Mkuu Inakuuma,
Unajua kwamba Lema ni aina ya kiongozi mwenye mvuto has kwa vijana.Siku ya mazishi ya Mheshimiwa Sumari Vijana walishindwa kuzuia hisia zao na kwenda kumzonga.Hili kimsingi sio kosa lake,si rahisi yeye angewafukuza kwamba nendeni kule.Laiti kama hao washili wangethibitisha maneno ambayo LEMA aliyasema ya kuwakashifu hapo sawa tungejadili hii issue.Wameishia kusema kwamba lema aliwaudhi kwa kukusanya kundi la vijana.
Laiti ungejua jinsi LEMA anavyopendwa Arusha ungeelewa ninachosema.Lema anapendwa,Ana ushawishi mkubwa ndio maana hawa wazee wanaitwa washili ambao mwenyekiti wao ni Hezron Sumari wa ukoo wa Sioi Sumari lazima wamwogope kwamba atabadilisha akili za watu wengi.Kina Hezron na washili wenzake wanapigania mtoto wao Sioi apite.