Wasira amtaka RPC Arusha awaombe radhi wanahabari

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Umma), Stephen Wasira, amemtaka Kamanda wa Polisi Polisi mkoani Arusha,Thobias Andengenye, kuwaomba radhi waandishi wa habari waliopigwa na polisi na kuharibiwa mali zao wakati wa maandamano ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Wasira alitoa kauli hiyo juzi jijini hapa wakati wa kikao cha pamoja cha maaskofu, watumishi wa Jiji la Arusha, wakuu wa wilaya, polisi na maafisa Usalama wa Taifa.

Alilazimika kusema hayo kufuatia mwandishi wa Abood Media Kanda ya Kaskazini, Fortunatus Ruta, kutaka kujua msimamo wa serikali kuhusu kitendo cha Polisi kuwakamata na kuwasweka ndani waandishi waliokuwa katika kazi zao siku ya tukio hilo ambapo pia vifaa vyao vya kazi viliharibiwa.

Alisema "vita havina macho, lakini kitendo hicho si kizuri hivyo RPC unatakiwa kukaa na waandishi wa habari kumaliza tatizo la kuharibiwa mali zao kwa kuomba radhi," alisema.

Kuhusu kuharibiwa mali zao na madai ya waandishi hao, alisema kama kuna madai, basi yapelekwe kwa Chama cha Waandishi wa Habari Arusha ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo na kumuonya Kamanda Andegenye ahakikishe tatizo hilo halijitokezi tena.

Akifanya majumuisho ya mazungumzo na Baraza la Maaskofu juu ya sakata la mauaji ya watu watatu na uchaguzi wa Meya, Wasira alisisitiza kuwa tatizo la kanuni humalizwa kwa kanuni na uchaguzi wa meya utatatuliwa kwa kanuni.

Hata hivyo, baada ya kikao hicho, hakuna kiongozi wa dini aliyekuwa tayari kufuta kauli yao ya kutoutambua uchaguzi wa meya na Meya aliyechaguliwa, Gaudence Lyimo.

Wakati hali ikiwa hivyo kuhusu sakata la waandishi wa habari kutaka kusitisha ushirikiano na Jeshi la Polisi kwa muda usiojulikana, muda uliotolewa na Klabu ya Waandishi wa Habari Arusha (APC) wa siku saba kumtaka Kamanda Andegenye kuomba radhi, uliisha juzi na hajafanya hivyo.

Waandishi waliokamatwa na kuharibiwa vifaa vya kazi ni Mussa Juma na Thomas Mashalla (Mwananchi) na Moses Kilinga ambaye ni Katibu Msaidizi wa APC.

Naye Mwenyekiti wa APC, Claud Gwandu, alisema baada ya kuona muda waliotoa kama chama umeisha bila RPC kufanya chochote, viongozi wa chama hicho wanatarajia kukutana na kulizungumza kwa upana ili kujua hatua zaidi za kuchukua.
CHANZO: NIPASHE
 
Haisaidii kwani ni tabia iliyojengeka kuwa mwandishi sichochote nisawa na migapicha wa mtaani!hata yeye alishampiga mwandishi aliyekuwa katika kazi yake na hakuomba msamaha kwenye jamii ya waandishi!
 
Waombwe radhi na walipwe vyombo vyao vilivyoharibiwa,at least that will make sense....
 
HV kwa siku thread zinatakiwa ziwe ngapi?kwa mtu mmoja!pia kufikisha 100 siwezi kaka ni ngumu sana may be 10

labda niwe natafuta umaarufu au ubunge!!!but am happy to be here sababu napata inforamations na kujua jinsi ya kujenga hoja kiukweli najifunza mengi sana kwa wana jf
 
Haisaidii kwani ni tabia iliyojengeka kuwa mwandishi sichochote nisawa na migapicha wa mtaani!hata yeye alishampiga mwandishi aliyekuwa katika kazi yake na hakuomba msamaha kwenye jamii ya waandishi!
Yaah naikumbuka ile!sijui ni hasira au madaraka!hawa viongozi hata sijui kama huwa wanaangalia reference za matukio yao ya nyuma hapo tena unawezakuta RPC akagoma kuomba radhi!pili anaetakiwa kuomba radhi ni IGP au RPC?maana RPA alitoa kibali na IGP akatoa tamko la kuahirisha maandamano kwa mdomo!
 
Waobwe radhi waandishi tu!Wengine kichapo ni halali yao,hata kama wamekufa au wamepata vilema!
 
Back
Top Bottom