kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,685
WASIOOA – WALIOACHIKA - KUFA MAPEMA.
Utafiti mpya wa masuala ya uhusiano umebainisha kuwa watu wenye umri kati ya miaka 35 na 40, ambao hawajaoa au kuolewa wapo kwenye hatari ya kufa mapema tofauti na waliooa au kuolewa.
Matokeo ya utafiti huo, uliofanywa hivi karibuni na wataalamu wa masuala ya uhusiano ukiongozwa Dk. Ilene Siegler wa Idara ya Sayansi ya Tabia kutoka Chuo Kikuu kilichopo Kaskazini mwa Jimbo la Carolina nchini Marekani, umebainisha pia kwamba NDOA NI KINGA INAYOMWONGEZEA BINADAMU MUDA WA KUISHI.
Aidha, watafiti hao wamebainisha kwamba wanawake waliopewa talaka au kufiwa na wenza katika umri wa kati wapo kwenye hatari ya kufa mapema zaidi.
Watafiti hao wameeleza kuwa watu ambao maishani hawajawahi kuoa au kuolewa wapo kwenye hatari ya kufa mapema mara tatu zaidi ya wale waliokuwa katika ndoa imara katika maisha yao, hasa wakiwa kwenye umri wa kati.
Matokeo hayo ambayo yalichapishwa kwenye jarida la Annals journal la Marekani na kuandikwa kwenye mtandao wa Daily Mail, ulihusisha watu 4,802, wakiwamo watu waliozaliwa miaka 40 iliyopita.
Ulibaini kuwa kati ya watu wazima wenye umri kama huo wengi wao walikufa wakiwa na miaka 50, kutokana na kuishi peke yao.
Kwa kutumia dodoso na maswali ya moja kwa moja walibaini kuwa pamoja na mtu aliyekuwa kwenye ndoa kuishi kwenye maisha hatarishi kwa kunywa pombe kupita kiasi na kuvuta sigara, bado walio kwenye ndoa wana nafasi ya kuishi muda mrefu zaidi kwa asilimia 2.3.
Dk. Ilene Siegler, anasema kuwa maisha ya kwenye ndoa ni kinga inayofanya wanandoa waishi kwa muda mrefu.
"Inaonyesha kuwa na mke au mume ni kunga ya maisha hasa katika umri wa kati, hali hii ikiwaathiri zaidi wanaume kuliko wanawake," amesema Siegler.
Alisema kuwa utafiti huo umewawezesha kubaini kuwa kati ya vifo 238 vilivyotokana na athari za kutokuoa au kuolewa, wanaume ndiyo waliothirika zaidi na kwamba kati yao wanawake walikuwa ni 32 tu.
Alifafanua kuwa wanaume wameathirika zaidi kutokana na kutokuwa karibu na familia, hivyo kufanya mambo tofauti na mwanamke, ambao hata kama hajaolewa anaweza kuwa karibu na familia na kupata ushauri wa baadhi ya mambo, ingawa hali hiyo haimfanyi kuwa salama, anasema Siegler.
Dk. Siegler alitolea mfano utafiti uliofanywa hivi karibuni na nchi saba za Ulaya, akieleza kwamba utafiti huo umeonyesha kuwa mtu aliye kwenye NDOA HUWA NA FURAHA KIMWILI, KIAKILI NA KIAFYA na humfanya awe na marafiki wazuri, pia hutata ulinzi kwa kuwa wanandoa wana kawaida ya kujilinda wenyewe.
"Kwa mujibu wa utafiti huo wa Sweden ni kwamba wanawake waliopewa talaka au kufiwa na mwenza kwenye umri wa kati wapo kwenye hatari ya kufa mapema mara tatu zaidi," anabainisha Siegler.
Matokeo haya ya utafiti yanaungwa mkono na Dk. Rebena Sima wa Idara ya Saikolojia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akieleza kuwa kwa kawaida binadamu yeyote ni lazima awe kwenye uhusiano.
