Wasichokifahamu NEC

Wasichokifahamu NEC

emalau

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Posts
2,775
Reaction score
3,109
Kwa siku mbili au tatu zilizopita nimekuwa nikifuatilia kwenye vyombo vya habari juu ya rai ya NEC kuwataka watu kuondoka kwenye vituo vya kupigia kura mara baada ya kupiga kura.
Katika jamii ya watu wastaarabu na wanaotendeana haki hivyo ndo inavyotakiwa kuwa. Katika makala yake Generali Ulimwengu kama wiki mbili zimepita alisema katika chaguzi za nchi za Afrika hatujafikia kiwango cha ustaarabu cha kutendeana haki.

Katika kudhihirisha hilo katika uchaguzi uliopita kama watu wangepiga kura wakarudi nyumbani leo hii mbunge wa Arusha mjini Lema asingekuwa mbunge. Wenje Nyamagana asingekuwa mbunge, Nasari asingekuwa mbunge. Wasimamizi walikuwa wakipewa presha watangaze watu walioshindwa kuwa washindi, lkn kwa usimamizi wa wananchi waliobaki vituoni ushindi ulilindwa. Kwa mfano Arumeru thermosi zilikuwa zinaingizwa na kura lkn wananchi walizuia.

Isitoshe CCM ni chama bilionea uwezekano wa kuwahonga wasimamizi ni mkubwa sana. Kwa hiyo NEC inapotoa matamko yake ijue inafanya kazi ktk jamii ambayo kutendeana haki bado kuko katika kiwango cha chini, kwa hiyo watwambie ni kwa namna gani tunaweza kuzuia hilo.

Nawakilisha wanajamii
 
Mkurugenz wa NEC alikuw msajir wa mahakam sitak kuongelea uwezo wake ila natak kuongelea upofu unaotufanya kuwa wapuuz kias hik anakir kwamb sheria ya uchaguz kifungu cha 104 kinazuia mkusanyiko au mkutano au kuvaa sare ndan ya mita 200... Kwa tafsir yake anasema kwamb sheria haijaruhus kuksanyika nje ya mita mia mbili sasa najiuliza jee sheria ya uchaguz ilkuw na intention gani kuwek limit ya mita 200 kwann haikuzuia moja kwa moja bila kuwek limit
 
DA wewe jamaa una akili sana, umeongea oja na ushahidi,safi sana ni bahati sana kuwa na watu kama wewe,hapa nakuhakikishia kuwa goli la mkono linatafutiwa mazingira.tusubiri.
 
Katika makala yake Generali Ulimwengu kama wiki mbili zimepita alisema katika chaguzi za nchi za Afrika hatujafikia kiwango cha ustaarabu cha kutendeana haki.

Hapa umemaliza kila kitu.
Ndio maana hadi leo tume ya uchaguzi haiaminiki kabisa.
Hawapo tayari kufanya uchaguzi wa huru na haki hadi washurutishwe na wananchi.
 
Kama sheria inaongelea mita mia mbili , basi tutaiheshimu sheria na kukaa mita mia mbili
 
Mkurugenz wa NEC alikuw msajir wa mahakam sitak kuongelea uwezo wake ila natak kuongelea upofu unaotufanya kuwa wapuuz kias hik anakir kwamb sheria ya uchaguz kifungu cha 104 kinazuia mkusanyiko au mkutano au kuvaa sare ndan ya mita 200... Kwa tafsir yake anasema kwamb sheria haijaruhus kuksanyika nje ya mita mia mbili sasa najiuliza jee sheria ya uchaguz ilkuw na intention gani kuwek limit ya mita 200 kwann haikuzuia moja kwa moja bila kuwek limit

Kuweka taarifa yako vizuri Kailima professionally ni afisa rasilimali watu aka afisa utumishi na alikuwa mkurugenzi wa utawala kabla ya kuwa mkurugenzi wa nec. Hajawahi kuwa msajili wa mahakama
 
Kulinda kura ni lazima. Kama nia ya JK siyo kuiba kura, yeye watu kusubiri matokeo vituoni linamkera kwa nini?
 
Leo Mtukufu rais wetu, Mh. Prof. Dr. Hon. Mrisho Kikwete amesisitiza kuwa, kichapo kipo kwa asilimia 100 kwa wale watakao kaa hata mita 1000 kutoka kituoni.
Sasa, tunajiuliza, yeye hazisomi sheria hizi?? Na kwanini ccm wajisumbue hivi na watu walioketi mahali pamoja bila kelele wala mkwaruzo wanangojea tu atangazwe mshindi wao??
Naanza kuwaamini wale wataalamu wa magoli ya mikono. Kumbe ndo maana mnasema; Ushindi ni lazima?? Je, hizo kura mmeshazipiga tayari? Kwa nini msumbue watu kwenda vituoni wakati ushindi tayari mnao?? Je, hiyo fedha ya kupigia kura kura mabayo tiyari mshindi ,mnaye, si mnunulie hata watu Panadol tu kuliko kuiharibu?? Nawaza tuu msinichukue bureeee
 
Tutafuata Sheria ya Uchaguzi Ni Meta 200; Haya Matamko Mengine Ni Kama Campaign za Kisiasa Kama Walivyotamka ya kwamba

Wanao uwezo, Ujuzi na Maarifa ya Kushinda Uchaguzi. La Muhimu Ni Sheria Ifuatwe" Kura zeetu Tutazilinda" Kwani tume Hii ya CCM

Hawaaminiki.

