WASHAIRI TUSILALE.
Sanaa ya ushairi ni sanaa ya kale
sana na pia ni sanaa inayodumu kwa
miaka mingi na pia ni sanaa
inayoafanya marika yote bila ya kuleta
athari kwa rika lingine na bado marika
yote yakafanya kazi kwa pamoja.
ni sanaa yenye maadili na kuzingatia
tamaduni za jamii.
ni wakati sasa wa wasanii wa sanaa
hii kuhamka na kufanya kazi ya
ushairi kwa masilahi na kuelimisha
jamii.
mashairi ni mengi sana na kila siku
yanaandikwa na swali la kujiuliza ni
JE WASHAIRI WANAFAIDIKA VIPI
KUPITIA KAZI ZAO ?
unaweza kudhani labda ushairi wa
zama hizi haupendwi lakini kiukweli
sanaa hii inawapenzi wengi ila tatizo
wasanii wenyewe hawajajitoa
kupeleka kazi zao ktk jamii kama
wafanyavyo wAnamuziki wa kizazi
kipya.
ni vyombo vichache sana vinavyotoa
nafasi ya kuweka hadharani kazi za
ushairi lakini vingi vimeipa kisogo
sanaa hii.
na inakuwa ngumu kuiweka wazi kwa
kuwa hata muhamko wa wasanii
wenyewe kuwa mdogo.
kwa kifupi,KUTUNGA TUMETUNGA
SANA NA SASA NI WAKATI
WAMABADILIKO,USHAIRI KWA FAIDA
YA JAMII NA MSHAIRI.
Idd ninga
. .. .
iddyallyninga@gmail.com