Wasikieni Simba eti Yondani kafungisha

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,445
Lawama ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya Tusker, imemuangukia beki huyo ambaye anashutumiwa kuwa ni kawaida yake.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza tayari kumekuwa na kikao kilichowakutanisha viongozi kuwajadili wachezaji kadhaa wenye mwelekeo wa ‘kuiumiza’ Simba na Yondani ameonekana ana makosa mengi zaidi.

Mmoja wa viongozi walioingia katika mkutano huo uliofanyika siku mbili baada ya Simba kulala kwa Yanga. Amesema Yondani hatadumu katika klabu hiyo.

“Sipendi kutajwa gazetini, lakini hili utaliona tu. Unajua imekuwa ni kawaida, kila unapofika mchezo wa Yanga kuna wachezaji ambao lazima wabembelezwe kuwa wawe makini wasitufungishe.

“Lakini kama hiyo haitoshi hao hao ndiyo wamekuwa wakitufungisha, angalia Yondani mechi hii amefanya uzembe, mpira ulikuwa wake. Kaenda kucheza rafu makusudi halafu kajiangusha. Hata hakuamka badala yake alikuwa anamuangalia Ngassa anaenda kufunga huku akisingizia misuli.

“Kama una kumbukumbu alifanya hivyo mechi nyingine dhidi ya Yanga kumauchia Baraza apige krosi. Sisi tunaelewa tatizo ni nini na hata kocha pia ameliona hilo, ile si hali ya kawaida,” alisema kiongozi huyo akionyesha kukerwa na namna alivyofanya Yondani.
Dakika za mwisho kabisa za muda wa nyongeza wa dakika 30, Yondani alienda kurukia mpira uliokuwa unaonekana hauna madhara yoyote dhidi ya Ngassa.

Ajabu alitaka kumrukia Ngassa ambaye alimkwepa na kuchukua mpira kasi, wakati anaondoka, Yondani alianguka na kulala kabisa. Ngassa alitoa krosi safi kwa Shamte Ally aliyeimaliza Simba akafunga kirahisi

Tunawasubili Mapinduzi Cup sijui nako mtakuja na lawama gani.
 
Ndio tatizo la mipira ya kibongo kama walimuona ni mtu wa kufanya makosa kila wakati walimpanga wa nini?? Kila Simba au Yanga akimfunga mwenzie lazima lawama zipelekwe kwa wachezaji kuwa walihujumu timu. Acheni hizo mambo ya kizamani hayo. Muacheni Yondani acheze mpira msitake kutafuta visingizio,mpira ni kushinda, kufungwa au kutoka sare!!! Yananiboa kishenzi...
 
Simba hawana mpya, mara wamlaumu refa na tena leo Yondani, hakuna mpya kwa mnyama, Yanga inatisha bana
 
Kwani Simba kafungwa!Mbona nilisikia tambo zao eti kundi la Yanga lilikuwa nyanya,sasa naamini hiyo nyanya ndio imekuwa chachandu ya kutafunia nyama za simba na paka.Jamani tamu,hivi sasa nina bonge la pande la paka mkononi natarajia kumpelekea mchawi mmoja anayeitwa masofasofa nae akatafune.Kwa ugumu wa kundi la simba ndio maana wote wamepigwa 2-1 na Yanga tena goli la ushindi ni dakika za mwishoooni
 
simba wakubali yaishe na wajipange kwa michezo ijayo, kufungwa na yanga isiwachanganye
 
mnyama bana anachekesha sana, badala ya kuilaumu yanga kwa kuifunga
wao wanambana yondani!
 
Siku ya kufa mbwa pua zote zinaziba....
Yondani, kaseja, mgosi na wengine pua zao ziliziba
 
mpira wetu bongo unapelekwa na kamati za ufundi watu wameenda kuangalizia wamegundua kuwa jamaa kafungisha. na nimesikia mganga wao pia wamemtimua.nyie simba acheni mipira ya miaka ya 47 kabumbu halipigwi hivyo wazee.
 
Back
Top Bottom