Anasema kwamba kama binadamu hayupo kwenye uhusiano ni lazima atakuwa na upungufu Fulani, ambao kibinadamu ni maradhi, ikiwamo msongo wa mawazo na mengine yanayofanana na hayo.
"Hata iweje, wanandoa wanakuwa wanaaminiana kiasi cha kupeana ushauri. Sasa kwa kuwa mpweke ni lazima mhusika atakosa mtu wa kushauriana naye jambo linalosababisha kusononeka nap engine hata kuongea peke yake, kitu ambacho ni hatari zaidi," anaeleza Dk. Sima akiongeza:
"MPENZI anaweza kuwa wa siku moja au mbili au zaidi, lakini uaminifu kati ya MKE au MUME ni kitu kingine, hivyo walio kwenye uhusiano wa namna hiyo huwa kwenye hatari zaidi kwa kuwa huongeza msongo wa mawazo kutokana na kutokuwa na uaminifu kati wahusika."
Alifafanua kuwa kwa tamaduni za kiafrika mtu ambaye hajao au kuolewa hawezi kutoa ushauri au kuchangia lolote kama walio kwenye ndoa, hivyo mhusika hujitenga mwenyewe kwa kuhisi anadharauliwa jambo litakalomfanya awe mpweke na kufanya mambo ya kukurupuka.
Naye Modesta Kmonga ambaye ni mtaalamu wa masuala ya saikolojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma alisema kuwa binadamu akishakuwa mtu mzima anakuwa na uamuzi binafsi kwa mambo yake na kwamba akiwa na mwenza, mara nyingi hukumbushwa yaliyo mema na kukatazwa mabaya hali ambayo kwa asilimia kubwa husaidia kumfanya mhusika kuwa alikatazwa na mwenza wake.
"Hata kama wanagombana kwa kiasi gani ni lazima kuna baadhi ya mambo wanashauriana, hasa kwenye matatizo ya kifamilia na kwenye masuala ya msingi kwa mfano matatizo kazini, ugonjwa na mambo kama hayo. Hivyo kuna muda ni lazima kwa mtu mzima kuwa na mwenza wake karibu, hii humsaidia sana kupata faraja na kuongeza siku za kuishi," amesema Kimonga.
Anasema kuwa kuishi bila mwenza ni hatari zaidi na ndiyo sababu watu wanaoishi hivyo hufa mapema kutokana na kuwa kwenye hatari ya maambukizi ya maradhi hasa ya zinaa na Ukimwi kwa vile huwa huru kujihusisha kwenye uhusiano usio salama.
Gabriel pia aliwashauri wanaume na wanawake wafuate taratibu, ikiwemo kupima afya kabla ya kuoa au kuolewa mapema ili waweze kuongeza siku za kuishi.
…….., itaendelee; Source by; Mwananchi.
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]
WAKATI taifa likikabiliwa na ongezeko la vifo vinavyotokana na maradhi, ajali na hata baadhi ya watu kujiua, wataalamu na wanasayansi nchini wametaja mbinu mbalimbali ambazo binadamu akizifuata, anaweza kuishi zaidi ya miaka 100. Wataalamu hao, kutoka vitengo mbalimbali vya Sayansi ya Jamii na Viumbe hapa nchini, wamesema mtu akiishi bila kuathirika akili na mwili, anaweza kuishi maisha marefu zaidi kuliko yule anayeathirika katika vitu hivyo. Wasomi hao wamebainisha kuwa mgawanyo wa mwili, akili na roho, ni mambo muhimu katika mwili wa mwanadamu yaliyo na uwiano unaoingiliana na havitenganishiki.
Kukabili msongo wa mawazo
Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Mtaalamu wa Saikolojia na Mkuu wa Kitengo cha Sosholojia wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Joyce Nyoni aliitaja mbinu ya kwanza ya kuongeza maisha kuwa ni kukabiliana na msongo wa mawazo. Daktari huyo alisema akili ya mtu huweza kuathiri mwili. Wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na maradhi yanayotokana na msongo wa mawazo, kama vile maradhi ya moyo au vidonda vya tumbo. "Wengi wetu tuna msongo wa mawazo, jambo dogo linaweza kumfanya mtu akashindwa hata kula au kulala, ni lazima tujifunze kukubaliana na hali halisi ya maisha, huku tukiamini kuwa, hakuna jambo lisilo na utatuzi," alisema Dk Nyoni.
Alisema wapo wanawake wengine ambao hupoteza maisha kwa sababu ya waume zao kuwatesa au kuwatelekeza. "Ni lazima tufahamu kuwa maisha hata siku moja hayawezi kunyooka, ni lazima viwepo vikwazo vya hapa na pale, kwa hiyo hatuna budi kujifunza kuzikabili changamoto za maisha," alisema. Utafiti uliwahi kufanyika na kuonyesha kuwa, wanawake chini ya miaka 50 na walio katika kipindi cha kufunga hedhi, (menopause) ambao hawawezi kukabiliana na msongo wa mawazo, wanaugua maradhi ya moyo. Alisema yeye kama mtaalamu wa masuala ya saikolojia, huwashauri watu kutulia na kukubaliana na matokeo yoyote katika maisha.
Kuishi mfumo chanya, kucheka
Jambo lingine ambalo mtaalamu huyu alishauri ni kuishi katika mfumo chanya. Alisema watu wengi hawatosheki na kile kidogo wanachopata, badala yake wanaishi kwa kulalama jambo ambalo kwa asilimia kubwa, huchangia maradhi ya moyo. "Mara kwa mara huwa nawaeleza wanafunzi wangu, ukimwona mwanamke kavaa mikufu, bangili na hereni nyingi masikioni, vyote vya dhahabu, huyo ni mgonjwa, kwa sababu ukimnyang'anya au akiibiwa ujue ataugua," alisema Dk Nyoni. Alisema, ni vyema watu waishi kwa kuridhika na chochote wapatacho, badala ya kutoridhika na hali yao na kutamani maisha ya wengine.
"Namthamini mwanamke anayetoka nyumbani, amechana nywele zake kawaida, amepaka mafuta, lakini anajiamini, kuliko yule ambaye anataka atazamike kuwa ni wa thamani na mwenye fedha, mbele za watu, kwa kuvaa nguo za thamani kubwa au kuendesha magari ya kifahari," alisema .Mtaalamu huyo alitaja mbinu nyingine ya kurefusha maisha kuwa ni kucheka au kuwa na furaha
Mazoezi, usingizi wa kutosha
Naye Dk Nandera Mhando, wa Kitengo cha Sosholojia na Athropolojia cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema hakuna ubishi kuwa zipo tabia ambazo husababisha baadhi ya watu kukumbwa na maradhi na kufa katika umri mdogo. "Wapo ambao hawana kabisa tabia za kufanya mazoezi, hawa huwa na uzito mkubwa na miili yao inapokuwa na mafuta mengi, maradhi ya moyo huwa yamepata nyumba, lakini pia kutopata usingizi wa kutosha nalo ni tatizo," alisema.
Tabia ya mtu, vyakula
Dk Mhando alisema, tabia ya mtu ni sababu nyingine inayoweza kumfanya mtu awe na maisha mafupi, kwa mfano, kupenda kufanya ngono, kuvuta sigara, na ulevi ni mambo yanayosababisha maradhi na kuleta kifo.
"Kama mtu tayari ameathirika, halafu anandelea kufanya ngono kwa kiasi kikubwa, si ajabu mtu huyo kufa mapema, lakini wanaokunywa pombe na kuvuta sigara kwa wingi, nao mara nyingi huugua maradhi ya figo, mapafu, ini nk.," alisema. Daktari huyu aliongeza kwamba, aina za vyakula tunavyokula nayo vinachangia kupima afya ambayo kimsingi ni kipimo cha maisha ya binadamu.
Alisema wanaokula vyakula asilia, kama mboga za majani, kunywa maji na kula matunda kwa wingi, si rahisi kushambuliwa na maradhi, tofauti na wanaokula wanga peke yake ambao wanakuwa katika hatari ya kupata maradhi, hatimaye kifo. Imethibitishwa kuwa, Mwanabaolojia mmoja, wa nchini Marekani, Ancel Keys, hata baada ya kustaafu, aliendelea kufanya kazi za bustani nyumbani kwake kwa kiasi kikubwa jambo lililomfanya kuishi miaka 100. Alifariki mwaka 2004.
Dini
Mtaalamu wa Sosholojia ya Dini kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Thomas Mwendaluka, alisema, dini ni moja ya maeneo ambayo huweza kuchangia mtu kuishi maisha marefu.
"Dini ina pande mbili, hasi na chanya, kwa sababu kwa upande mmoja inatoa tumaini. Inamsaidia mtu kiimani kuishi maisha marefu na vilevile ni chanzo cha kufupisha maisha," alisema Mwendaluka. Alisema, watu huweza kujengwa kiroho na kuamini uponyaji wa magonjwa yaliyoshindikana. Kwa mfano tangu UKIMWI ulipoingia , waathirika wengi wamekimbilia katika taasisi za dini na kule hujengwa kiroho na kiimani na kujisikia wamepona na kuongeza siku za kuishi. "Lakini baadhi ya imani, kwa mfano Boko Haram, zinawataka waumini wajitoe muhanga kuua, hilo hufupisha maisha ya wengi," alisema Mwendaluka. David Larson, Mshauri wa Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili wa nchini Marekani, alifanya utafiti wake mpana juu ya uhusiano wa moja kwa moja uliopo kati ya dini na afya.
Uchunguzi wake ulionyesha wazi kwamba upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya muumini aliyejitoa kwa moyo katika imani husika na afya yake. Alishangaa kubaini kwamba, wale wanaohudhuria kanisani wanaishi muda mrefu kuliko wale wasiohudhuria. "Nilishangazwa kujua kuwa kutumainia uweza wa Mungu ndio msingi wa ustawi wa kweli na maisha ya afya yenye furaha," alisema Larson.
Kunywa maji mengi
Daktari wa Kitengo cha Patholojia katika Hospitali ya Muhimbili, Innocent Mosha anasema maji ni jambo lingine linaloweza kukupa afya na kukuepusha na maradhi. "Kazi ya maji ni kusafisha ini na figo, kwa hiyo si ajabu mtu asiyekunywa maji ya kutosha akawa na afya mbaya kwa sababu uchafu hubaki katika damu," alisema Dk Mosha. Matabibu wengi wanashauri kuachana na aina za vyakula kwa mfano, nyama ya wanyama yenye mafuta ya majimaji (saturated fat) na mafuta mazito (cholesterol), ambavyo huongeza hatari ya kupata shinikizo la damu, kupooza
(stroke), ugonjwa wa moyo, kansa, unene usio wa kawaida, kisukari na magonjwa mengineyo. Mwandishi wa kitabu cha ‘The Blue Zones' Dan Buettner, ambaye alifanya utafiti kuhusu siri ya ya kuishi maisha marefu katika nchi za Bara la Australia, Greece na China, aligundua kuwa, watu wa nchi hizo wana tabia za kufanana ambazo bila shaka huwafanya waishi maisha marefu. Alisema wote hula milo yenye kiasi kidogo cha nyama na wanafanya mazoezi. Mwisho…
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

…….
Mtaalamu huyo aliendelea kutoa ushahidi wa tafiti mbalimbali alizoziona akisema kuwa utafiti kutoka Sweden unaonyesha kuwa wakati ndoa humlinda mhusika dhidi ya maradhi ya Alzheimers, wanaishi na MPENZI wakiwa kwenye umri wa kati wapo kwenye hatari ya kupata matatizo ya akili."Kwa mujibu wa utafiti huo wa Sweden ni kwamba wanawake waliopewa talaka au kufiwa na mwenza kwenye umri wa kati wapo kwenye hatari ya kufa mapema mara tatu zaidi," anabainisha Siegler.
Matokeo haya ya utafiti yanaungwa mkono na Dk. Rebena Sima wa Idara ya Saikolojia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, akieleza kuwa kwa kawaida binadamu yeyote ni lazima awe kwenye uhusiano.
Anasema kwamba kama binadamu hayupo kwenye uhusiano ni lazima atakuwa na upungufu Fulani, ambao kibinadamu ni maradhi, ikiwamo msongo wa mawazo na mengine yanayofanana na hayo.
"Hata iweje, wanandoa wanakuwa wanaaminiana kiasi cha kupeana ushauri. Sasa kwa kuwa mpweke ni lazima mhusika atakosa mtu wa kushauriana naye jambo linalosababisha kusononeka nap engine hata kuongea peke yake, kitu ambacho ni hatari zaidi," anaeleza Dk. Sima akiongeza:
"MPENZI anaweza kuwa wa siku moja au mbili au zaidi, lakini uaminifu kati ya MKE au MUME ni kitu kingine, hivyo walio kwenye uhusiano wa namna hiyo huwa kwenye hatari zaidi kwa kuwa huongeza msongo wa mawazo kutokana na kutokuwa na uaminifu kati wahusika."
Alifafanua kuwa kwa tamaduni za kiafrika mtu ambaye hajao au kuolewa hawezi kutoa ushauri au kuchangia lolote kama walio kwenye ndoa, hivyo mhusika hujitenga mwenyewe kwa kuhisi anadharauliwa jambo litakalomfanya awe mpweke na kufanya mambo ya kukurupuka.
Naye Modesta Kmonga ambaye ni mtaalamu wa masuala ya saikolojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma alisema kuwa binadamu akishakuwa mtu mzima anakuwa na uamuzi binafsi kwa mambo yake na kwamba akiwa na mwenza, mara nyingi hukumbushwa yaliyo mema na kukatazwa mabaya hali ambayo kwa asilimia kubwa husaidia kumfanya mhusika kuwa alikatazwa na mwenza wake.
"Hata kama wanagombana kwa kiasi gani ni lazima kuna baadhi ya mambo wanashauriana, hasa kwenye matatizo ya kifamilia na kwenye masuala ya msingi kwa mfano matatizo kazini, ugonjwa na mambo kama hayo. Hivyo kuna muda ni lazima kwa mtu mzima kuwa na mwenza wake karibu, hii humsaidia sana kupata faraja na kuongeza siku za kuishi," amesema Kimonga.
Anasema kuwa kuishi bila mwenza ni hatari zaidi na ndiyo sababu watu wanaoishi hivyo hufa mapema kutokana na kuwa kwenye hatari ya maambukizi ya maradhi hasa ya zinaa na Ukimwi kwa vile huwa huru kujihusisha kwenye uhusiano usio salama.
…………………………………………………………………
Gabriel amesema kuwa dokta huyo alimshauri kuoa ambapo yeye mwenyewe alikuwa hataki kwa kuwa watoto wake ni wadogo akihofia watapata taabu kuelewana na mama wa kambo, lakini alizidi kumshauri hadi akafikia uamuzi wa kuooa mwanamke ambaye alikuwa ni mpenzi wake baada ya kuambiwa kuwa hata kuwa wapenzi mnaokaa mbalimabali ni tatizo pia kwani kunakuwa hakuna uaminifu.Godius Kahyarara ambaye ni mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kitengo cha Sayansi ya Uchumi alisema kuwa kuishi bila kuwa na ndoa kunamfanya mhusika kuweza kujiingiza kwenye hatari yeye mwenyewe bila kujua, huku akiamini yupo huru kufanya chochote na wakati mwingine kuwashangaa waliiooa kwa kuwaona wamejifunga."Kitu kingine ambacho ni hatari zaidi watu ambao hukaa peke yao iwe wanawake au wanaume hula vyakula visivyo rasmi, hawana muda wa kupumzika na hata uamuzi wao huwa wa kukurupuka na huo niyo ugonjwa mbaya zaidi kwani huwasababisha kuwa na afya dhaifu wakiishi maisha hayo kwa muda mrefu' afya ambayo ni rahisi kupata maradhi ya kuambukiza kama vile kifua kikuu, magonjwa ya zinaa ikiwemo Ukimwi," alisema Kahyarara.Akitoa ushuhuda wake Juma Amrani, ambaye aliwahi kuwa na mke waliyeishi kwa miaka mitatu na kuachana alisema kuwa:Baada ya kuachana na mke wake huyo hata maisha yake yamebadilika kutokana na kuwa na uamuzi usio sahihi ikiwemo kuuza nyumba walioukuwa wakiishi maeneo ya Boko nje kodogo ya jiji la Dar es Salaam na sasa anaishi nyumba ya kupanga huku akikabiliwa na wakati mgumu wa kutokutanamani kurudi nyumbani mapema."Niko kwenye mipango ya kutafuta mke wa kuoa licha ya kuwa hapo awali niliapa sitafanya hivyo kutokana na vitendo visivyo vya kistaarabu alivyonionyesha mke wangu niliyeachana naye kwa kuwa naona kabisa sipo sawa," alisema Amrani. Naye Faidha Abdul ambaye ni mama wa watoto watatu ambao alizaa bila kuolewa kutokana na kushindwanan na wanaume aliozaa nao, amesema kuwa anapata wakati mgumu sana hasa kwa watoto wa kike kutokana na matendo yao kuonekana yeye anachangia kwa kuwa nay eye hana mume.Alisema kitu hicho kinamkera sana na hutamani angeolewa hata na mwanamume mwingine, achilia mbali baba wa watoto hao, ili aweze kuwa angalau na stara."Watoto wa kike wamekuwa sasa kwani wameshamaliza elimu ya Sekondari, kibaya zaidi hawanisikii na walianza uhuni siku nyingi jambo linalonifanya nikosane na kaka yao, akiamini ninafurahia, huku majiarani wakinishutumu kuwa wamefuata tabia yangu ya uhuni kwa kuwa naishi bila mume. Hali hii inaninyima raha," alilalamika Faidha. Kwa upande wake Silvanus Gabriel alisema kuwa alipofiwa na mkewe nusura apoteze maisha kutokana na kukumbwa na maradhi mfululizo ikiwemo kupooza.Alisema kuwa tatizo lilianza kwa kupungua uzito bila mpangilio ghafla, baadaye alipata ugonjwa wa kiharusi uliosababisha mkono na mguu wa kushoto kuishiwa nguvu."Nilipokuwa kwenye mazoezi Muhimbili nikakutana na daktari ambaye nilimfahamu kwa jina moja tu la Dk. Thomas, ambapo katika maongezi ya kawaida alitaka kujua chanzo cha maradhi yangu! Nikamwambia sikuwa na tatizo zaidi ya kupungua uzito ambapo nilikuwa na kilo zaidi ya 80 nikafika kwenye 45 kwa muda mchache ambapo sikuwa na maradhi yoyote hata homa," alisema.Aliongeza: Akaniuliza tena sikuwahi kupata tatizo siku za nyuma? Nikamwambia hakuna zaidi ya kufiwa na mke wangu mwaka mmoja uliopita. Cha kushangaza! dokta alicheka na kuniambia hilo ndiyo tatizo.
………………………..
Gabriel pia aliwashauri wanaume na wanawake wafuate taratibu, ikiwemo kupima afya kabla ya kuoa au kuolewa mapema ili waweze kuongeza siku za kuishi.
…….., itaendelee; Source by; Mwananchi.
"LINGANISHA NA HII, HAPO CHINI (by Mwananchi) na Jadili"
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 48"]
[TR]
[TD="width: 98%, bgcolor: transparent"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TR]
[TD="width: 98%, bgcolor: transparent"]
Mbinu za kuishi zaidi ya miaka 100 zagunduliwa