Wasifu wa dr.slaa hazarani hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasifu wa dr.slaa hazarani hapa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lu-ma-ga, Sep 28, 2010.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Dk. Willibrod Peter Slaa

  1. Anachokisimamia

  Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, umakini na uwajubikaji katika uongozi wan chi na utendaji serikalini.
  Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzania wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti.

  2. Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

  Dk. Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung'unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

  3. Mafanikio ya DK. Slaa kielimu na Kitaaluma

  Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
  Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheriaü ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
  Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
  Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
  Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.


  4. Mafanikio ya Dk . Slaa kikazi na kitaalamu

  Dk. Slaa amefanya kazi katika maeneo na sehemu mbalimbali. Baadhi ya nyadhifa alizoshika na kazi alizofanya ni hizi zifuatazo:
  Mkurugenzi Mtendaji, Chama chaü Wasioona Tanzania, 1992 – 1998
  Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzaniaü (TEC), 1985 – 1991
  Mkurugenzi wa Maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu), 19977ü – 1979 na 1982 – 1985
  Padri wa Kanisa Katoliki kuanzia 1977 hadiü 1991

  5. Vitabu alivyoandika

  Utimilifu wa Msichana (1977)ü
  ü Utimilifu wa Mvulana (1977)
  Expediency and Exigency Liturgical Legislationü (1981)

  6. Ufasaha katika lugha nane (8)

  Dk. Slaa anajua kuzungumza na kuandiak ligha nane za kimataifa zifuatazo:
  Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.

  7. Uzoefu wa Dk. Slaa Kisiasa

  Dk. Slaa ana uzoefu wa musa mrefu katika shughuli za kisiasa. Baadhi ya nyadhifa alizoshika ni hizi zifuatazo.

  Mbunge wa karatu kwa miaka 15 kutoka 1995 hadi 2010

  Katibu Mkuu wa CHADEMA, 2002 hadi sasa
  Makamu Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, 1998 – 2002

  Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuuü wa CHADEMA kutoka 1995 hadi sasa

  8. Uzoefu wa Dk. Slaa KItaifa na Kimataifa

  Dk. Slaa ana uzoefu mbalimbali kitaifa na kimataifa kama ifuatavyo.

  Mjumbe w akuwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la Afrika,ü Carribean na Pcific-FU (ACP-EUC Joint Assembly), 1996 – 2000.

  Mjumbe kamatiü ya Uongozi (ACP-EU Joint Assembly)

  Mjumbe katika Bunge la SADC kutoka 1998ü hadi 2010

  Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge la SADC(Interü Parliamentary Cooperation and Capacity Building Committee) kutoka 1998 hadi 2010.

  Nibu kiongozi wa kamati ya Upinzani Bungeni, 2006-2010

  Mwenyekiti Kamati ya Hesabu za SErikali za Mitaa, Bunge la Tanzania 2008-2010

  9. Mafanikio kisiasa na kiutendaji

  Dk. Slaa amekuwa mbunge wa karatu kwa miaka 15 mfululizo.
  Karatu ni moja ya wilaya hapa nchini zenye maafanikio makubwa ikiwamo miundo mbinu bora, maji na huduma nyingine za kijamii, Dr. Slaa anataka kutumia uzoefu wake wa miaka 15 ya ubunge wa karatu kwa ajili ya taifa zima.

  Ndiye katibu Mkuu aliyefanikiwa zaidi kuijenga CHADEMA kwa kushirikiana na viongozi wengine ameweza kuipitisha CHADEMA katika changamoto mbalimbali na kukifanya kuwa chama kilicho tayari kushika uongozi wa taifa.

  Bila kujali vitisho vya watawala aliibua rasmi kafsha za ufisadi mbaya kuliko zote zilizowahi kutokea hapa nchini zikihusisha wizi wa fedha za umma katika Benki kuu. Madai yake mazito Bungeni yalimlazimisha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu nchini kutoroka nchini.

  10. Baadhi ya vipaumbele vya Serikali itakayoundwa na Dk Slaa
  Kuanzisha mchakato wa kuandikisha upya katiba nadni ya siku 100 baada ya kuunda serikali.  Kupambana na kuwashughulikia mafisadi katika nafasi zote, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha
  zote zilizoibwa zinarejeshwa na wahusika wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

  Kuhakikisha kuwa kilimo chetu kiwe bore naü cha kisasa, chenye faida na kinachofikia viwango vya kimataifa katika kuvuna, kuhifadhi, kusafirisha na kuuza mazao mbalimbali.

  Kuhakikisha kuwa kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora katika ngazi zote.

  Kuanzisha utaratibu wa kuwalipa pensheni wazee wote wenye umri wa umri 60 na kuendelea nchi nzima na kurekebisha mfumo wa malipo ya pensheni kwa wastaafu.

  Kuanzisha utaratibu mpya wa upandaji mishahara kwa watumishi wa umma na wa sekta binafsi utakaohakikisha kuwa misharara inapanda kadri gharama za maisha na mfumuko wa bei unavyopanda
   
Loading...