Wasichana 11 wadaiwa kufanya ukahaba Dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
WASICHANA 11 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Sokoine Drive jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kufanya biashara ya kujiuza katika maeneo ya wazi.

Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, John Kijumbe alidai jana kuwa watuhumiwa walitenda kosa hilo, Oktoba 14, mwaka huu.

Alidai wasichana hao, walikutwa barabara ya ufukweni saa 8:15 usiku wakiuza miili yao, jambo ambalo ni kosa kisheria.
Kijumbe aliwataja watuhumiwa kuwa ni Lucy Edward (21), Abir Ameir (24), Fatuma Ghaza (20), wakazi wa Kinondoni wakati Janeth Joseph (30) na Amina Ramadhani (26), wakazi wa Magomeni.

Aliwataja wengine kuwa ni Lina Frank (22), mkazi wa Tabata Bima, Subira Suleiman, (26) mkazi wa Mchikichini wilayani Ilala, Paulina John (27), mkazi wa Changombe, Mwanaidi Hussein (31), mkazi wa Mwananyamala, Fatuma Said (26), mkazi wa Mabibo na Amina Abdallah (35), mkazi wa Mbagala.

Watuhumiwa hao, walikana shtaka hilo na walirejeshwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kulipa Sh1 milioni kila mmoja. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 18, mwaka huu.

Wakati huohuo, wapigadebe watatu wamepandishwa kizimbani kwa kosa la kuwalazimisha abiria kupanda magari wasiyoyataka.
Mwendesha mashtaka huyo, alidai watuhumiwa walitenda kosa hilo, Oktoba 15 maeneo ya Mbagala Mission.

Aliwataja wapigadebe hao kuwa ni Said Juma (24), Kibwana Abudi, (25), na Mudsa Abdullah (22).

Hata hivyo, watuhumiwa walikana shtaka hilo na wamerejeshwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kulipa Sh 5,000 kila mmoja.

Mahakama imehairisha kesi hiyo mpaka Oktoba 21, mwaka huu itakapotajwa tena.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Matatizo ya Dada zetu kufanya mambo ya ukahaba Mijini yataisha lini jamani?
 
Ulianza siku nyingi sana kwa hiyo kudhani utakwisha ni kupoteza muda, watu wakajifunze Uholanzi
 
ukahaba hauendani na umaskini, ni tabia+tamaa ya kutaka vya juu, hata nchi tajiri ukahaba upo

Upo sahihi mkuu, kama ni umasikini ndo sababu nchi tajiri kusingekuwa na makahaba, vile vile kwenye vijiji ambako kuna umasikini wa kutisha ndo kungekuwa na makahaba weng
 
Back
Top Bottom