Wasira Hajui majukumu yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasira Hajui majukumu yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mndeme, Jul 4, 2011.

 1. m

  mndeme JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida, leo imethibitika kuwa Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu hajui majukumu yake kwa sababu kwa mujibu wa Tangazo la Serikali analotoa Rais baada ya kuunda serikali Wasira anatakiwa kuratibu: Mosi mahusiano ya serikali na dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia, Pili usalama wa taifa, na Tatu Tume ya Mipango.

  Alichokifanya leo akiwasilisha hotuba ya bajeti ya ofisi yake, amegusia kwa undani suala la dira ya taifa ya 2025 na mpango wa maendeleo wa miaka mitano ambao umewasilishwa hivi juzi na kwa ujumla hotuba yake imerudia hotuba karibia yote ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano aliyotoa juz juz bungeni.

  Tofauti na hayo Msemaji wa Kambi ya upinzani Israel Natse aligusia mambo yote hayo kwa mujibu wa instrument ya majukumu ya mawazir.

  Hii inaonesha semina elekezi za Rais kwa wateule wake hazijazaa matunda walikuwa wanakula posho tu.

  Kazi ipo.
   
 2. Bless the 12

  Bless the 12 Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe aise, mie ni mmoja wa watu waliokuwa wanafatilia hiyo hotuba yake. Kwa kweli inatia aibu ufinyu uliokuwepo kwenye hiyo hotuba. Nadhan ile ya upinzani imegusia mambo muhimu zaidi na coverage yake imekuwa bora kuliko ya Wasira.

  Wamekula posho tu hao, bado tuna kazi!
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  huyu mzee wasira ni ovyo sana..........gongo inamuharibu sana huyu
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani uwepo wa Wizara hii ya Mh. Wasira ni makosa ya kimsingi mno kwenye mfumo wa utawala wetu na mgawanyo wa madaraka (fundementally wrong). Kwa mfano:
  1. Usalama wa taifa - Kwa hiyo Othman ana-report kwa Wasira? Wizara ya mambo ya ndani inafanya nini?
  2. Tume ya Mipango - hii imejikita zaidi kwenye economic issue na sio mahusiano ya jamii ambayo Wasira anaonekana kusimamia.
  3. Mahusiano ya serikali na dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia - Tanzania tuna tatizo kubwa kuhitaji a full-fledged Ministry kusimamia haya mambo? Kwa nchi inayoomba msaada hata wa vi-boat vya doria tunapata faida gani kwa kugharamia Wizara nzima kwa kazi ambayo ingefanya na 'Department' ndani ya wizara fulani i.e Social welfare?

  Nilishangaa sana kumuona Mh Wassira akisoma Mpango wa Maendeleo Bungeni wa miaka mitano maana nilitegemea Waziri wa Fedha awe ndio mhusika mkubwa kwenye hili. Nashawishika kusema ndani ya cabinet kuna muingiliano wa kazi na hii sio tu itazidisha kuzorota kwa utendaji (maana kila mtu atasema fulani ndio anahusika) bali pia litaleta manung'uniko baina ya wizara. Bad managment style.
   
 5. mgaza2001

  mgaza2001 Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 96
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15


  FJM nakuunga mkono,hivi yeye mwenyewe haoni aibu kazi ni kulala tuu bungeni akichangia ndo anarudia rudia yale yale ya nyuma. WE NEED TO CHANGE THEM, NOT THEM TO CHANGE US.
   
Loading...