PreGE2025 Wasira: CCM inakuja na ilani yake ya uchaguzi mkuu , ambayo itakuwa na majawabu ya changamoto mbalimbali za vijana

PreGE2025 Wasira: CCM inakuja na ilani yake ya uchaguzi mkuu , ambayo itakuwa na majawabu ya changamoto mbalimbali za vijana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Chama Cha Mapinduzi CCM kimesema ilani yake ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, itakuwa na majawabu ya changamoto mbalimbali za vijana ikiwemo namna ya kutatua changamoto ya ajira.

Hayo yameelezwa leo Machi 22, 2025 na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kemondo, Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuimarisha uhai wa Chama.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesema kuwa Chama kinafahamu changamoto ambazo vijana wanakumbana nazo na kwamba Ilani ijayo ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, itakuja na majibu ya shida zao.
 
CCM wameshindwa kutatua changamoto za maadui wetu wa tangu tunapata uhuru zaidi ya kuongeza maadui wengine kama uchawa, ufisadi na uongo, leo hii wanawezaje kutoona aibu ya kuwadanganya Watanzania kuwa ilani yao ya 2025 - 2030 inaenda tatua changamoto!!!
 
Kila siku za wikiiii ni miki miki ( juma nature)
Shairi la ( mpaka lini?) 1961- 2030 ahadi tuuuuu! Mpaka lini?
Hawa wanao chagua ccm ni akina nani haswa???
 
Imeshindikana kutoa majawabu kwa miaka yote ccm imetawala,ndio wake watoe leo. No reforms no election
 
Back
Top Bottom