Wasomi wa Tanzania wabadilike

Dec 23, 2016
31
69
Miongoni mwa kitu kikubwa ambacho wasomi watanzania wamekikosa (hasa Hawa wenye PhD kwenda juu) ni kutokujua kua social networks na technology kwa ujumla zina nafasi kubwa sana kwa wao; kushare elimu yao.

Kuwafikia wanafunzi wengi Tanzania, Africa na duniani kwa ujumla. Kuingiza hela kubwa huenda zaidi hata ya mishahara wanayoipata huko vyuoni na kwenye mashirika na taasisi.

Baadhi wasomi wanahisi kwenda kwenye siasa au kubaki kwenye tasisi walizopo kama vyuoni, kisha kujitutumua na kuwabana wanafunzi wapate GPA ndogo, ndio kutawafanya wajulikane kua wamesoma na wanajua sana.

Dunia ya sasa inahitaji wasomi wanaoijua technolojia na wenye kujichanganya na Jamii.

Wasomi kwasasa ni wengi na wanaongezeka kila siku. Ukisema ujitutumue utabaki na elimu yako kwenye vitabu unavyo andika ambavyopia wanaopenda kusoma ni wachache.

Unaweza kufatilia nchi kama India ambayo imewekeza kwenye technolojia kiasi kwamba walimu wengi wa vyuoni , na vyuo pia vimefungua channels mpaka za YouTube nushare knowledge online na kuwafikia wenye uhitaji wa elimu.

Ushauri wangu kwa Wasomi wa Tanzania
Jichanganyeni kwenye social networks (mf. Kama YouTube) fungueni websites, na mtumie techonolojia nyingne zitakazowafanya muwafikie watu wengi kitaifa na kimataifa.

Wasalam

Kwa Elimu na makala za kijasusi, ulinzi na usalama, uchambuzi wa sheria n.k
 
Tanzania hakuna wasom ndugu ni wababaishaji tuu wamejipa degree za phd na masters hakuna kitu kabisa msimamishe mbele za watu uone
 
Back
Top Bottom