Phlagiey
JF-Expert Member
- Oct 26, 2013
- 3,500
- 1,688
..::Kazi kweli kweli::..
Niliwahi kusikia huu msemo sehemu fulani basi nikajua kila sehemu utakuwa na maana na ukiutumia utakufumbua macho na kukuonesha kilicho mbele yangu.
Kuna wakati nakumbuka uliwahi kunisaidi sana msemo huu baada ya kuingiwa wasiwasi kwenye issue fulani hivi ambayo jamaa walipanga kuniuzia mzingo kumbe ule mzigo ulikuwa fake. Hapa wasiwasi ukawa umeniokoa.
Toka hapo nikaupa huu msemo imani hasa nikikumbuka matukio ya nyuma.
kwa vile tayari nilikuwa imeshaujengea imani basi nikaugeuzia katika mahusiano yangu, ilikuwa ikitokea tukikorofishana na mpenzi wangu basi naanza kupata wasiwasi na kuhisi kwamba wenda amepeta jamaa huku ndiyo maana ananizengua, haikuishia hapo mara nyingine nilikuwa nikipiga simu nikaambiwa inatumika kama mara mbili tatu basi wasiwasi huo nahisi kunajamaa atakuwa anaongeanae mbona simu iko bize muda mrefu!.
Kumbe sikujua kwamba kunamisemo mingine haistahili kutumiki kwenye mapenzi na ukiiendekeza matumizi yake unahatarisha mahusiano na junge fikra mbaya zitakazo pelekea kuvunjika kwa mahusiano kutokana mitazamo inayoletwa na wasiwasi.
Ikafikia wakati wa kujitafakari ni kipi hasa mbona haya mapenzi yamekuwa mwiba tofauti na zamani, kumbe nilichokua nakosea ni kili nilicho kiwekea imani ndiyo ilikuwa sumu ya mapenzi, baada ya kulijua hilo amani ikarejea ndani ya mahusiano yetu nikawa siishi tena kwa wasiwasi.
Ujumbe wangu kwako
Sio kila ukisikiacho kinafaa kujaribiwa katika mahusiano ya mapenzi.
Mapenzi ni hisia hazipaswi kuchezewa.
Jaribu kuichunguza mitazamo unayoingia nayo katika mahusiona.