Wasalimisha viroba vya 140 millioni

Wasalimisha viroba vya 140 millioni

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2016
Posts
212
Reaction score
720
Wafanyabiashara 13 wa Wilaya za Babati na Hanang’ Mkoani Manyara, wamesalimisha katoni 1,540 za pombe zilizofungashwa kwenye karatasi (viroba) zenye thamani ya sh140 milioni.

Wafanyabiashara hao walisalimisha katoni hizo za pombe za viroba kabla ya upekuzi ulioendeshwa na polisi, maofisa wa usalama wa Taifa, chakula na dawa (TFDA) na mamlaka ya mapato nchini (TRA).

Akizungumza jana na waandishi wa habari, kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Francis Massawe alisema wafanyabiashara hao walisalimisha wenyewe viroba hivyo bila kushurutishwa.

Kamanda Massawe alisema katika wilaya ya Hanang’ zilisalimishwa katoni 871 na kwa wilaya ya Babati zilisalimishwa katoni 669 na wafanyabiashara hao wanaopaswa kupongezwa kwa hatua hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Wenye viwanda si wangeitisha viroba vyote virudishwe ili wafanye packaging upya?wamekaa kimya tu watu wanapata hasara wakati waliuza mpaka siku ya mwisho!
 
Its true vingerudi factory kwa packaging mpya maana issue si ziwekwe kwenye chupa?
 
Hivyo viroba vilikuwa na nembo ya TBS na TRA?
 
Wenye viwanda si wangeitisha viroba vyote virudishwe ili wafanye packaging upya?wamekaa kimya tu watu wanapata hasara wakati waliuza mpaka siku ya mwisho!
Na hao walionunua hadi siku ya mwisho walikuwa wanategemea nn?
 
Nafikiri suruhisho pekee ambalo litapunguza hasara kwa wafanyabiashara ni Kwanzaa wenye viwanda kuitisha products zao kiwandani na kuipack kwenye chupa! Maana km Zanzi ,Konyagi, K vant Nk zipo za chupa.
 
Back
Top Bottom