UKAWA Walishasema Wapigakura Tulinde Kura zetu na sheria ya Uchaguzi Inatukubalia Kusubiria Mita 200. Ni Ujinga

Kwenda Kupiga Kura ukaenda Kulala, Kunywa pombe au Kucheza bao Huku nyumba Impact ya Kura yako Isifanye Ulichokikusudia

"Mabadiriko".Lowassa & Mbowe Walishasema Tusubirie Matokeo Mita 200.
 
Leo Mtukufu rais wetu, Mh. Prof. Dr. Hon. Mrisho Kikwete amesisitiza kuwa, kichapo kipo kwa asilimia 100 kwa wale watakao kaa hata mita 1000 kutoka kituoni.
Sasa, tunajiuliza, yeye hazisomi sheria hizi?? Na kwanini ccm wajisumbue hivi na watu walioketi mahali pamoja bila kelele wala mkwaruzo wanangojea tu atangazwe mshindi wao??
Naanza kuwaamini wale wataalamu wa magoli ya mikono. Kumbe ndo maana mnasema; Ushindi ni lazima?? Je, hizo kura mmeshazipiga tayari? Kwa nini msumbue watu kwenda vituoni wakati ushindi tayari mnao?? Je, hiyo fedha ya kupigia kura kura mabayo tiyari mshindi ,mnaye, si mnunulie hata watu Panadol tu kuliko kuiharibu?? Nawaza tuu msinichukue bureeee

Kama kweli Mh Raisi hana nia mbaya awaache watu wakae mita 200 wasubiri matokeo yao hata kama yatatoka kesho yake nauhakika watu watakesha.. Kama vipi Lowassa na team nzima ya Ukawa waombe msaada umoja wa mataifa mapemaa wanaweza shushiwa meli ya watu hapa fasta.
 
Kulinda kura ni lazima. Kama nia ya JK siyo kuiba kura, yeye watu kusubiri matokeo vituoni linamkera kwa nini?

Sioni shida yao na hofu ya nini ?

Anayetaka kusibiria matokeo akiwa nyumbani kwake aende waliotayari kusibiria mita mia mbili hata kama siku ya Tatu waendelee shida iko wapi. Si ni haki ya kupata majibu baada ya upigaji kura!

Masharti ya kutokuleta vujo au kampeni au mkutano sharti ya zingatiwe na watakaobaki kisubiri matokeo!

Leo Raisi wao kasema kuwa wapiga kura wako 28mil....
Sheria inasema tukae 200m leo wamekataa kila kitu
 
mimi nasema nitakaa mita mia mbili away, kama nikuniua acha waniua lakini damu yangu itakuwa imekomboa kizazi changu. i'm sick n tired of injustice in this country
 
Kwa siku mbili au tatu zilizopita nimekuwa nikifuatilia kwenye vyombo vya habari juu ya rai ya NEC kuwataka watu kuondoka kwenye vituo vya kupigia kura mara baada ya kupiga kura.
Katika jamii ya watu wastaarabu na wanaotendeana haki hivyo ndo inavyotakiwa kuwa. Katika makala yake Generali Ulimwengu kama wiki mbili zimepita alisema katika chaguzi za nchi za Afrika hatujafikia kiwango cha ustaarabu cha kutendeana haki.

Katika kudhihirisha hilo katika uchaguzi uliopita kama watu wangepiga kura wakarudi nyumbani leo hii mbunge wa Arusha mjini Lema asingekuwa mbunge. Wenje Nyamagana asingekuwa mbunge, Nasari asingekuwa mbunge. Wasimamizi walikuwa wakipewa presha watangaze watu walioshindwa kuwa washindi, lkn kwa usimamizi wa wananchi waliobaki vituoni ushindi ulilindwa. Kwa mfano Arumeru thermosi zilikuwa zinaingizwa na kura lkn wananchi walizuia.

Isitoshe CCM ni chama bilionea uwezekano wa kuwahonga wasimamizi ni mkubwa sana. Kwa hiyo NEC inapotoa matamko yake ijue inafanya kazi ktk jamii ambayo kutendeana haki bado kuko katika kiwango cha chini, kwa hiyo watwambie ni kwa namna gani tunaweza kuzuia hilo.

Nawakilisha wanajamii

Kwenye kura zao za maoni rushwa ilikuwa ndio muhimili wa kuchaguli. Leo tuta waamini vipi. Kwamba nguruwe tumachie shamba la mihogo?
 
