GE2025 Wasira: Mchagueni Samia. Yuko tayari kutumia juhudi binafsi kuleta maendeleo

GE2025 Wasira: Mchagueni Samia. Yuko tayari kutumia juhudi binafsi kuleta maendeleo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira miongoni mwa sababu za Watanzania kymchagua Mgombea urai wa CCM Dk. Samia Suluhu Hassan ni pamoja na uwezo wake kutumia juhudi binafsi kuleta maendeleo ya Watanzania.

Aidha, kupitia CCM chini ya Dk. Samia, Watanzania wataendelwa kuwa salama huku fursa za uchumi zikiendelea kufunguka kupitia sekta mbalimbali ukiwemo uwekezaji.

Aliyaeleza hayo alipozungumza na wana CCM katika mji wa Vwawa, wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe alipokuwa akimtafutia kura Dk. Samia na wagombea ubunge na udiwani waliosimamishwa na Chama kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.

"Tukiwaambia Watanzania tuchagueni la kwanza tutawathibitishia umoja wa Watanzania utalindwa la pili tutawahakikishia amani ya Tanzania inalindwa na tatu maendeleo ya Tanzania yanapatikana. Mambo matatu; umoja.amani na maendeleo ya kudumu maendeleo ya watu ndio ajenda zetu kuu.

"Kwa hiyo tukija hapa ni mwaka wa uchaguzi, tunapokuja tunawaambia Watanzania tuchagueni hatuwaambii watuchague kwa kubabaisha, tunawaambia tuchagueni kwa sababu sisi ni Chama kinachoahidi na kutekeleza, ndiyo sifa yetu. CCM ni Chama kinachoahidi na kutekeleza na hatujazuia vyama vingine," alieleza.

Alisema CCM inatambua kuwa wananchi wanataka mambo muhimu zikiwemo huduma bora za kijamii pamoja na uchumi imara.

"Jumuiya ya watu wanataka uchumi, uchumi pamoja na kuwa na chakula cha kutosha, uchumi ni pamoja na kuwa na nyumba nzuri unaishi, uchumi ni pamoja na watoto watapata mahali pakusoma, ukiugua unapata hospitali na unaweza kuwa na uwezo wa kiuchumi na ukanunua nguo zako, angalau mambo matano ambayo yanakufanya uishi maisha mazuri.

wasiera.png
 
Back
Top Bottom