapoteza muda na mkiwa wengi mnakuwa mnabishana sana

hii jamiiforums ni ya max na rafiki yake mmoja tu mike... sio wanachuo kibao
 
Back
Top Bottom