blessings
JF-Expert Member
- Jul 9, 2012
- 7,418
- 7,077
Ni ukweli usiopingika kuwa PhD (ya kusomea, si ya kupewa) ndio shahada ya juu kabisa katika mfululizo wa elimu hapa duniani. Tena ukiipata unaheshimika na dunia ina matarajio makubwa sana kwako kwa kuzalisha maarifa, tafiti na huduma kwa jamii (inayokuzunguka na duniani kwa ujumla) inashangaza Afrika na hususani Tanzania wasomi hapa "hulilia" kuteuliwa katika nafasi za utendaji (kimsingi huitaji kuwa na PhD kupitia mafaili/kusaini ya watumishi) kwa vyeo vya wakuu wa wilaya, mkoa, kamishna, mkurugenzi, naibu/ katibu mkuu. Hili tusi kwa wasomi na wanetu/wadogo zetu kuonyesha kuwa hakuna thamani ya kuwa msomi kama utafanya kazi za watu wa kawaida. Narudia tena kazi za PhD holder si katika utendaji (kusaini barua) bali ni kufundisha, kufanya tafiti na huduma za kitaalam kwa jamii. Siasa na utendaji si kazi za hadhi yenu.
** Mawaziri & Manaibu (PhD) - 11
*** Makatibu Wakuu & Manaibu - 21
** Mawaziri & Manaibu (PhD) - 11
*** Makatibu Wakuu & Manaibu - 21