Wasifu (CV) ya Mrisho Gambo aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

4b996e0f552f46d5a59386c3a511d94b.jpg
Kijana wa mfano wa kuigwa.
iga
 
Gambo atavurunda Arusha, hachelewi, maana aliyemteua anafikiri anaweza kukabiliana na upinzani.... Akicheza rafu yatamkuta yaliyomkuta Mulongo mapema sana....
 
Ni kiongozi mzuri, mfuatiliaji na mbunifu. Hata hivyo anatakiwa kupunguza jazba. Ajifunze pia kuwa na akiba ya maneno na kuepuka kutumia nguvu kupita kiasi.
 
Mrisho gambo amesema yy hajabebwa kama wasemvyo watu


Kuna watu wameniomba niweke CV yangu hapa, naiweka kwa muhtasari tu!

Nizaliwa Mei 22, mwaka 1982 katika Hospitali ya Ocean Road ya Dar es Salaam. Nilipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Ilala Boma na kuhitimu darasa la saba mwaka 1997 na kupata bahati ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kidato cha kwanza hadi cha nne, katika Shule ya Sekondari Kibaha na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2001. Mwaka 2002 nilichaguliwa kujiunga kidato cha tano Shule ya Ufundi Tanga, maarufu kama Tanga Technical School. Nilihitimu kidato cha sita mwaka 2004.

Mwaka 2005 nilichaguliwa kujiunga na elimu ya juu, katika Chuo cha Uhasibu Arusha, kusomea stashahada ya juu katika Sayansi ya Kompyuta (computer science) na kuhitimu mwaka 2008. Mwaka 2009 niliajiriwa kwa nafasi ya mchambuzi wa mifumo ya kompyuta katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Mwaka 2011, niliajiriwa kama msimamizi mwandamizi wa mifumo ya kompyuta wa Chuo cha Kimataifa cha Nelson Mandela. Pia mwaka 2011 nilijiuzulu nafasi hiyo pale Chuo cha Nelson Mandela na kurudi Jiji la Arusha. Niliweza kurudi Jiji la Arusha kwa kuwa sikuwa nimeacha kazi, bali niliomba likizo bila malipo.

Baadaye niliendelea na safari yangu ya elimu na mwaka 2010 nijiunga tena Chuo cha Uhasibu Arusha kusoma shahada ya uzamili (masters degree) katika masuala ya uongozi na teknolojia ya habari na kuhitimu mwaka 2011.

April 2012 niligombea ubunge wa Afrika Mashariki na na kushika nafasi ya sita kati ya watu 81 tuligombea.

May 2012 niliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe nafasi ambayo ninayo hadi sasa!
 
Kwa hiyo anajisifu, akamuuliza yule aliyekuwa mkuu wa mkoa Morogoro na PhD yake nini kilimtokea
 
Uteuzi wa JPM kuhusu Gambo umezua gunzo jijini Arisha kiasi cha baadhi ya wananchi kuwa rais amechemka.
 
Kama anataka kuendelea kubaki Arusha, sharti ni moja, Aache kiherehere cha KiCCM na atulie na kufanya kazi kwa weledi sio kuwabugudhi wapinzani. La Sivyo hachukui Round hapa. Amuulize Mulongo!
Jamani wana JF kila ninaposoma naona maandishi yanayomuonya RC mpya wa Arusha kuwa akitaka kujua amuulize Mulongo yaliyomkuta Arusha. Naomba kufahamishwa Mulongo alikumbwa matukio gani Arusha ambayo hawezi kuyasahau.
 
Kama anataka kuendelea kubaki Arusha, sharti ni moja, Aache kiherehere cha KiCCM na atulie na kufanya kazi kwa weledi sio kuwabugudhi wapinzani. La Sivyo hachukui Round hapa. Amuulize Mulongo!
Kama anataka kuendelea kubaki Arusha, sharti ni moja, Aache kiherehere cha KiCCM na atulie na kufanya kazi kwa weledi sio kuwabugudhi wapinzani. La Sivyo hachukui Round hapa. Amuulize Mulongo!
We km nani?!
 
CHADEMA mnaonesha mmepanic na Huu uteuzi!shughuli ya kujamba mnaharisha!hapa mlitakiwa kumpongeza na kuahidi kutoa ushirikiano na si vingine!huyu ni rais wa mkoa!
 
Back
Top Bottom