PreGE2025 Wasira: CCM itateua wagombea ubunge, sio kuwakata

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,234
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitakuwa na utaratibu wa kuwakata wagombea bali kitateua wale wanaofaa kwa mujibu wa vigezo na taratibu za chama.

Akizungumza Juni 24, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Zamani, Wasira amewahutubia wanachama wa CCM kutoka majimbo mawili ya uchaguzi ya Sengerema na Buchosa, ambapo amesisitiza tofauti kati ya maneno "kukata" na "kuteua".

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ameeleza kuwa CCM itaendelea kutumia vikao halali vya chama kufanya maamuzi ya kuteua wagombea wake kwa kuzingatia sifa, maadili, na uhalali wa kisiasa, bila kuendeshwa na hisia au makundi.

Kauli hiyo imekuja wakati ambapo maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2025 yanaendelea kushika kasi, huku wanachama wengi wakiwa na matarajio ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Ti

Tofauti yake nini? Ukizifata sana siasa za bongo utaumia kichwa. Shika dini ukifa ukaishi maisha ya neema
 
Ancestor hata akiongea la maana watanzania hawaliamini. It is against nature for the fossils to advise the living things.
 
Back
Top Bottom