Wasomi uchwara wa leo vyuo vikuu na umoja wa ufa

Wasomi uchwara wa leo vyuo vikuu na umoja wa ufa

Joined
Aug 7, 2013
Posts
12
Reaction score
11
"TUMEPANGA KUZUNGUKA NCHI NZIMA KUSHAWISHI WATANZANIA KUMUUNGA MKONO MAKAMBA IWAPO ATAAFIKI KUWANIA NASAFI HIYO YA URAIS KWENYE UCHAGUZI MKUU UJAO". Binafsi nilishituka sana nilipoisoma hii habari kwenye gazeti la Mwanachi la tarehe 19 augosti.

Ninachojua mimi hata msomi wa sayansi yoyote anajua maana ya Historia. Labda niwakumbushe tu. Historia ni kujifunza mambo yaliyopita, yaliyopo ili tujue tunakoelekea. Sasa nduguzangunyi inaonekana tunasoma historia halafu tunabaki huko huko tutokako hatujui tulipo leo wala tuendako, ni sawa na mikataba ya akina chief mangungo kupewa bunduki kwa vipande vya almasi na mikataba ya leo ya kupewa net ya sh. 2,000/= kwa kugawa ardhi kwa wazungu walewale yenye urani, chuma, gesi na madini mengine. Hapa wasomi uchwara mnawadhalilisha wasomi walio elimika.

Ninachotaka kuwaambia akina Theonest Theophil na wenye akili kama za kwake wanaojiita wasomi wa vyuo vikuu 21 wa Tanzania, hii ninayoandika hapa sio siasa bali ni U-Tanzania halisi, turudi kwenye historia ya mwaka 2000 wakati Jakaya anagombea, ni wasomi wa vyuo vikuu hawahawa kwa kuongozwa na Ridhiwani ndio waliotushawishi kumchagua Kikwete na yanayoendelea leo tunayaona tunauzwa kwa kutumia vyandarua vya mbu na vidola vichache vya MCC. Mengine sitaki kuyazungumza wale wazalendo wa kweli wasije pandisha hasira zao.

Ndugu wasomi wa leo hasa wale wenye njaa ya leoleo tu, tunachotakiwa kujadili leo ni suala la KATIBA mpya ndio majibu ya kila kitu. Baada ya kupata katiba mpya yenye tija kwa watanzania, narudia tena; Yenye tija kwa watanzania, ndipo tuangalie nani atafaa kuiongoza Tanzania kwa mujibu wa mkataba mpya tuliouweka baina ya viongozi na waongozwa. Tuache dhana ya kuwa na watawala na watawaliwa, nadhani tulitakiwa tuwe tumesahau toka enzi ya ukoloni. Ndugu wasomi wa vyuo vikuu wa leo msitupotoshe tujadili katiba, kama mnafikiri kwamba wanasiasa wameuteka mjadala wa katiba basi ninyi jitahidini kuujadili kulingana na matakwa ya watanzania kama TAHLISO kila mnapokutana, zungukeni nchi nzima kuwashawishi watanzania kuwa ni katiba ya namna gani itawasaidia sio kupita njia ya mkato ya 'eti kwakuwa viongozi wanaendekeza malumbano visasi na uadui kwa hiyo njia rahisi ya kupita ni kushawishi watanzania kumchagua Makamba. Kwanza mnawatia aibu walimu wanu waliowafundisha toka shule ya msingi kuwa waliwafundisha MAANA (DEFINITION) bila kuwafafanulia muendelezo wa maana hizo, hata hivyo msomi mzuri anatakiwa kuelimika si kutafuniwa kila kitu huwezi kuwa mtafiti mzuri. Lakini Nampongeza Donat Salla kama mtendaji mkuu wa TAHLISO baada ya kutoa majibu mazuri kwamba TAHLISO kazi yake ni kusimamia elimu, utafiti na machapisho ya kazi za kitaaluma, kuteua wagombea ni kazi ya vyama vya siasa.

Ndugu zangu ninachotaka kuwaambia hapa ni kwamba hivi sasa TUJADILI KATIBA MPYA na sio nani anafaa kugombea, TUTAMJUA MGOMBEA BAADA YA KATIBA MPYA KUTUNGWA na atakayeweza kuisimamia sio sasa msiturudishe nyuma. Kwanza wanasiasa kujadili katiba sio dhambi ila tuwaunge mkono wale wanaojadili katiba kwa maslahi ya watanzania na tuwakatae wale wanaojadili kwa maslahi yao binafsi. Hata kama Mpendwa wetu Hayati Mwalimu Nyerere angefufuka leo hii hawezi tena kuwa rais kwa katiba hii ya sasa.

Mwisho nasisitiza tena kwa wale wasomi wenye njaa kama Theonest Theophil njaa yenu ya siku moja haitawasaidia, jaribuni kuamka na kuelimika, tuangalie historia. HUU NI WAKATI WAKUJADILI KATIBA MPYA NA SI NANI ANAFAA KUWA RAIS 2015. TUTAMJADILI BAADAYE MTU ATAKAYEFAA KUWA RAIS KWA MUJIBU WA KATIBA YETU TUTAKAYEITENGENEZA.

Mngoni wa Kusini.
 
Back
Top Bottom