Mkuu,
Unajua hapa unachanganya kidogo, kwani kuwa msomi haina maana unajua hata kuchagua mke mzuri kuliko yule ambaye hakusoma....Msomi mzuri anachoweza kuchagua ktk chama ni kutazama itikadi, katiba, sera na ilani zake ambazo yeye kama msomi anaweza kuzichambua na kuona mapungufu au mazuri yake.. Msomi hatakiwi kuchagua chama kwa kutazama sura za watu hilo ndio litakuwa kosa la kisomi..
Sasa unapoona wasomi wetu wamechagua CCM, pengine wanaridhika na kukubaliana na vitu hivyo hapo juu kuliko vingine.Pia wanaweza kvutiwa na sura ya mgombea kwani ndivyo tulivyo.. hapa hakuna uhakika wa kisomi kumkamata mtu mapenzi yake.
Na hakika mimi nilitegemea wasomi hawataweza kujiunga na chama au kukipa support kwa sababu huko kuna JK, Malecela, Sharif Hamad, Lipumba, Mrema, Mbatia, Mbowe au Dr.Slaa ila kwa sababu wanaridhika na mrengo wa chama hicho Kisiasa na Kiuchumi..Lakini ajabu ya Mungu, hoja nyingi nazoziona zinahusu mtu au watu fulani kufikia msomi na wasiokuwa wasomi kuchagua chama...
Besides that, Msomi ni binadamu mwenye tamaa pia kama binadamu wengine..Usomi wake hauharamishi Ujinga wa tamaa za kibinadamu ambapo FEDHA hutawala. Tena msomi anaweza kuwa mpumbavu na mwizi mzuri sana kwa sababu ana aminika kwa elimu yake kama alivyosema Nyerere..
Tuelewe tu uwezo huo wa msomi anaweza kuutumia kwa nia njema au mbaya na bado elimu yake ikawa palepale..anayafanya yote kwa makusudi akijua outcome yake..
And U can't take that away from him/her!
Mkuu hizi ndizo siasa za Bongo, ukizielewa wala hazikunyimi usingizi kwani - NDIVYO TULIVYO!