Wasomi/viongozi wetu wa sasa hawana uzalendo

Chelamoche

Member
Jun 20, 2012
7
0
Nasikitika sana kwa wasomi wetu wa Tanzania kukosa Uzalendo nikiwa kama mlipa kodi kwa kila mwezi.Mimi nafikiri mfumo wetu wa elimu kwa sasa hivi sio mzuri kwani serikali haiwajibiki kwa wananchi wake kuwapatia elimu ya bure kama ilivyokuwa zamani.Nakumbuka wakati nasoma tangu usafiri wa kwenda shule za bweni tulilipiwa na serikali,si hivyo tu tuliokuwa vyuo vya ufundi tulipewa pesa ya sabuni kila mwisho wa mwezi iliyojulikana kama kichele.Lakini baada ya kumaliza chuo JKT tulijifunza jinsi ya uwajibikaji na kutimiza malengo yako utakapoanza kazi.Lakini baada ya kumaliza JKT kwa mujibu wa sheria serikali iliwajibika kukupangia kituo cha kufanyia kazi.Sasa hivi mambo si hivyo wasomi na viongozi wetu wana shule zao na hospitali zao pamoja na familia zao ni lini Msomi na kiongozi wa Tanzania ataupata uchungu kutoka shule za kata na hospitali zetu?
 
Back
Top Bottom