UNDENIABLE
JF-Expert Member
- Feb 26, 2013
- 2,326
- 1,315
Salaam,
Kwanza natanguliza samahani kwa wale wadada!
Jana nilikuwa eneo la tabata kimanga, dsm bar ya freeland nawaza na kuwazua juu ya mwenendo wa maisha yangu ya kila siku huku nikikumbuka maneno ya Mrembo by Nature kuhusu mitandao na wanaume wa mipango, nadhani naeleweka hapa!
Pembeni yangu wamekaa wadada warembo(wanaonekana ni wadada wenye fahamu zao(exposure)), wanapiga story za hapa na pale, story nyingi zinahusu wanaume/mapenzi na kidogo hali ya maisha! Story za mapenzi zinaonesha kuwa wamechoshwa na mapenzi kwa ujumla, wanalalamika kuwa wanaume sio waaminifu na pia wanawake wamekuwa wakijirahisisha sana kitu kinachopelekea dharau kubwa kutoka kwa wanaume, kwa lugha ya kibiashara wanasema wanaume wanakuwa na choice kubwa kushinda wanawake!
Katika story zao mmoja wao akasema namnukuu ila sio rasmi sana
"ngoja niwaambieni kitu kimoja unajua wahenga walisema akili ni nywele kila mtu ana zake, sasa mwenzangu nywele za waafrika ni ngumu hivyohivyo na akili zao ni ngumu, tazama wahindi, tazama wazungu wao nywele zao laini sisi wenyewe tunahangaika kulainisha nywele ili tuwe na nywele laini, laiti tungeweza kulainisha na akili zetu pia labda tungekuwa na akili laini na tungepata unafuu wa haya mapenzi na maisha kwa ujumla" mwisho wa kunukuu!
Samahani:
Huenda mmoja ama wote wa wale wadada ni wanaJF ama wanapitiagapitiaga nyuzi za hapa JF km guests, kama ndio naomba kuomba samahani kwa huu uzi, bila shaka haujawaharibia credibility yenu!
Ahsante sana!

Last edited by a moderator: