DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amesema wagombea wakiwamo wabunge wanaomaliza muda wao watakaochukua fomu Julai 2, 2025 na kuzirudisha, baada ya vikao vya chama hicho, watatazamwa na kupendekezwa wagombea wanaokubalika na wananchi
Amesema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuvunja bunge Juni 27, mwaka huu, kazi iliyobaki kwa chama hicho, itakuwa ni kuendesha taratibu za kupata wagombea na kusisitiza haitakata mtu bali itateua.
Wasira ameyasema hayo leo, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza, wakati akihitimisha ziara yake katika mkoa huo.
Amesema wagombee ni wengi lakini watachuja na wala hawatakata mtu bali watateuwa: "Kukata ni kwa hasira, ukiteua unatazama uwezo kwa wakati. Kwa hiyo CCM hatukati mtu, ila tunateua wagombea wachache kati ya wanachama wengi.
"Maana tunawanachama wengi, hivyo watakaobaki watasubiri uchaguzi ujao maana vijana wako wengi," amesema Wasira.