A teller
JF-Expert Member
- Feb 6, 2018
- 531
- 724
Hebu vuta picha, namna ulivyosota kuipata hiyo degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama wafagiaji wa jiji ukiwa shule ya msingi. Umepiga jaramba maili kadhaa kuifata shule. Umekumbana na kashkashi za walimu ``wanoko``, ukiwona tu bandama zinacheza ``ndombolo`` na tumbo linaunguruma kama jenereta la kiwanda.
Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage kama segerea , wadudu ni wengi kuliko maharage ! Hukukata tama ulivumilia kwa kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itamulika.
Ukupigao ndio ukufunzao , pale ulipochaguliwa chuo! Masikini akipata…Boom lote liliyeyuka kwenye nguo! Ulitaka na wewe ufanane na`` watoto wa jiji``.! Ulihudhuria disco zaidi kuliko Lecturer . Flat screen, `dance floor` vikahamia chumbani kwako! Supplementary zikakukosa kosa , tia maji Mungu si Athumani ukamaliza chuo na gamba lako !
Wazazi wakawa na matumaini sana, ndio muda wa kula`` pensheni``, maana msomi umeshavaa joho ! umerudi na rundo la makaratasi tu kama gari la magazeti.! Yote hayo ukawaambia wazazi yanaitwa ``madesa`` na uliyasoma sana kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na `vizenga`(vibomu) , ulijulikana kama mzee wa ``kujilipua``.
Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na vifijo. Haikupita wiki zile `Bata` za chuo ukaanza kuzimiss, daah! Ulifulia hasa hata kifurushi uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani!
Uliowaacha ambao hawakuendelea na masomo , wapo mtaani ,baadhi wamepauka kama kopa la mtwara , wengine wanan`gaa kama kikalio cho stova – wamewekeza kwenye biashara zao! Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuu! Umeshikwa na haya , sura imekushuka kama viraka vya nyongeza vilivyoisaliti suruali!
Kila kazi unayoomba, unaambulia usaili tu! Nyingine hata usaili hupati hata hutii pua! Kazi moja mnaitwa alfu tano! Khaa! Ulidhani mlisoma `survival for the fittest` ili mfaulu mtihani tu? Ndiyo uko maabara sasa. Unazikumbuka pesa ulizotumia kula `bata` chuoni , lol, leo`bata` unakuwa wewe!
Umeanza `kuisoma namba`! umepauka kama koti la mtunguo Tandika Mungu si Athumani ,ukabahatika ajira mpya huko kwetu `nanjilinji`` Mshahara laki 3, huna jinsi inabidi tu uende ! miaka mitatu sasa imepita huna tofauti na uliowakuta hapo `kijijini`. Zile ndoto na hekaya za chuoniza kuwa na kazi ya 1.5 , ununue gari, ujenge nyumba, uwe na ``demu`` mkali , zoote zimeyeyuka kama samli kikaangoni ! magari unayaona mjini tu , mademu wakali unaendelea tu kuwaita `shemeji! ndio hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anayechagua wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia mchuzi! Sasa umekuwa mzee wa Kaunda suti za kupauka kama inzi wa chooni . Gucci unaziona kwenye filamu tu , wewe ni magauni ya chirimeni tu!
Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata mshahara ! mwanzoni ulikuwa unaona taabu kukaa kijijini , kila weekend uko mjini, unajifanya alwatani ``Vasco da Gama`` baada ya shida kukutandika vibao, sasa huna jeuri ya kupanda gari kila wiki !! Hivi si ulisema ukializa chuona kupata kazi utaunga kusoma masters? Vipi kwani vyuo vimefungwa?
Haya niyo maisha ya vijana wengi ! hudhani mtaani kuna maziwa na asali wakishamaliza degree zao ! mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo degree ! kuna wakati degree inabidi uiweke pembeni ili ufunike kombe ``mwanaharamu`` apite! lakini pia mtaa utakupokea kama ulivyojiandaa! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na kuhifadhi kidogo basi mtaani utaziona fursa za kuwekeza hicho kidogo ulichonacho. Kama ulikula bata tu na mtaani umerudi na mawigi, kucha feki na ``modo`` za kuvaa mlegezo basi mtaa hautakuonea aibu, utakupa swaga zake .
Nguo ya ijumaa, hufuliwa Alhamisi.
Nimeona nifanye kushare na nyie.