Wanahangaika na suala mabalo liko kisheria. Wao kazi yao iwe kusimamia sheria ili watu wasiivunje; siyo kutunga sheria ingine kwa matamko na maelekezo. Nafikiri tatizo kubwa liko kwenye muundo wa tume ambao unawashawishi wananchi kutokuwa na imani kwamba itatenda haki na hivyo maelekezo kama haya nje ya sheria yanazidi kuwaaminisha hivyo. Siku kadhaa zilizopita Mh Jaji Lubuva mwenyewe alishasema hana uwezo wa kuwawajibisha wasimamizi wa uchaguzi huko wilayani na kwenye kata kwa sababu hawawajibi kwake!
 
kwa hizi kauli mbili ya kwanza kutoka kwa nape bao la mkono. na pili rais kikwete kusisitiza kukaa mbali na vituo ingawa sheria imefafanua ni umbali wa mita 200. ni wazi hapa kuna siri nzito. lakini tutayajua yote haya ngoja tusubiri.
 
Leo Mtukufu rais wetu, Mh. Prof. Dr. Hon. Mrisho Kikwete amesisitiza kuwa, kichapo kipo kwa asilimia 100 kwa wale watakao kaa hata mita 1000 kutoka kituoni.
Sasa, tunajiuliza, yeye hazisomi sheria hizi?? Na kwanini ccm wajisumbue hivi na watu walioketi mahali pamoja bila kelele wala mkwaruzo wanangojea tu atangazwe mshindi wao??
Naanza kuwaamini wale wataalamu wa magoli ya mikono. Kumbe ndo maana mnasema; Ushindi ni lazima?? Je, hizo kura mmeshazipiga tayari? Kwa nini msumbue watu kwenda vituoni wakati ushindi tayari mnao?? Je, hiyo fedha ya kupigia kura kura mabayo tiyari mshindi ,mnaye, si mnunulie hata watu Panadol tu kuliko kuiharibu?? Nawaza tuu msinichukue bureeee

Atavaa jezi na familia yake ili watekeleze hizi orders za kuwashikisha adabu watanzania?

Polisi wenyewe wamechoka na mateso wanataka mabadiliko na kamwe hawatakuwa tayari kutumia kuua ndugu zao kwa misingi ya kuhujumu haki.

Jeshi la wananchi halina hata mpango. Tena shida ni pale taarifa za Mwamunyan... zinavyokuwa tata bila maelezo ya kina kutolewa.

Hakuna jeshi litamsadiai kufanya hujuma. Labda avae jezi na familia yake, waende kupiga wananchi wasio na hatia.

Tutakaa mita mia mbili kama shria yetu inavyotupa uhuru. Mengine haya, ni yake na mke na watoto wake. Sisi hayatuhusu na wala asitake kulazimisha majeshi yetu yafanye kazi haramu.

Kikubwa kwa sasa anatakiwa atoe amri, General Dave atoke aliko aje kusema na wananchi. Kinyum cha pale hasomeki na hana suppoort yoyote ya kuringia kutoka ndani na nje ya chama na sirikali yake.
 
Leo Mtukufu rais wetu, Mh. Prof. Dr. Hon. Mrisho Kikwete amesisitiza kuwa, kichapo kipo kwa asilimia 100 kwa wale watakao kaa hata mita 1000 kutoka kituoni.
Sasa, tunajiuliza, yeye hazisomi sheria hizi?? Na kwanini ccm wajisumbue hivi na watu walioketi mahali pamoja bila kelele wala mkwaruzo wanangojea tu atangazwe mshindi wao??
Naanza kuwaamini wale wataalamu wa magoli ya mikono. Kumbe ndo maana mnasema; Ushindi ni lazima?? Je, hizo kura mmeshazipiga tayari? Kwa nini msumbue watu kwenda vituoni wakati ushindi tayari mnao?? Je, hiyo fedha ya kupigia kura kura mabayo tiyari mshindi ,mnaye, si mnunulie hata watu Panadol tu kuliko kuiharibu?? Nawaza tuu msinichukue bureeee

Hahahaaa mkuu, ur just thinking loud??
 
Hebu tujiulize swali rahisi hv unaweza kwenda dukani ukampa mwenye duka pesa na usimwambie nini unahitaji na ukaondoka,mwenye duka akisema ww ni kichaa hakika atakuwa sahihi,hivyo ndivyo CCM wanavyotugeuza vichaa tupige kura tuondoke bila kujua kitu.Tutakaa Mita 200 kwa Amani kama tulivyokaa kwenye chaguzi za seeikali za mitaa kwa amani kabisa.
 
Hivi hakuna uwezekano wa kutafuta uhalali wa kisheria kwa kumshitaki lubuva kabla ya uchaguzi ili kuepusha vurugu ?
 
Back
Top Bottom