Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,924
- 30,272
WASIFU WA JULIUS NYERERE:
USAJILI WA TANU, VIZINGITI VYA SERIKALI, KUSAKA WANACHAMA NA SAFARI YA UNO 1955
Naendelea kusoma kitabu cha pili cha maisha ya Mwalimu Nyerere.
Historia ya TANU na wazalendo wake wote waliopigania uhuru wa Tanganyika ni ‘’one epic story,’’ ikiwa itaelezwa kwa ukweli wake.
Ikiwa mwandishi kwa hofu tu ya kuandika baadhi ya mambo mfano kueleza wale waliokuwa na Nyerere mstari wa mbele kutoka siku ya kwanza katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika na akaogopa kuandika ukweli atakuwa mchuzi wa historia ya TANU kautia maji na maji yale yataondoa ladha ya viungo vyote ndani ya upishi ule.
Jambo hili litamuathiri mpishi mwenyewe na ladha ya mchuzi wenyewe.
Nimejishtukia niko katika maisha ya Mwalimu Nyerere TANU ishaundwa na kusajiliwa, kadi zishatengenezwa, keshakwenda UNO na kurudi chama kinaendelea.
Hakuna taarifa vipi TANU iliundwa na vipi ilisajikiwa.
Hapa pamerashiwa.
Ngoma imeondolewa juani.
Ladha ya historia ya TANU inapotea.
Tuanze na siku Nyerere amekwenda kusajili TANU.
Abdul Sykes, mdogo wake Ally na Nyerere walikubaliana kuwa Rais wa TANU Julius Kambarage Nyerere aende kukisajili chama kwa Msajili wa Vyama akitoka huko wakutane Mtaa wa Kipata nyumbani kwa Ally Sykes ili kupeana taarifa.
Nyumba hii ya Kipata ina historia ndefu katika harakati za kupigania haki za Waafrika.
Kuanzia mwaka wa 1929 hadi 1942 haya ndiyo yalikuwa makazi ya Kleist Sykes, katibu muasisi wa African Association.
Mzee Kleist alikuwa akifanya mikutano mingi ya African Association pale nyumbani kwake Mtaa wa Kipata hadi kufikia mwaka wa 1942 alipohamia kwenye nyumba yake mpya Mtaa wa Aggrey na Sikukuu.
Nyumba hii nyumba hii ya Kipata ilipokuwa inakaliwa na Ally Sykes na harakati za kuunda TANU zinapamba moto Ally Sykes aliweka ‘’cylostyle machine,’’ kwenye nyumba hiyo ambayo alikuwa akichapa kwa siri mikaratasi yake ya ‘’uchochezi,’’ dhidi ya serikali.
Hii mikaratasi iliwahangaisha sana Special Branch wakaitafuta hii mashine hadi wakgundua ilipo na ukawekwa mtego wa kumnasa Ally Sykes.
Lakini hawakumpata.
Askari walipoingia ndani kufanya upekuzi wakakuta mashine na makaratasi vyote haviko vimetoweka kimiujiza.
Kwa hiyo haikuwa ajabu kuwa siku ile ya kupokea taarifa za kusajiliwa TANU hawa wazalendo - Abdul Ally na Nyerere waamue wakutane kwenye, ‘’command post,’’ yao Mtaa wa Kipata.
Hapo niruhusu msomaji niingize kitu kidogo.
Mkabala ya nyumba hii ilikuwa nyumba ya Abdallah Simba, Liwali wa Songea na rafiki ya babu yangu Salum Abdallah.
Baba yangu amekulia nyumba hii na kwa ajili hii basi yote ya wakati ule kayaona kwa macho yake na kama hakuyaona kayasikia kutoka kwa Abdul au Ally au kayasikia katika gumzo la mtaani mathalan siku nyumba ya Ally Sykes ilipozingirwa na askari waliokuja kukamata mashine iliyokuwa ikichapa makaratasi ya uchochezi dhidi ya serikali.
Barazani kwenye nyumba hii ya Liwali Abdallah Simba alikuwa fundi cherehani jina lake Kitwana.
Huyu Bwana Kitwana alikuwa rafiki ya baba yangu toka udogo wao hapo Mtaa wa Kipata hadi mimi napata umri wa utambuzi nimewakuta ni marafiki.
Miaka mingi baadae mimi nimekuwa sasa kijana nina fahamu zangu nilikuwa nikipita Mtaa wa Kipata namkuta Bwana Kitwana pale barazani bado akishona na nitasimama kidogo kumwamkia.
Siku zile za TANU Bwana Kitwana aliweza kuwa pale barazani anashona na akamsikiliza Nyerere akihutubia Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Mimi nikimwita ‘’Baba Mzee Kitwana,’’ kama tulivyofunzwa adabu njema na wazee wetu kuwa rafiki ya baba yako na yeye ni baba yako.
Mzee Kitwana yeye ameona ingia toka nyingi nyumbani kwa Ally Sykes katika siku zile za kuunda TANU miaka ya 1950.
Basi siku ile ya usajili wa TANU Abdul akawa kaja pale Mtaa wa Kipata nyumbani kwa mdogo wake Ally kumsubiri Nyerere arudi kutoka kwa Msajili wa Vyama awape taarifa.
Nyerere alipofika alikuwa mnyonge hana furaha akawapasha habari rafiki zake kuwa TANU imekataliwa usajili kwa kuwa Nyerere hakuwa na orodha ya wanachama.
Baada ya kusikia maneno yale Abdul akasema, ‘’Nitafutieni Mzee Said Chamweyewe.’’
Ally Sykes ndiye aliyechapa kadi 1000 za kwanza za TANU kutoka fedha zake mfukoni kisha akachapa kadi nyingine 2000 kwa fedha alizochukua TAGSA.
Mzee Said alipofika kwa Abdul Sykes, Abdul alimpa kadi za TANU na kitabu cha rejesta akamwambia aende Rufiji akaandikishe wanachama wa TANU.
Wanachama wakapatikana na majina yao akapelekewe Msajili.
Kizingiti hiki kikawa kimevukwa.
Mwandishi akiandika historia ya safari ya Nyerere UNO kuwa Nyerere alikwenda na kurudi bila kueleza matayarisho yake ndiyo yale yale ya mchuzi kutiwa maji.
Historia ya safari ya TANU hawezi kukamilika ikiwa haitaelezwa historia ya Iddi Faiz Mafungo aliyekuwa Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika, ambae ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kukusanya fedha za safari hii.
Iddi Faizi alipata kuwa Katibu wa TANU mbali ya kuwa Mweka Hazina.
Iddi Faiz ni mmoja kati ya wanachama wa mwanzo wa TANU waolihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo mwezi August 1954.
Iddi Faiz katika pilikapilika ya kukusanya fedha za safari ya UNO wakati akirudi kutoka Tanga alipokwenda kuchukua fedha za safari kutoka kwa Mwalimu Kihere, yeye bila kujua kumbe Special Branch walikuwa mgongoni kwake wakifuatilia nyendo zake zote.
Wakati anarudi Dar es Salaam yuko ndani ya basi askari walilisimamisha basi alilopanda wakamshusha na kumpekua lakini hawakumkuta na kitu.
Walimchukua hadi Central Police, Dar es Salaam kwa mahojiano lakini hakuna walichoambulia kutoka kwake.
Iddi Faiz alishikilia kauli yake kuwa yeye hajui lolote kuhusu hizo fedha wanazosema amezichukua kutoka Tanga.
Hawakuwa na la kumfanya wakamwachia.
Bila ya kumuunganisha Nyerere na wazalendo wenzake kama hawa aliokuwanao bega kwa bega siku zile katika kuijenga TANU na kupigani uhuru wa Tanganyika, historia ya Nyerere ya kupigania uhuru inapoteza uhalisia, inakuwa haina ladha wala msisimko unaostahili kuwapo.
Picha ya kwanza ni nyumba za mitaa ya Gerezani katika miaka ya 1950 na ya pili ni nyumba ya Ally Sykes Kipata kama ilivyo baada ya.kuvunjwa nyumba ya asili na kujengwa gorofa.
Picha ya tatu ni siku waliyomsindikiza Nyerere uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO Februari, 1955 kuliani kwa Nyerere ni Iddi Faiz Mafungo.