Wasichana wa chuo na mashauzi kumbe hawana kitu

Rich Pol

JF-Expert Member
Oct 11, 2013
7,874
5,683
Pole na majukumu wana JF.
Nimeona tu share hiki kisa nilikutana nacho mwanzoni mwa mwezi huu.
Nilikuwa Mwanza airport kwa safari ya kurudi Dar. Baada ya kucheck in nikiwa nimekaa kusubiri kuingia kwenye ndege pembeni yangu alikuja akakaa bint mzuri tu akiwa busy na simu yake, hakunisalimia nikaona nimsalimie japo nisikie sauti yake, badala yake aliitikia kwa kichwa tu bila kuniangalia,

Muda si mrefu akaja jamaa wa cargo akimfuata yule dada akaanza kuongea kwa sauti ya juu kila mtu alisikia pale akimwambia samaki wake wamezidi uzito hiyo hela haitoshi kama vipi aongeze elfu 10 au ndoo moja ibaki,

Nikaamua kumsema jamaa awe na adabu siyo kupayuka kila mtu asikie jamaa akaomba msamaha, ila yule demu akasisitiza hana hela na samaki wale ameagizwa tu na hela aliyopewa ndiyo hiyo, nikaamua kutoa wallet na kumpa yule mtu akaondoka, demu akaniambia asante nami nikaitikia kwa kichwa.

Tumesafiri na tumefika Dar saa tatu kasoro usiku, nikiwa nje nikamuona na ndoo mbili za samaki na bag lake anapatana bei na driver taxi mpaka sinza, eti ana elfu 15, ma driver taxi wakamwambia hiyo hela tukakuache buguruni uchukue daladala, nikaona nimsaidie tena maana ndugu yangu alinifuata pale, nikamchukua na kumuacha sinza mori alishukuru sana akachukua namba yangu.

Weekend iliyofuata akanipigia simu anataka kunitoa dinner nikakubari, kweli jioni akaniambia nimfuate Namanga yuko saloon na yuko na rafiki yake, nami nikamchukua rafiki yangu na kumpitia, nikamuuliza unanitoa out kiwanja gani? Akajibu chagua mwenyewe, nia yangu nijue uwezo wake kipesa,

Nikaamua twende Sea cliff na tukaingia Spurs, tukala na kunywa wote wanne tulienjoy sana, sasa ikaja bill na jamaa akanipa mimi, mimi nikampa demu maana ndiye aliniomba kunitoa out, alipoifungua bill nikaona macho yamemtoka,

Baadaye wakaanza kujadiliana na mwenzie chinichini nami nikawa busy na simu yangu, mwisho " am sorry Rich utakuwa na hela hapo maana pale saloon wametucharge zaidi huku imepungua, nikaichukua bill na kuingalia ilikuwa 187,500. Akawa ananipa elfu 50 niongezee, nikamwambia it's ok nikachukua $100 nikaweka kwenye bill baada ya chanji kurudi tukaondoka na nikawaacha sinza.

NB: Nyie wanawake tukiwatoa out mjue huwa tumejipanga haswa, msijaribu kutuiga.
 
We nawe unazingua...kama ungekuwa umemwambia yeye akuchagulie alafu mkaenda sehemu akashindwa kulipa dongo lako lingekuwa na mantiki. Pengine hakuwa anajua bei....hiyo ni # 1. 2# We mtu kasema anakutoa we we out unaanzaje kubebana na mshkaji???! Mlikubaliana iwe hivyo???Bajeti yake ulikuwa unaijua!!!???

Next time nenda mwenyewe, na mlipaji ndo achague pa kwenda.
 
We nawe unazingua...kama ungekuwa umemwambia yeye akuchagulie alafu mkaenda sehemu akashindwa kulipa dongo lako lingekuwa na mantiki. Pengine hakuwa anajua bei....hiyo ni # 1. 2# We mtu kasema anakutoa we we out unaanzaje kubebana na mshkaji???! Mlikubaliana iwe hivyo???Bajeti yake ulikuwa unaijua!!!???

Next time nenda mwenyewe, na mlipaji ndo achague pa kwenda.
Aliniambia yuko na rafiki yake nami nikamwambia nakuja na rafiki yangu
 
Back
Top Bottom