Wasanii acheni kulalamika kuibiwa kazi zenu na kukosa faida

Kalam mpya

Member
Mar 30, 2017
84
76
Wasanii hapa nchini either wamekosa elimu au wana elimu sana wamekosa maarifa au Life skills ya kazi zao.

Tutakubalina wote kwa pamoja kua wasanii wote kabla ya kutoa kazi zao midomo kwanza kabisa wanarusha ktk mitandao ya kijamii karibu yote.

Wakati wapo studio wanatambulisha kazi za midomo yao, Watanzania wote wanajua na tayari wameisikia au tayari wameshadukua kazi hizo na tayari wanazo majumbani.

Wanapotoka studio wanakuta kazi zao zipo kitaa mapema sana.

WEWE MSANII KWA HILI UNAMLAUMU MTU AU JILAUMU WEWE MWENYEWE?

Ile kazi ya msanii mmoja aliekamatwa na kuachiwa mimi sijawahi kuinunua hata kuishika, lakini nimeisikiliza vizuri kwa simu na computer.

Mnatafutaje mchawi wakati ninyi wenyeji wa wachawi wa kazi zenu?

Sidhani kama hamkuchukua njia mbadala ya kujisahihisha ktk kazi zenu mtapata faida, laah.

Sina ushahidi wakati ule mlikua na kazi nyingi leo uimbe tu upate milion 100 sijui. Pengine humo ndani ya mziki uuze na uji wa ulezi.

MKIDHIBITI HILO KURUSHA KAZI ZENU MITANDAONI MTAONA FAIDA. VINGINEVYO, ANZISHENI KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA MATUNDA
Mtaenda sawa.

POLENI WASANII WETU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom