Wasipoifuta kuna hatari kwa Preventive Detention Act kutumika dhidi ya viongozi hawa wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasipoifuta kuna hatari kwa Preventive Detention Act kutumika dhidi ya viongozi hawa wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 10, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wadau:

  Kila mara huwa najiuliza: Kwa nini ile sheria ya kuwaweka watu kizuizini bila ya kufunguliwa mashitaka (Preventive Detention Act) bado ipo hadi leo hii?

  Hiyo sheria kandamizi haijaondolewa na tangu ujio wa siasa za vyama vingi haijawahi kutumiwa na kiongozi yoyote wa nchi. Kwa maneno mengine sheria hiyo ipo kisheria lakini siyo halali.

  Hivi hawa viongozi wa serikali ya CCM wa sasa hivi hawaoni umuhimu wa kuiondoa? Hawaoni kwamba inaweza kuwarudia wao wenyewe.

  Nasema hivi kwa sababu hatujui Mwenyezi Mungu ameipangia Tanzania yetu hii kitu gani – katika miaka ijayo huwezi kujua katupangia nini.

  Siombei machafuko, lakini kwa madudu viongozi wa CCM wanayowafanyia Watanzania, wanaweza kujikuta wametupwa nje ya uongozi-kama ilivyotokea katika nchi nyingi tu Barani humu, na sikioni kitu chochote kinachoweza kuniridhisha kuwa nchi hii ni ya kipekee yaani unique.

  Madudu yanayofanywa na viongozi wetu ni yaleyale waliyokuwa wakiyafanya hao wengine kwa wananchi wao na kujikuta wako nje.

  Sasa wapinzani wakishika nchi wanaweza kupata urahisi mkubwa wa kuwashughulikia mafisadi hawa wa CCM walioko katika uongozi sasa kwa sababu sheria hiyo haitahitaji ushahidi thabiti wa ufisadi hao. Serikali mpya inaweza kuwasweka ndani wakaozea huko, na ikawa haijavunja sheria wala Katiba.

  Ikitokea hivyo, hivi wafuasi wa CCM (yaani wapinzani) kweli watapata nguvu ya kuilalamikia serikali hiyo mpya?

  CCM lazima itumie akili. Kuna kila dalili sheria hii inaweza kuwarudia wao.

  Nawasilisha.   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu Zak, kwa nini unawaamsha awalio lala? hasa kama ni mafisadi? We acha tu wabanwe na sheria yao wenyewe, na hapo ndipo patakuwa patamu!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hakika upo uwezekano mkubwa sana wa hilo kutokea.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa CCM wanajiamini sana! Hawajui la kesho. Wimbo wao huu 'Amani na utulivu" unaanza kuwa kichekesho kutokana na madudu wanayofanya. After all amani haiimbwi kwenye majukwaa, bali hujengwa kwa misingi madhubuti ya haki.
   
 5. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  wanajiamini kwa uchakachuaji na technology ya kichina!
   
 6. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ayaaaa mbona unawashitua wewe? Huoni unaharibu ukichukulia kuwa hiyo sheria haijatumika muda mrefu?!
   
 7. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  hawajashtuka tu?
   
 8. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/2-1985.pdf

  Hapo utapata amendment yake ya 1985. Naona wanaruhusu ku-challenge detention order in court. Na mahakama za sasa ivi haziwezi kuruhusu detention orders zisizokuwa na evidence.
  Tatizo hapa ni evidence. The crime committed by the mafisadi ni ngumu ku-pin down kwa mtu mmoja. Sio sawa na wizi wa kuku. Watu wametengeneza shell companies, nk kujificha nyuma yake. Hizi kesi zitakuwa ndefu. Sio rahisi kama mnavyodhani.
   
 9. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Zak kwa historia yote ilipo dunia mwisho wa sheria mbovu uishia kwa waliyoitunga, huo ndio ukweli na unachokisema ndiyo historia ya udhalimu maana wanaotunga sheria mbovu ujishau wakidhani kuwa wao watakuwa madarakani milele, bila kujuwa kuwa siku wakitoka hiyo hiyo sheria mbovu itawachapa.   
 10. nyamemba

  nyamemba JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2015
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 689
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Huwezi kujiapiza kuwa nikikatwa patachimbika, wewe nani? Ngoja ukome nyau wewe.
   
 11. Sibonike

  Sibonike JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2015
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 10,286
  Likes Received: 4,992
  Trophy Points: 280
  Nasubiri kujua hilo shimo lina ukubwa gani? Au ni dogo kuliko analochimba nyau akijisaidia?
   
 12. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2015
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,337
  Likes Received: 8,452
  Trophy Points: 280
  mbona unajiuliza mwenyewe na kujijibu mwenyewe.hizi "matipo" ID hizi shida kweli.
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2015
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Mkuu ulianzisha thread na kuanza kujijibu mwenyewe..
   
 14. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2015
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,337
  Likes Received: 8,452
  Trophy Points: 280
  nandiko lake lina mantiki,ila imeonyesha kwamba hata ile ID iliyo muuliza swali ktk post ya kwanza,anaimiliki ni yeye mwenyewe mleta mada.LMAO.
   
Loading...