Wasomi wa vyuo vikuu na dhana ya upinzani wa kisiasa

nsami

Senior Member
Jun 11, 2010
175
8
Nianze kwa kumnukuu hayati Baba wa Taifa enzi za uhai wake alipata kusema hivi kuhusu chuo kikuu.

"A university is an institution of higher learning; a place where people's minds are trained for clear thinking, for independent thinking, for analysis, and and for problem solving at the highest level. This is the meaning of a university anywhere in the world"

Kwa tafsiri hiyo ni wazi kuwa jamii inategemea msomi wa chuo kikuu kutoa mchango chanya na kuiunga mkono michango chanya itolewayo na mtu yeyote ktk kusudi la kujenga Taifa. Sio kupinga hoja au kuikubali hoja ktk misingi ya tofauti za kiitikadi za siasa kati mtoa hoja na mchangiaji.

Hivyo basi tunapoona msomi wa chuo kikuu anafanya jambo au anaunga mkono jambo ambalo lina mapungufu makubwa ya kulinganishwa na uwezo wake kulingana na tafsiri ya chuo kikuu, tunapata wasiwasi juu ya hatima ya taifa letu linalokwenda kukabidhiwa kwa wasomi wetu kama viongozi wa kesho!

Tunaposhangaa, sio kama tunashangaa kwamba kwa nini msomi huyo ameshindwa kuwa mpinzani wa kisiasa bali tunashangaa kwa nini ameshindwa kufanya uchambuzi yakinifu na kutoa ushauri wa kujenga na sio kubomoa.

Kila mtu (hata msomi) ana uhuru wa kujoin na chama chochote cha siasa (hata upinzani) kikatiba.

Pia tukumbuke kuwa kila chama ni chama cha upinzani kwa chama kingine labda tuzungumzie upinzani wa serikali na hii haihitaji kuwa mwanachama wa chama kingine, unaweza kuwa ndani ya chama tawala lkn haikuzuii kuwa na mawazo yanayopingana na kauli za serikali labda kama uko ktk Baraza la Mawaziri.

Naomba kuwakilisha.
 
Mkuu,
Unajua hapa unachanganya kidogo, kwani kuwa msomi haina maana unajua hata kuchagua mke mzuri kuliko yule ambaye hakusoma....Msomi mzuri anachoweza kuchagua ktk chama ni kutazama itikadi, katiba, sera na ilani zake ambazo yeye kama msomi anaweza kuzichambua na kuona mapungufu au mazuri yake.. Msomi hatakiwi kuchagua chama kwa kutazama sura za watu hilo ndio litakuwa kosa la kisomi..

Sasa unapoona wasomi wetu wamechagua CCM, pengine wanaridhika na kukubaliana na vitu hivyo hapo juu kuliko vingine.Pia wanaweza kvutiwa na sura ya mgombea kwani ndivyo tulivyo.. hapa hakuna uhakika wa kisomi kumkamata mtu mapenzi yake.

Na hakika mimi nilitegemea wasomi hawataweza kujiunga na chama au kukipa support kwa sababu huko kuna JK, Malecela, Sharif Hamad, Lipumba, Mrema, Mbatia, Mbowe au Dr.Slaa ila kwa sababu wanaridhika na mrengo wa chama hicho Kisiasa na Kiuchumi..Lakini ajabu ya Mungu, hoja nyingi nazoziona zinahusu mtu au watu fulani kufikia msomi na wasiokuwa wasomi kuchagua chama...

Besides that, Msomi ni binadamu mwenye tamaa pia kama binadamu wengine..Usomi wake hauharamishi Ujinga wa tamaa za kibinadamu ambapo FEDHA hutawala. Tena msomi anaweza kuwa mpumbavu na mwizi mzuri sana kwa sababu ana aminika kwa elimu yake kama alivyosema Nyerere..
Tuelewe tu uwezo huo wa msomi anaweza kuutumia kwa nia njema au mbaya na bado elimu yake ikawa palepale..anayafanya yote kwa makusudi akijua outcome yake..
And U can't take that away from him/her!
Mkuu hizi ndizo siasa za Bongo, ukizielewa wala hazikunyimi usingizi kwani - NDIVYO TULIVYO!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom