Wasiooa Njia Panda

Wasiooa Njia Panda

African Believer

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
436
Reaction score
428
Habari wana Jf

Natumai mu wazima wa afya.

Uzi wangu unahusiana na changamoto tunayokabiliana nayo sisi tusiooa bado.

Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kasumba ya wake za watu kuwakana waume zao pindi wanapo tongozwa na wanaume wapya.

Inatokea umemuelewa mtoto wa kike unamtupia sound yeye anasema poa tu. Unamuuliza juu ya mahusiano yake yeye anasema hana mtu, cha ajabu mkishaanza mambo fulani ndipo changamoto huibuka na baadaye kuja kugundua umeingizwa chaka, na unaetoka nae ni mke wa mtu. Wakati mzee mzima ulitaka kutia nanga.

Jamani kinadada mlioolewa tufungieni vioo basi na sisi tupate nyumba zetu toka kwa masela wenzetu.
 
Ila wake za watu inaonekana mna matatizo kweli maana kila siku kuna threads zinazowahusu

Badilikeni basi
Wanaanzaje kubadika sasa kwani na wao hawapendi utamu?
Mbona waume zao na wenyewe hawajabadilika wapo vilevile kama bado hawajaoa?
Hebu waacheni wake za watu na wao wafaidi utamu wa ladha na mapishi tofauti ya ndizi.

Maendeleo hayana chama
 
Wanaanzaje kubadika sasa kwani na wao hawapendi utamu?
Mbona waume zao na wenyewe hawajabadilika wapo vilevile kama bado hawajaoa?
Hebu waacheni wake za watu na wao wafaidi utamu wa ladha na mapishi tofauti ya ndizi.

Maendeleo hayana chama
Hahahah
Kwa iyo wanashindana..mwaga mboga nimwage ugali
 
Hahahah
Kwa iyo wanashindana..mwaga mboga nimwage ugali
Kama kawaida sasa hivi kila mtu anapenda kubadilisha ladha, tatizo hua ni uthubutu tu kama mume ameweza na anafurahia utamu tofauti kwa nini na mke nae asifurahie banaaaaaa

Maendeleo hayana chama
 
Vyuoni wapo wengi tu,kwa nini uangaike na wake za watu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom