Wasifu wa Julius Nyerere: Usajili wa tanu, vizingiti vya Serikali, kusaka wanachama na safari ya Nyerere UNO 1955

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,788
30,084
WASIFU WA JULIUS NYERERE:

USAJILI WA TANU, VIZINGITI VYA SERIKALI, KUSAKA WANACHAMA NA SAFARI YA UNO 1955

Naendelea kusoma kitabu cha pili cha maisha ya Mwalimu Nyerere.

Historia ya TANU na wazalendo wake wote waliopigania uhuru wa Tanganyika ni ‘’one epic story,’’ ikiwa itaelezwa kwa ukweli wake.

Ikiwa mwandishi kwa hofu tu ya kuandika baadhi ya mambo mfano kueleza wale waliokuwa na Nyerere mstari wa mbele kutoka siku ya kwanza katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika na akaogopa kuandika ukweli atakuwa mchuzi wa historia ya TANU kautia maji na maji yale yataondoa ladha ya viungo vyote ndani ya upishi ule.

Jambo hili litamuathiri mpishi mwenyewe na ladha ya mchuzi wenyewe.

Nimejishtukia niko katika maisha ya Mwalimu Nyerere TANU ishaundwa na kusajiliwa, kadi zishatengenezwa, keshakwenda UNO na kurudi chama kinaendelea.

Hakuna taarifa vipi TANU iliundwa na vipi ilisajikiwa.

Hapa pamerashiwa.
Ngoma imeondolewa juani.

Ladha ya historia ya TANU inapotea.
Tuanze na siku Nyerere amekwenda kusajili TANU.

Abdul Sykes, mdogo wake Ally na Nyerere walikubaliana kuwa Rais wa TANU Julius Kambarage Nyerere aende kukisajili chama kwa Msajili wa Vyama akitoka huko wakutane Mtaa wa Kipata nyumbani kwa Ally Sykes ili kupeana taarifa.

Nyumba hii ya Kipata ina historia ndefu katika harakati za kupigania haki za Waafrika.

Kuanzia mwaka wa 1929 hadi 1942 haya ndiyo yalikuwa makazi ya Kleist Sykes, katibu muasisi wa African Association.

Mzee Kleist alikuwa akifanya mikutano mingi ya African Association pale nyumbani kwake Mtaa wa Kipata hadi kufikia mwaka wa 1942 alipohamia kwenye nyumba yake mpya Mtaa wa Aggrey na Sikukuu.

Nyumba hii nyumba hii ya Kipata ilipokuwa inakaliwa na Ally Sykes na harakati za kuunda TANU zinapamba moto Ally Sykes aliweka ‘’cylostyle machine,’’ kwenye nyumba hiyo ambayo alikuwa akichapa kwa siri mikaratasi yake ya ‘’uchochezi,’’ dhidi ya serikali.

Hii mikaratasi iliwahangaisha sana Special Branch wakaitafuta hii mashine hadi wakgundua ilipo na ukawekwa mtego wa kumnasa Ally Sykes.

Lakini hawakumpata.

Askari walipoingia ndani kufanya upekuzi wakakuta mashine na makaratasi vyote haviko vimetoweka kimiujiza.

Kwa hiyo haikuwa ajabu kuwa siku ile ya kupokea taarifa za kusajiliwa TANU hawa wazalendo - Abdul Ally na Nyerere waamue wakutane kwenye, ‘’command post,’’ yao Mtaa wa Kipata.

Hapo niruhusu msomaji niingize kitu kidogo.

Mkabala ya nyumba hii ilikuwa nyumba ya Abdallah Simba, Liwali wa Songea na rafiki ya babu yangu Salum Abdallah.

Baba yangu amekulia nyumba hii na kwa ajili hii basi yote ya wakati ule kayaona kwa macho yake na kama hakuyaona kayasikia kutoka kwa Abdul au Ally au kayasikia katika gumzo la mtaani mathalan siku nyumba ya Ally Sykes ilipozingirwa na askari waliokuja kukamata mashine iliyokuwa ikichapa makaratasi ya uchochezi dhidi ya serikali.

Barazani kwenye nyumba hii ya Liwali Abdallah Simba alikuwa fundi cherehani jina lake Kitwana.

Huyu Bwana Kitwana alikuwa rafiki ya baba yangu toka udogo wao hapo Mtaa wa Kipata hadi mimi napata umri wa utambuzi nimewakuta ni marafiki.

Miaka mingi baadae mimi nimekuwa sasa kijana nina fahamu zangu nilikuwa nikipita Mtaa wa Kipata namkuta Bwana Kitwana pale barazani bado akishona na nitasimama kidogo kumwamkia.

Siku zile za TANU Bwana Kitwana aliweza kuwa pale barazani anashona na akamsikiliza Nyerere akihutubia Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mimi nikimwita ‘’Baba Mzee Kitwana,’’ kama tulivyofunzwa adabu njema na wazee wetu kuwa rafiki ya baba yako na yeye ni baba yako.

Mzee Kitwana yeye ameona ingia toka nyingi nyumbani kwa Ally Sykes katika siku zile za kuunda TANU miaka ya 1950.

Basi siku ile ya usajili wa TANU Abdul akawa kaja pale Mtaa wa Kipata nyumbani kwa mdogo wake Ally kumsubiri Nyerere arudi kutoka kwa Msajili wa Vyama awape taarifa.

Nyerere alipofika alikuwa mnyonge hana furaha akawapasha habari rafiki zake kuwa TANU imekataliwa usajili kwa kuwa Nyerere hakuwa na orodha ya wanachama.

Baada ya kusikia maneno yale Abdul akasema, ‘’Nitafutieni Mzee Said Chamweyewe.’’

Ally Sykes ndiye aliyechapa kadi 1000 za kwanza za TANU kutoka fedha zake mfukoni kisha akachapa kadi nyingine 2000 kwa fedha alizochukua TAGSA.

Mzee Said alipofika kwa Abdul Sykes, Abdul alimpa kadi za TANU na kitabu cha rejesta akamwambia aende Rufiji akaandikishe wanachama wa TANU.

Wanachama wakapatikana na majina yao akapelekewe Msajili.

Kizingiti hiki kikawa kimevukwa.

Mwandishi akiandika historia ya safari ya Nyerere UNO kuwa Nyerere alikwenda na kurudi bila kueleza matayarisho yake ndiyo yale yale ya mchuzi kutiwa maji.

Historia ya safari ya TANU hawezi kukamilika ikiwa haitaelezwa historia ya Iddi Faiz Mafungo aliyekuwa Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika, ambae ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kukusanya fedha za safari hii.

Iddi Faizi alipata kuwa Katibu wa TANU mbali ya kuwa Mweka Hazina.

Iddi Faiz ni mmoja kati ya wanachama wa mwanzo wa TANU waolihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo mwezi August 1954.

Iddi Faiz katika pilikapilika ya kukusanya fedha za safari ya UNO wakati akirudi kutoka Tanga alipokwenda kuchukua fedha za safari kutoka kwa Mwalimu Kihere, yeye bila kujua kumbe Special Branch walikuwa mgongoni kwake wakifuatilia nyendo zake zote.

Wakati anarudi Dar es Salaam yuko ndani ya basi askari walilisimamisha basi alilopanda wakamshusha na kumpekua lakini hawakumkuta na kitu.

Walimchukua hadi Central Police, Dar es Salaam kwa mahojiano lakini hakuna walichoambulia kutoka kwake.

Iddi Faiz alishikilia kauli yake kuwa yeye hajui lolote kuhusu hizo fedha wanazosema amezichukua kutoka Tanga.

Hawakuwa na la kumfanya wakamwachia.

Bila ya kumuunganisha Nyerere na wazalendo wenzake kama hawa aliokuwanao bega kwa bega siku zile katika kuijenga TANU na kupigani uhuru wa Tanganyika, historia ya Nyerere ya kupigania uhuru inapoteza uhalisia, inakuwa haina ladha wala msisimko unaostahili kuwapo.

Picha ya kwanza ni nyumba za mitaa ya Gerezani katika miaka ya 1950 na ya pili ni nyumba ya Ally Sykes Kipata kama ilivyo baada ya.kuvunjwa nyumba ya asili na kujengwa gorofa.

Picha ya tatu ni siku waliyomsindikiza Nyerere uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO Februari, 1955 kuliani kwa Nyerere ni Iddi Faiz Mafungo.
 
Attachments

  • NYUMBA ZA GEREZANI 1950s.jpg
    NYUMBA ZA GEREZANI 1950s.jpg
    42.5 KB · Views: 1
  • NYUMBA YA SYKES KIPATA.jpg
    NYUMBA YA SYKES KIPATA.jpg
    5.9 KB · Views: 1
  • SAFARI YA JULIUS NYERERE UNO 1955.jpg
    SAFARI YA JULIUS NYERERE UNO 1955.jpg
    33.5 KB · Views: 1
Shukrani kwa historia nzuri sana mzee wangu

Hakika hakuna mapambano ya mtu mmoja, na ukiona mtu mmoja tu anajisifu amepambana basi hastahili kuitwa mpambanaji

Hata wahenga walituambia "usijisifu una mbio, msifu na aliyekukimbiza"
 
Shukrani kwa historia nzuri sana mzee wangu,
Hakika hakuna mapambano ya mtu mmoja, na ukiona mtu mmoja tu anajisifu amepambana basi hastahili kuitwa mpambanaji,
Hata wahenga walituambia "usijisifu una mbio, msifu na aliyekukimbiza"
Ahsante mama yangu.
 
WASIFU WA JULIUS NYERERE:

USAJILI WA TANU, VIZINGITI VYA SERIKALI, KUSAKA WANACHAMA NA SAFARI YA UNO 1955

Naendelea kusoma kitabu cha pili cha maisha ya Mwalimu Nyerere.

Historia ya TANU na wazalendo wake wote waliopigania uhuru wa Tanganyika ni ‘’one epic story,’’ ikiwa itaelezwa kwa ukweli wake.

Ikiwa mwandishi kwa hofu tu ya kuandika baadhi ya mambo mfano kueleza wale waliokuwa na Nyerere eleza mstari wa mbele kutoka siku ya kwanza katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika na akaogopa kuandika ukweli atakuwa mchuzi wa historia ya TANU kautia maji na maji yale yataondoa ladha ya viungo vyote ndani ya upishi ule.

Jambo hili litamuathiri mpishi mwenyewe na ladha ya mchuzi wenyewe.

Nimejishtukia niko katika maisha ya Mwalimu Nyerere TANU ishaundwa na kusajiliwa, kadi zishatengenezwa, keshakwenda UNO na kurudi chama kinaendelea.

Hakuna taarifa vipi TANU iliundwa na vipi ilisajikiwa.

Hapa pamerashiwa.
Ngoma imeondolewa juani.

Ladha ya historia ya TANU inapotea.
Tuanze na siku Nyerere amekwenda kusajili TANU.

Abdul Sykes, mdogo wake Ally na Nyerere walikubaliana kuwa Rais wa TANU Julius Kambarage Nyerere aende kukisajili chama kwa Msajili wa Vyama akitoka huko wakutane Mtaa wa Kipata nyumbani kwa Ally Sykes ili kupeana taarifa.

Nyumba hii ya Kipata ina historia ndefu katika harakati za kupigania haki za Waafrika.

Kuanzia mwaka wa 1929 hadi 1942 haya ndiyo yalikuwa makazi ya Kleist Sykes, katibu muasisi wa African Association.

Mzee Kleist alikuwa akifanya mikutano mingi ya African Association pale nyumbani kwake Mtaa wa Kipata hadi kufikia mwaka wa 1942 alipohamia kwenye nyumba yake mpya Mtaa wa Aggrey na Sikukuu.

Nyumba hii nyumba hii ya Kipata ilipokuwa inakaliwa na Ally Sykes na harakati za kuunda TANU zinapamba moto Ally Sykes aliweka ‘’cylostyle machine,’’ kwenye nyumba hiyo ambayo alikuwa akichapa kwa siri mikaratasi yake ya ‘’uchochezi,’’ dhidi ya serikali.

Hii mikaratasi iliwahangaisha sana Special Branch wakaitafuta hii mashine hadi wakgundua ilipo na ukawekwa mtego wa kumnasa Ally Sykes.

Lakini hawakumpata.

Askari walipoingia ndani kufanya upekuzi wakakuta mashine na makaratasi vyote haviko vimetoweka kimiujiza.

Kwa hiyo haikuwa ajabu kuwa siku ile ya kupokea taarifa za kusajiliwa TANU hawa wazalendo - Abdul Ally na Nyerere waamue wakutane kwenye, ‘’command post,’’ yao Mtaa wa Kipata.

Hapo niruhusu msomaji niingize kitu kidogo.

Mkabala ya nyumba hii ilikuwa nyumba ya Abdallah Simba, Liwali wa Songea na rafiki ya babu yangu Salum Abdallah.

Baba yangu amekulia nyumba hii na kwa ajili hii basi yote ya wakati ule kayaona kwa macho yake na kama hakuyaona kayasikia kutoka kwa Abdul au Ally au kayasikia katika gumzo la mtaani mathalan siku nyumba ya Ally Sykes ilipozingirwa na askari waliokuja kukamata mashine iliyokuwa ikichapa makaratasi ya uchochezi dhidi ya serikali.

Barazani kwenye nyumba hii ya Liwali Abdallah Simba alikuwa fundi cherehani jina lake Kitwana.

Huyu Bwana Kitwana alikuwa rafiki ya baba yangu toka udogo wao hapo Mtaa wa Kipata hadi mimi napata umri wa utambuzi nimewakuta ni marafiki.

Miaka mingi baadae mimi nimekuwa sasa kijana nina fahamu zangu nilikuwa nikipita Mtaa wa Kipata namkuta Bwana Kitwana pale barazani bado akishona na nitasimama kidogo kumwamkia.

Siku zile za TANU Bwana Kitwana aliweza kuwa pale barazani anashona na akamsikiliza Nyerere akihutubia Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mimi nikimwita ‘’Baba Mzee Kitwana,’’ kama tulivyofunzwa adabu njema na wazee wetu kuwa rafiki ya baba yako na yeye ni baba yako.

Mzee Kitwana yeye ameona ingia toka nyingi nyumbani kwa Ally Sykes katika siku zile za kuunda TANU miaka ya 1950.

Basi siku ile ya usajili wa TANU Abdul akawa kaja pale Mtaa wa Kipata nyumbani kwa mdogo wake Ally kumsubiri Nyerere arudi kutoka kwa Msajili wa Vyama awape taarifa.

Nyerere alipofika alikuwa mnyonge hana furaha akawapasha habari rafiki zake kuwa TANU imekataliwa usajili kwa kuwa Nyerere hakuwa na orodha ya wanachama.

Baada ya kusikia maneno yale Abdul akasema, ‘’Nitafutieni Mzee Said Chamweyewe.’’

Ally Sykes ndiye aliyechapa kadi 1000 za kwanza za TANU kutoka fedha zake mfukoni kisha akachapa kadi nyingine 2000 kwa fedha alizochukua TAGSA.

Mzee Said alipofika kwa Abdul Sykes, Abdul alimpa kadi za TANU na kitabu cha rejesta akamwambia aende Rufiji akaandikishe wanachama wa TANU.

Wanachama wakapatikana na majina yao akapelekewe Msajili.

Kizingiti hiki kikawa kimevukwa.

Mwandishi akiandika historia ya safari ya Nyerere UNO kuwa Nyerere alikwenda na kurudi bila kueleza matayarisho yake ndiyo yale yale ya mchuzi kutiwa maji.

Historia ya safari ya TANU hawezi kukamilika ikiwa haitaelezwa historia ya Iddi Faiz Mafungo aliyekuwa Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika, ambae ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kukusanya fedha za safari hii.

Iddi Faizi alipata kuwa Katibu wa TANU mbali ya kuwa Mweka Hazina.

Iddi Faiz ni mmoja kati ya wanachama wa mwanzo wa TANU waolihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo mwezi August 1954.

Iddi Faiz katika pilikapilika ya kukusanya fedha za safari ya UNO wakati akirudi kutoka Tanga alipokwenda kuchukua fedha za safari kutoka kwa Mwalimu Kihere, yeye bila kujua kumbe Special Branch walikuwa mgongoni kwake wakifuatilia nyendo zake zote.

Wakati anarudi Dar es Salaam yuko ndani ya basi askari walilisimamisha basi alilopanda wakamshusha na kumpekua lakini hawakumkuta na kitu.

Walimchukua hadi Central Police, Dar es Salaam kwa mahojiano lakini hakuna walichoambulia kutoka kwake.

Iddi Faiz alishikilia kauli yake kuwa yeye hajui lolote kuhusu hizo fedha wanazosema amezichukua kutoka Tanga.

Hawakuwa na la kumfanya wakamwachia.

Bila ya kumuunganisha Nyerere na wazalendo wenzake kama hawa aliokuwanao bega kwa bega siku zile katika kuijenga TANU na kupigani uhuru wa Tanganyika, historia ya Nyerere ya kupigania uhuru inapoteza uhalisia, inakuwa haina ladha wala msisimko unaostahili kuwapo.

Picha ya kwanza ni nyumba za mitaa ya Gerezani katika miaka ya 1950 na ya pili ni nyumba ya Ally Sykes Kipata kama ilivyo baada ya.kuvunjwa nyumba ya asili na kujengwa gorofa.

Picha ya tatu ni siku waliyomsindikiza Nyerere uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO Februari, 1955 kuliani kwa Nyerere ni Iddi Faiz Mafungo.
Unatukumbusha mengi hata ambao kwakipindi hicho tulikua hatujazaliwa
 
Mohamed Said mimi binafsi naamini katika historia inayochambuliwa, kukosolewa na kurejewa.

Kitu gani umejifunza kwenye vitabu hivi, ambacho hukukijua awali?
 
Mbona hayo majina yote ya waliopigania uhuru ni waislam,vp vijana wa kikristo kipindi hicho walikua wapi .
 
Kiranga,
Naomba kulitengeneza swali lako hapo katika yale ambayo sikuyajua awali ili niwe na uwanja wa kunitosha kuzungumza.

Kitu cha kwanza ni kuwa bado ipo hofu kubwa ya kuieleza historia ya Nyerere kwa ukweli wake khasa linapokuja kuundwa kwa TANU na historia za wale waliomtangulia katika hilo.

Waandishi wanawakwepa wazalendo kama Sykes Brothers, Hamza Mwapachu, Iddi Faiz Mafungo na wengineo mfano wa hao waliokuwa majimboni kama Yusuf Olotu, Bilal Rehani Waikela, Salum Mpunga kwa kuwataja wachache.

Utafiti mwingi umeelekezwa kwenye barua za Nyerere akiandikiana na wasomi wa Fabian Society na rafiki zake ilhali hao hawakuwapo katika uwanja wa mapambano.

Mchango wa Waislam kama Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi hauonekani sasa hapa sura inayojitokeza ni kuwa kanisa halikuunga mkono TANU na Waislam pia hawakuunga mkono TANU.

Lakini ukweli sasa unajulikana.

Bado ipo hofu ya kueleza ukweli.

Historia ya Nyerere na mgogoro wake na Waislam baada ya uhuru umekwepwa pia.
 
Fogohz,
Vijana wa Kikristo walikuwapo na walichangia katika kupigania uhuru lakini walikuwa wachache.

Waliingia kwa wingi baada ya Kura Tatu mwaka wa 1958.
 
Kiranga,
Naomba kulitengeneza swali lako hapo katika yale ambayo sikuyajua awali ili niwe na uwanja wa kunitosha kuzungumza.

Kitu cha kwanza ni kuwa bado ipo hofu kubwa ya kuieleza historia ya Nyerere kwa ukweli wake khasa linapokuja kuundwa kwa TANU na historia za wale waliomtangulia katika hilo.

Waandishi wanawakwepa wazalendo kama Sykes Brothers, Hamza Mwapachu, Iddi Faiz Mafungo na wengineo mfano wa hao waliokuwa majimboni kama Yusuf Olotu, Bilal Rehani Waikela, Salum Mpunga kwa kuwataja wachache.

Utafiti mwingi umeelekezwa kwenye barua za Nyerere akiandikiana na wasomi wa Fabian Society na rafiki zake ilhali hao hawakuwapo katika uwanja wa mapambano.

Mchango wa Waislam kama Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi hauonekani sasa hapa sura inayojitokeza ni kuwa kanisa halikuunga mkono TANU na Waislam pia hawakuunga mkono TANU.

Lakini ukweli sasa unajulikana.

Bado ipo hofu ya kueleza ukweli.

Historia ya Nyerere na mgogoro wake na Waislam baada ya uhuru umekwepwa pia.
Unafikiri kweli ufinyu huo wa kuandika mambo unatokana na hofu au ni mapungufu ya kawaida tu ya wanahistoria.

Historia ina mengi sana na si rahisi kumaliza yote, wewe kama muandishi unajua hilo.

Ndiyo maana mpaka leo miaka 55 baada ya kifo cha Churchill, watu wanaandika biograhies zake tu. Awali mwaka huu nimetoka kusoma biography ya Churchill iliyoandikwa na Andrew Roberts inaitwa "Churchill: Walking With Destiny".

Kitabu kina kurasa 1152, lakini hakijammaliza Churchill. Kuna vingine kaandika mwenyewe ma volume na volume, lakini kuna mengi hajayamaliza.

Nimetoa mfano wa biography ya Churchill kwa sababu ni mtu aliyeandikwa sana, na waandishi wengi wanamuandika tofauti na kujikita sehemu tofauti.Hakuna vitabu viwili vya maisha ya Churhill vilivyo sawa kabisa.

Sasa huoni kwamba inawezekana kilichowapelekea kuandika hivyo si hofu, ni uamuzi tu?

Wewe kama mwanahistoria, unajua sana kwamba kuna debate kubwa sana ya kuandika historia kwa kuangalia "big men's events" au kuandika historia kwa kuangalia maisha ya watu wengi, kwa maana ya kuangalia jamii kwa ujumla badala ya kufocus kwa mtu mmoja.

Sasa, huoni kwamba huu ni mtindo tu wa kuandika biography, unaojikita katika kumuangalia mtu mmoja zaidi ya jamii nzima iliyomzunguka?

Siku hizi kuna mpaka psychological biographies, watu wanaandikwa kwa namna ya kwamba inakuwa kama muandishi anataka kuingia kichwani cha anayeandikwa kujua alikuwa anajisikiaje muda huo, aliwaza nini etc.

Mimi binafsi naona usomi wa historia siku hizi umetoka kwenye ku glorify na ku lionize a few big men, na unaenda ku democratize history kwa kuwahusisha watu wengi zaidi. Kwa minajili hiyo, naungana nawe kwamba, kumuandika huyu giant Nyerere tu, bila kuwaelezea wale waliombeba kwenye mabega yao na kumfanya akawa giant, hakutaitendea haki historia. Kwa hilo nataka nikushukuru hata kwa kututajia majina tu ya waasisi wengi, pamoja na kuandika vitabu.

Lakini swali langu liko pale pale, unajuaje uandishi huu wa kumuweka mbele Nyerere tu umesukumwa na hofu, na si aina ya uandishi tu waliyotaka kuitumia waandishi?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom