Washirika wa Hamad Rashid waanzisha chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Washirika wa Hamad Rashid waanzisha chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed


  Hatimaye washirika wa Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, wamewasilisha maombi kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, kuomba kusajili chama kipya cha Alliance for Democratic Change (ADC).

  Maombi hayo yaliwasilishwa jana mchana na Mwenyekiti wa muda wa chama hicho, Said Miraji Abdullah, ambaye ni mshirika wa karibu wa Hamad na Katibu Mkuu wake, Kadawi Limbu, na kupokelewa na Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Galasia Simbachawene.

  Miongoni mwa nyaraka zilizoambatanishwa na barua ya maombi hayo, ni pamoja na fomu PP 2 ya tamko la maombi ya usajili, PP 1 ya maombi ya kupewa usajili, nakala ya rasimu ya katiba ya chama hicho toleo la kwanza, 2012 pamoja na stakabadhi ya malipo ya maombi.

  Akipokea nyaraka hizo kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, Simbachawene alisema zitapelekwa kwa wanasheria kwa ajili ya kupitiwa na kwamba, iwapo zitabainika kuwa zina upungufu, zitarejeshwa kwa uongozi wa chama hicho kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho kabla ya kuwasilishwa tena kwa Ofisi ya Msajili.  Washirika wengi wa Hamad Rashid ambao baadhi walikuwa viongozi na wanachama wa kawaida wa Chama cha Wananchi (CUF) waliojiengua katika chama hicho kwa nyakati tofauti, walifika katika ofisi za msajili, huku wanachama wanawake waliovalia fulana za rangi nyeusi zenye maandishi ya rangi nyeupe yanayosomeka: ‘Anti Virus’ wakiimba kwa furaha, “Chama kipya,…chama kipya,…chama kipya.”


  Miraji ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama cha Wananchi (CUF), ikiwamo Ukurugenzi wa Ulinzi na Usalama na Umeneja wa Kampeni za mgombea urais wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alisema wamelazimika kuanzisha ADC, baada ya vyama vilivyopo kutokuwa na uwakilishi wa wananchi.

  Alisema ADC haitajali mtu yeyote kwa misingi ya dini, rangi wala kabila lake, badala yake watu wote watakuwa na nafasi sawa katika chama hicho.

  Naye Limbu ambaye aligombea ubunge kwa tiketi ya CUF Jimbo la Temeke katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alisema kutojiunga na vyama vingine vya siasa baada ya kujiengua CUF, kumetokana baada ya kubaini vyama hivyo havina tofauti na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa maneno mazuri, lakini yenye udanganyifu ndani yake, huku rasilimali za nchi zikiishia mikononi mwa watu wachache.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Anti Virus means Anti Coruption, Anti Sultanism Etc,etc! ADC - Dira ya Mabadiliko.
   
Loading...